SAFARI YA KIFO - SEHEMU YA TANO


 

SIMULIZI: SAFARI YA KIFO

 

SEHEMU YA TANO

Mara ghafla Ibrah akatazama ktk mti mmoja kisha wakagongana uso kwa uso na lile jitu ktk mti lililoanza kukimbia.

 

Tunaendelea…

"Leo hutukimbii mwanaharamu wewe" Alifoka Michael mbabe kwa hasira kisha akaanza kulifukuza Ibrah hakuwa nyuma naye akaungana na Michael kwa pamoja kulifukuza.

Leyla alikuwa akilia sana, baada ya mpenzi wake Ibrah kujitosa lakini Raphael alimtia moyo na kumuahidi kuwa Ibrah atarudi tu leyla hakutaka kukubali hata kidogo alikuwa akilia tu na kupiga mayowe.

"Jamani hakuna haja ya kuwasubiri hapa wao safari hii hawawezi kupona kabisa.Wameshajitolea kufa hivyo sisi tukatafute msaada kijiji cha pili." Aliongea Joseph ambaye alianza kusimama na kuwasihi wenzake kuondoka.

Hakuna aliyemuunga mkono hata mmoja kisha akaanza kuondoka peke yake lakini kabla hajafika mbali alipigwa mshale wa koromolo kumbe katika wale vijana sita waliobaki kule waligawana kazi kuwa wengine washambulie huku na wengine kwengine. wanafunzi walisimama kwa hamaki huku wakitazama mahala ambapo mshale umetokea.

Upande mwengine Michael mbabe na Ibrah walimfukuza yule kiumbe kisha wakafika sehemu ambapo yule mtu aliwapotea kimiujiza.

"Muhimu kuwa makini Michael, hawa viumbe wana akili nyingi kuliko maelezo ukitumia hiyo hirizi yako unawaona wangapi waliopo karibu" Ibrah alimuuliza Michael mbabe huku wote wakiwa makini na tayari kwa lolote lile.

" wapo watatu" Alijibu Michael mbabe huku akiigusisha hirizi yake katika kifua chake.

Ghafla kuna kisu kilirushwa ambacho wote kwa pamoja walikikwepa na kwenda kupiga mti.

"Tazama kule" Michael alisema kumuonesha Ibrah upande ambao wale viumbe watatu walikuwa wanatokea  mmoja alikuwa akija kwa kukimbia bila silaha lakini wawili walikuwa wanatembea, ambapo mmoja alikuwa na kisu huku mwengine akiwa na mashine ya kukatia miti (chainsaw) ikiwa imewashwa..

Walitazamana wote wawili kisha Michael akaibusu ile hirizi yake Mara ya mwisho na wao wakaanza kumkimbilia yule kiumbe aliyekuwa akiwafuata.

Upande mwengine wale wanafunzi wote walipigishwa magoti na yule mama wa mgahawa akiwa na vijana wake wa kazi wawili ambao mmoja wao anatumia silaha ya mshale huku mwengine akiwa mikono mitupu.

"Mmekula ktk mgahawa wangu mkaondoka bila kunilipa si ndio ninyi?" Aliuliza yule mama wa mgahawa kwa kejeli.

"Mwenzenu aliwaambia wazi kuwa mgahawa wetu tunauza nyama za watu mkamuona chizi si ni nyie?" Aliongea huku akimsogelea Raphael aliyekuwa amemkumbatia Leyla.

"Binti unaonekana kuwa una nyama tamu sana wewe" alimwambia vile Leyla huku leyla akiwa anatetemeka kwa woga.

Alimvuta leyla kwa mikono yake kisha Raphael akainuka ili akamzuie yule mama lakini cha kuhuzunisha Raphael alipigwa mshale mgongoni mwake alipojaribu kuinuka tena alipigwa mshale wa pili kisha akadondoka kama mzigo.

Wanafunzi walipiga kelele nyingi sana za woga kisha yule mama akaamuru wanafunzi wote wale wauwawe.

