SAFARI YA KIFO - SEHEMU YA SABA (MWISHO)
SIMULIZI: SAFARI YA KIFO
SEHEMU YA MWISHO
Alipomsogelea
tu alipigwa ngumi moja nzito iliyomrusha pembeni na kumfanya ajibamize ukutani lilikuwa
ni lile jitu moja ambalo lilibaki wakati huo yule mama naye alikuwa amefika na
kisu chake.
Tunaendelea
Haraka
haraka Michael mbabe alijiinua pale chini na kulifuata lile jitu hatari ili
apambane nalo huku Ibrah akikwepa kisu cha yule mama na kumpiga kwa shoka la
kichwa moja kwa moja kichwa cha yule mama kikaruka na kujibamiza ukutani huku
mwili wa mama yule akitapatapa.
Kibarua
kizito kilikuwa kwa hili jitu lililobaki lilimpiga Michael ngumi nyingi za uso kisha
likamuongeza na teke lililomtupa chini mbali kidogo Ibrah alirusha shoka yake ambayo
ilikamatwa na lile jitu kwenye mpini wake kisha likafanikiwa kumpokonya Ibrah shoka
ile na kuitupa pembeni. Ibrah alilipiga ngumi nyingi ambazo lilionesha wazi
kuwa halisikii maumivu kisha lilkamkaba kooni na kumnyanyua juu Ibrah kwa
kutumia mkono wake mmoja Michael Alikuja na shoka lake kisha akaukata mkono wa
lile jitu kwa hasira, likamuachia Ibrah
huku likipiga kelele za maumivu. Michael aliinama kukwepa ngumi iliyotaka
kumpiga kisha akaliongezea kwa kulipiga shoka la goti.Jitu lilipiga magoti
chini kisha Michael mbabe akaliongeza na shoka la mgongo ambalo lilibaki pale
pale mgongoni.
Jitu
lilipiga kelele na kudondoka chini Ibra alikuwa ameshasogea kumfungua Leyla kisha
wakakumbatiana na kuanza kunyonyana ndimi zao, Michael aliumia rohoni ila
alifurahi pia baada ya kumuona leyla akiwa salama.
Baada
ya kama dakika 3 za kunyonyana bila kuongea leyla akavunja ukimya
"Asante
sana Michael, " Alimsogelea Michael na kumkumbatia kwa Mara ya kwanza
tangu wajuane. Chozi la furaha lilomtoka Michael akiamini ile ndoto yake ya
kutochukiwa na Leyla imeisha.
Mara
ghafla wakiwa wamekumbatiana Michael alimbadili Leyla upande kisha akapigwa
shoka la shingo na lile jitu ambalo lilikuwa halijafa vizuri.
Ibrah
alipiga kelele nyingi za hasira kisha akaokota shoka lingine na kuufumua ubongo
wa lile jitu Aliliponda ponda kwa hasira huku akilia
"Michael
hapana Michael amka amka hufi wewe Nimeshampoteza Raphael, ulibaki wewe
Michael. Wewe Michael tafadhali usituache" Ibrah aliongea kwa mfululizo
huku akilia kwa kwikwi.
Leyla
alikuwa akilia balaa,
"Michael
usiondoke Michael, Michael kama unanipenda usife basi Michael"
Michael
aliwatazama kwa jicho legevu kisha akasema
"Nakupenda
Leyla," kisha akafumba macho na kufariki.
Leyla
alimtikisa Michael huku akimwambia
"Nakupenda
pia Michael, amka basi, amka kama unanipenda, Michael....."
Alilia
sana Leyla alikumbuka siku ya 1 anakutana na Michael chuo kipindi hiko Michael
alikuwa mbabe kweli na mwenye roho mbaya lakini akiwa kwake Leyla basi michael
anakuwa mpole, akakumbuka jinsi ambavyo Michael alikuwa akimtetea pale ambapo
alikuwa akionewa au akisumbuliwa na wavulana Michael alihakikisha kuwa Leyla hapati shida yoyote pale chuoni alianza kunywa
pombe baada ya Leyla kumtamkia kuwa
hampendi na ana mtu wake ambaye ni Ibrah alikumbuka jinsi Michael alivyokuwa
akimpa pesa Mara kadhaa huku yeye akizikataa pesa zile,
Alikumbuka
walivyokuwa kwenye gari kuja ktt study tour Jinsi Michael alivyokuwa ana furaha
wakati huo Ibrah alikumbuka siku aliyopigana na Michael kule stendi kwasababu
ya mpenzi, akakumbuka siku ya 1 anamuokoa Michael na baadae wanashirikiana
kumaliza maadui zao hadi Leo hii wamefika hapa Ibrah naye alilia.
Walimuacha
pale pale Michael kisha wao wakashikana na kutoka nje kisha wakasimama pale
kusubiri gari ili waombe msaada.
Baada
ya dakika 40 Ibrah akiwa amekilaza kichwa cha leyla ktk bega lake walifanikiwa
kuliona gari moja likipita ktk Barabara hiyo Ibrah alisimama haraka na
kuipungia mkono isimame lakini iliwapita Baada ya dakika 5 ile gari ikarudi
"Mwanzo
nilihisi ni vibaka bwana ndipo mke wangu akasema aliwaona vizuri hivyo turudi
kuwachukua pandeni twende" aliongea mzee mmoja wa makamo aliyekuwa
akiendesha gari.
Walishushwa
Iringa mjini kisha wakatafuta mahala ambapo kituo kikuu cha polisi kinapatikana
wakatoa taarifa na maelezo ya kila kitu kilichowakumba polisi waliifuatilia ile
kesi na kutoa taarifa chuo pamoja na kwa wazazi wa wanafunzi wale huku
utaratibu wa kuzikwa ukifanyika Ibrah na Leyla walirudishwa Daresalaam, japo
chuo lilikuwa ktk majonzi makubwa sana, lakini Ibrah na Leyla walipewa pongezi
na zawadi nyingi sana pale chuoni zikiwemo fedha.
…BAADA YA
MIAKA 2…
Leyla
na Ibrah walimaliza chuo na kufunga ndoa kama mke na mume wakabahatika kupata
mtoto wa kiume, kisha wakampa jina la Michael, shujaa ambaye hawatokuja
kumsahau ktk maisha yao.
Maisha
mengine ya furaha yaliendelea, haikusikika tena kuwa sehemu ile wanakula watu watu
walihamia na kujenga makazi yao na Amani ikarejea.
*MWISHO*
Comments
Post a Comment