SAFARI YA KIFO - SEHEMU YA PILI
SIMULIZI:
SAFARI YA KIFO
SEHEMU
YA PILI
"Kalenga?? Basi
mmekwisha"
Aliongea yule mlinzi huku akitoa
macho
"Kwanini uncle?!"
Aliuliza Ibrah kwa mshangao mkubwa.
Inaendelea…
"Mh! Kwa siku hizi za karibuni
nasikia kuna wanadamu wanaowala wenzao, sijui lakini yawezekana
imeshaisha" aliongea yule mlinzi huku akipokea shilingi 500 kutoka kwa Ibrah.
"Muhimu umtegemee mungu na
muwe makini sana," aliongezea kisha Ibrah akatamani amuhoji zaidi yule
mlinzi, lakini honi ya gari ilikuwa ikipigwa kuashiria kuwa safari imeanza.
Ibrah aliondoka kuelekea kwenye
gari huku akiwa na maswali mengi kichwani. Baada ya dakika 3 gari ikaanza
kuondoka baada ya wanafunzi wote kuwepo ndani ya gari.
"Hakikisha uliyekuwa naye
mwanzo,yupo ndani ya gari sawa?"
Aliongea yule lecture huku
akipapasa macho yake kuangaza kwa wanafunzi.
"Tupo woteeee ondoa gari
bwana" aliropoka yule mlevi ambaye Leo hakuwa amelewa sana.
Dereva aliondoa gari kwa kasi
maeneo ya ipogolo kuanza safari ya kuelekea kalenga.Baada ya saa na dakika 50
gari ile ilikuwa imeshafika maeneo yale
ya kihistoria..
"Wooow! So amazing
jamani"
"Yeah ni pazuri sana"
"Woow!" Wanafunzi tofauti
tofauti walikuwa wakiongea huku wakishuka ktk ile gari.
Wengine walikuwa wakipiga picha na
kufurahi.
Ibrah alishuka na kufuatwa na Leyla.
"Ibrah nisamehe kwa
kilichotokea Jana, nisamehe na pole sana mpenzi" Leyla alilegeza jicho la
huruma kumtazama ibrah,ambaye alionekana kutojali alichosema Leyla
"Ibrah, Michael anakuja tena
na wale wenzake" Raphael alisogea haraka kwa Ibrah na kumnong'oneza
sikioni.
Ibrah aligeuka na kumuona Michael
(yule mlevi) anakuja na wenzake, Michael alikuwa anaogopeka sana kutokana na
ubabe aliokuwa nao pale chuoni, hata mitaani walimfahamu pia.
"Leyla nadhani unamuona
Michael, sitaki ugomvi tena naomba uondoke". Ibrah aliongea kumwambia Leyla,
ambaye naye pia aligeuka kumtazama Michael ambaye alikuwa ameshawakaribia
"Hivi una nini wewe mpumbavu, nikwambie
mara ngapi kuwa sikupendi? Sikupendi we mkaka, lisura lako libaya kama roho
yako ilivyo mshenzi mkubwa wewe! moyo wangu upo kwa Ibrah. Hivi kwanini
unapenda kumuonea kwasababu ya upole wake?"
Leyla alifoka kumfokea Michael,
ambaye alitabasamu tu na kumbusu Leyla.
"Mjinga wewe" Leyla
alifoka na kumtemea mate Michael, kisha akampiga kofi kali la shavu.vijana wa
Michael walitaka kumpiga Leyla, lakini Michael aliwazuia na kuwaambia wasimguse
mpenzi wake.
"Kuna nini hapa? Mbona kama
mnagombana?" Lecture alisogea mahala pale na kuuliza.
"Ah hapana tulikuwa
tukibishana kuhusu hapa kalenga tu. ni maswala ya academic sir."
Alijitetea Michael na kumfanya
Leyla aachie msonyo wa hasira.
"Mh! kama maswala ya taaluma
si mtayapata ndani, sasa mnabishana nini? Haya sogeeni kwa wenzenu kule". lecture
alitoa maelekezo, kisha Leyla akamkumbatia Ibrah na kuondoka naye.
Michael alikasirika sana, ila
hakuwa na namna naye akaondoka na wenzake.
" Nina wanafunzi 32 tu"
aliongea lecture kumwambia mtu wa malipo pale kalenga..
"Usijali karibu sana".
Kisha akapokea hela na kuzihesabu.
"Mnaweza kunisubiri hapo
nje".
Aliongea na kuingia ndani.
Baada ya dakika 5 alitoka na kuanza
kuwapeleka ktk maeneo mbalimbali ya kihistoria huku akiwaelezea kwa undani.
Wanafunzi walijifunza mpaka raha, walipiga
picha kila kitu isipokuwa fuvu la mkwawa ambalo waliliona bila kulipiga
picha.walifurahi sana na picha zilikuwa za kutosha sana. Baada ya masaa mawili,
kila kitu kilikuwa kimeisha, kisha wanafunzi wakawa wanapiga picha tu.
