SAFARI YA KIFO - SEHEMU YA SABA (MWISHO)
SIMULIZI: SAFARI YA KIFO SEHEMU YA MWISHO Alipomsogelea tu alipigwa ngumi moja nzito iliyomrusha pembeni na kumfanya ajibamize ukutani lilikuwa ni lile jitu moja ambalo lilibaki wakati huo yule mama naye alikuwa amefika na kisu chake. Tunaendelea Haraka haraka Michael mbabe alijiinua pale chini na kulifuata lile jitu hatari ili apambane nalo huku Ibrah akikwepa kisu cha yule mama na kumpiga kwa shoka la kichwa moja kwa moja kichwa cha yule mama kikaruka na kujibamiza ukutani huku mwili wa mama yule akitapatapa. Kibarua kizito kilikuwa kwa hili jitu lililobaki lilimpiga Michael ngumi nyingi za uso kisha likamuongeza na teke lililomtupa chini mbali kidogo Ibrah alirusha shoka yake ambayo ilikamatwa na lile jitu kwenye mpini wake kisha likafanikiwa kumpokonya Ibrah shoka ile na kuitupa pembeni. Ibrah alilipiga ngumi nyingi ambazo lilionesha wazi kuwa halisikii maumivu kisha lilkamkaba kooni na kumnyanyua juu Ibrah kwa kutumia mkono wake mmoja Michael Al...