Upande mwengine lile jitu lilipigwa ngumi nzito ya tumbo na Michael mbabe, kisha kabla hajakaa sawa alipigwa teke la shingo na Ibrah ambalo lilimtupa pembeni. Mvua ilianza kunyesha huku radi nazo zikianza kupiga ikiwa inaelekea alfajiri ya siku inayofuata, Ibrah alinyanyua jiwe lililopo chini kwa mguu wake na kulirusha kwa Michael mbabe, ambaye alilidaka na kumbamizia kichwani yule kiumbe ambaye aliinuka alipodondoka na kuwafuata na pale pale alimpasua kichwa na kumuua.

Yule kiumbe mwengine mwenye kisu alikuwa ameshafika nae alirusha mkono ambao Michael aliudaka na kumchota mwili mzima yule kiumbe kisha akamdondosha chini kwenye tope na kuanza kumpiga ngumi mfululizo za usoni.

Ibrah naye hakuwa nyuma alikuwa amezuiwa mshikio wa ile mashine ya kukatia miti ili aizuie isimkate. Alimpiga teke la sehemu za siri yule kiumbe ambaye aliiachia ile chainsaw kisha Ibrah bila kuchelewa akamuongeza tele lingine la tumbo ambalo lilimtupa pembeni, kisha akaikoto mashine ile na kumkata kichwa yule kiumbe pale chini alipodondokea.

Michael naye alimpiga ngumi nyingi za usoni yule kiumbe mwengine ambaye hakuonesha dalili za kufa yule kiumbe alimgeuza Michael na kuanza kumshushia kichapo huku akiokota kisu chake na kutaka kummaliza kabisa Michael Lakini kabla hajaokota kisu alisikia mlio wa mashine ya chainsaw karibu yake, na alipogeuka kutazama tu alipigwa nayo ya shingo.

Upande wa pili, wanafunzi wote waliuwawa hakuna hata mmoja aliyebaki kisha yule mama akaondoka na Leyla ili ampeleke ktk mgahawa wake.

Ibrah na Michael mbabe waliinuana taratibu, huku mvua ikizidi kuwa kubwa,kisha wakaanza kurejea kule walipowaacha wenzao.

Iliwachukua takribani nusu saa kuweza kufika lile eneo lakini kwa mbali waliwaona wenzao wakiwa wamelala. Michael na Ibrah wakianza kukimbia kichovu ambapo walikuja kubaini kuwa wenzao wote walishauwawa

Ibrah alikuwa akiitafuta maiti ya Leyla hakuiona ila alifanikiwa kumkuta Raphael akiwa hajakata roho vizuri.

"Raphael, nambie nini kimetokea"

Ibrah aliuliza kwa mshangao huku akianza kububujikwa na machozi

"Mimi niache Ibrah, nimeshakufa muhimu kamsaidie Leyla Leyla  ambae wamemchukua nisamehe sana kwa kushindwa kumtetea ila usifanye makosa niliyofanya Mimi tena". Kisha akapoteza Maisha hakusema kuwa wamempeleka wapi Leyla.

Alilia sana huku akikumbuka jinsi walivyokuwa wakicheza yeye na Raphael tangu wakiwa wadogo,

"tumezaliwa mwaka mmoja, tutaoa pamoja na kufa pamoja" ilikuwa ni kauli ya Raphael kipindi wakiwa wadogo alikumbuka kipindi wamechagua chuo kimoja huku Raphael akiwa ndiye mtetezi wake mkubwa alipoonewa pale chuoni. Alikumbuka jinsi Raphael alivyomtongozea kwa Leyla ambaye kwa sasa ni wapenzi.

Alikumbuka walivyokuwa ktk gari, kelele za wanafunzi wenzake laiti wangejua kuwa safari yao ilikuwa ni SAFARI YA KIFO Basi wasingekuja kabisa alimkumbuka lecture wao aitwaye Abasi ambaye waliookuwa darasani alikuwa akiwachekesha sana machozi mengi yalimtoka huku akipiga kelele.

Michael alimsogelea Ibrah na kumshika bega huku naye akilia.

"Wameondoka na Leyla akiwa hai" Ibrah alimwambia Michael mbabe ambaye sasa akili yake ilivurugwa macho yalibadilika na kuwa nekundu mishipa ilimsimama kisha aka

 

Je,akafanyaje sasa bwana Michael mbabe mtaalamu huyu ambaye hataki ucheze na Leyla.

 

 

Itaendelea

Kesho Saa 12 Jioni

Comments

Popular Posts