SAFARI YA KIFO - SEHEMU YA SITA

SIMULIZI: SAFARI YA KIFO

SEHEMU YA SITA

"Wameondoka na Leyla akiwa hai"

Ibrah alimwambia Michael mbabe ambaye akili yake ilivurugwa, macho yalibadilika na kuwa mekundu, mishipa ilimsimama kisha aka

 

 

Tunaendelea

Michael mbabe aliapa kuwa atauangamiza kila mkono utakaomdhuru leyla hata kwa kumpiga Kofi tu.

Alisimama na kuanza kuondoka bila kusema tena chochote.

"Unaenda wapi?!" Ibrah aliuliza

"Naenda kumtoa leyla katika mikono ya hawa washenzi wauwaji." Michael alijibu na kuanza kuondoka.

"Unajua mahala walipompelekea" Ibrah aliuliza tena

"Sijui itajulikana huko huko." Alijibu Michael na kuongeza hatua.

"Subiri kwanza" Ibrah alimshika mkono kumzuia Michael ambaye aligeuka na ngumi nzito iliyomkosa Ibrah baada ya kuikwepa,

"Nimekwambia niache lasivyo nitaanza na wewe" Michael alizungumza akiwa amechanganyikiwa.

"Michael hupaswi kuwa na jazba tulia tufanye mipango kwa akili" Ibrah aliongea

"We mjinga nini kwahiyo kumuokoa leyla sina akili?" Michael aliongea kwa hasira akiwa amakunja ndita zake kisha akamsomgelea Ibrah na kuanza kupigana wao kwa wao.

Michael alikuwa na ngumi nzito wakati Ibrah alikuwa mwepesi hivyo Michael alijikuta akichakazwa na kijana mdogo Ibrah.

Wakati wanaendelea kupigana ghafla Ibrah akapigwa mshale wa mguuni wakati anashangaa nani aliyempiga mshale Mara ghafla kuna mshale ulimkosa kosa Michael na kupiga kwenye mti.

Waliachana kisha wakageuka na kumuona yule mtu wa ajabu anayetumia mshale.

"Nilijua tu kuwa kuna watu hawajafa na watarudi hapa ili kukitafuta kifo kama wenzao" aliongea yule mtu ambaye ktk mdomo wake alikuwa na meno yaliyooza na baadhi ya mapengo.

"Hawa washenzi wengine tumewauwa kwa shida sana ila mama akasema kuwa mwenye nyama nzuri ni binti mmoja hivi na sio hawa" aliongea yule mtu na kumfanya Michael mbabe apatwe na hasira kisha akaanza kukimbia kumfuata yule mtu huku ibrah akiuchomoa ule mshale naye akaanza kukimbia taratibu kumfuata kule kule.

Yule mtu alitabasamu na kuuvuta vyema mshale wake alimkita mshale wa mguu mwengine Ibrah kisha akamuongeza na mshale wa bega la kulia.

Wakati huo Michael alimkaribia yule mtu na kumpiga teke zito la kifua alikuwa hawezi kupigana zaidi ya kutumia mshale Michael alimpiga sana ngumi za kutosha kisha akaanza kumburuza mpaka alipokuwepo Ibrah alichukua kisu na kumkabidhi Ibrah amchinje yule mtu.

"Umemuuwa Raphael rafiki yangu umeuwa marafiki zetu wengine mkamteka na leyla wangu mshenzi wewe nakuuwa sasa" Ibrah bila kuchelewa alimchinja wazi wazi yule mtu wa ajabu kisha naye akapoteza fahamu.

Alikuja kuzinduka akiwa ktk kitanda cha nyumba moja ya udongo akiwa amepona kabisa majeraha yake,

Alipotazama pembeni alimuona Michael akiwa yupo ktk msongo wa mawazo.

"Michael, tupo wapi?!"

Aliuliza kwa sauti ya kunong'ona.

"Tupo kwa bibi usijali nimejaribu kupiga simu nyumbani lakini simu hazipatikani yani tangu gari lilipoharibika siku zile mpaka sasa mtandao huku haukamati kabisa." Aliongea Michael

Mara akaingia bibi mmoja aliyekuwa ameshika kichupa cha dawa na kumuamuru Ibrah anywe Ibrah alikunywa kwani yule bibi ndiye aliwasaidia baada ya kupita ktk lile pori akiwa anatafutw dawa alituaona na kutusaidia.

"Huku ni kubaya sana na ni hivi karibuni tu ndipo watu wanakula nyama za watu haikuwahi kutokea kabisa yani" Yule bibi alianza kuongea

" ila nitawasaidia silaha kama ambavyo mwenzako(Michael) aliniomba mkamuokoe huyo mwenzenu ambaye mnadai kuwa wamemteka" aliongea yule bibi huku akiwapa Mashoka mawili na kuwaambia kuwa Yale sio Mashoka ya kawaida hivyo anawatakia kila la heri ktk safari yao kabla hawajaondoka walikula chakula na kufurahi kwa pamoja kisha wakaanza safari mpaka ktk ule mgahawa.

"Leo ama tufe sisi ama wafe waoi la lazima leyla tumuondoe akiwa mzima" Michael alimwambia ibrah kisha wakaubamiza ule mlango kwa shoka zao na kuingia ndani moja kwa moja.

"Leyla," Michael aliita baada ya kumuona leyla akiwa kafungwa kamba mikononi na mdomoni.

Alipomsogelea tu alipigwa ngumi moja nzito iliyomrusha pembeni na kumfanya ajibamize ukutani lilikuwa ni lile jitu moja ambalo lilibaki wakati huo yule mama naye alikuwa amefika na kisu chake

 

 

Naam,nini kitaendelea sasa,nani afe nani abaki?!

Itaendelea

Kesho Saa 12 Jioni

 

 

 

 

Comments

Popular Posts