Raphael alichukua simu yake aina ya
Samsung kisha akasogea na kupiga picha za kamera ya mbele(selfie) pamoja na
Leyla na Ibrah. Leyla naye hakuwa nyuma,alitoa I-phone yake kisha wakaendelea
kupiga picha.
"Simu yako ipo wapi
wewe?" Raphael alimuuliza Ibrah
"Ah ipo kwenye
begi,nimelisahau ndani ya gari" Ibrah alijilaumu kisha wakakubaliana kuwa,
ndani ya gari kuna usalama waondoe hofu tu. walipiga picha za mapozi tofauti. Mara
Ibrah amshike kiuno Leyla, Mara wanyonyane lips, Mara sijui madenda ya shingo
n.k. ilikuwa ni furaha isiyo na mfano.
Upande mwengine Michael na wenzake
walikuwa sehemu nyingine wakinywa pombe kwa msongo wa mawazo waliokuwa nao,
"Hivi yule mtoto anajiamini
nini kunichukulia demu wangu?" Aliuliza Michael
"Kilichobaki ni kumuuwa tu. anajiendekeza"
alitoa wazo rafiki yake mmoja Michael japo halikuungwa mkono, kisha
wakakubaliana apate mateso mpaka atakapomuacha Leyla. Walijiinua taratibu
kuelekea kwenye gari waliyokuja nayo.
"Wanafunzi malizieni kupiga
picha tuondoke" lecture aliongea huku akimshukuru yule aliyewapokea.
Wanafunzi walipotosheka walianza
kurudi katik gari.Leyla, Raphael na Ibrah walipendeza sana na mpigaji picha
alikuwa ni Raphael, huku leyla na Ibrah wakiwa katika mapozi ya mahaba mazito,
Basi wote walirudi katika gari, kila
mtu akimsimulia mwenzake kuhusu waliyofanya huku wakioneshana picha walizopiga.
"Gari imeisha mafuta, ngoja
tutafuta kijiji hapo tutulie ili tutafute mafuta maana sheli ipo mbali
kidogo" dereva aliongea,huku wanafunzi walianza kulalamikia dereva na
kumtusi.
“Msinilaumu mimi sasa, nawapa
msaada katika hiko kijiji ili nikichukua mafuta tuondoke bado mnakataa Basi ondokeni
na gari yenu mnayoijua" dereva alifoka na kufanya wanafunzi wote wawe
kimya.
"Unajua huko tunapoenda,
siamini kama kuna usalama kabisa." Ibrah alinong'ona kumwambia Raphael
"Kwanini Ibrah" Raphael
aliuliza kwa mshangao mkubwa
"Unamkumbuka yule mlinzi wa
mabafu kule ipogolo?"
"Ndio"
"Aliniambia kuwa huku kuna
watu wanakula nyama za watu"
Wakati wanaongea hayo, ghafla kuna gari
ikasimama pembeni ktk kimsitu kidogo.
"Dereva vipi weweeeee?"
Wanafunzi walilalama kumwambia
dereva.
“Shukeni hapa tutakaa Leo, alafu
kesho tutaenda katika kijiji cha jirani ili tupate msaada wa mafuta"
dereva aliongea kisha akawa wa kwanza kushuka.
"Sasa wengine hatujala jamani
aah!" Mwanafunzi mmoja alilalama na kuungwa mkono na wenzake
"Kweli kabisa hatujala jamani aah!"
"Mnalalamika nini nyie, ule si
mgahawa ule? Au sio?" Aliongea mwanafunzi mwengine huku akinyoosha kidole
chake pembezoni kwa Barabara.
Wanafunzi walikimbaza kisha
wakavuka Barabara na kuingia mule ndani.
"Shikamoo!shikamooo!shikamoo
mama" zilikuwa ni salamu nyingi sana za wanafunzi waliojazana mule ndani, wengine
wakiwa nje
"Marahaba wanangu
karibuni"
"Asante naomba chapati 3 na
supu!" Aliongea Michael mbabe,
"Mimi nipe chapati 2 na
chai" aliongea rafiki yake Michael huku wengine nao wakiagiza oda zao.
Supu ya Michael ilikuwa ya kwanza
kufika na aliyeileta alikuwa ni mtu aliyejifunika uso wake kwa koti refu la
kofia (prova).
Michael alivyoutazama vyema USO wa
yule mtu aliona kuwa USO wake umejaa damu zilizogandiana huku akiwa anatisha. Mara
yule mtu akaondoka na kuelekea jikoni, Michael alihisi labda ni pombe zake ndio
zinamchanganya, alitulia kwa dakika 5 bila kula, ambapo alishtuliwa na rafiki
yake
"Oya kula mwamba, tukamuwahi
mchumba wetu Leyla". Michael akaanza kula, mara akaona kidole cha mtu kwenye
ile supu, akaimwaga na kusimama kwa hasira.
Je,Michael mbabe atafanya nini Leo
na ubabe wake wote?
Itaendelea
Kesho Saa 12
Jioni
Very nice indeed
ReplyDelete