SAFARI YA KIFO - SEHEMU YA TATU

 


SIMULIZI: SAFARI YA KIFO

 

SEHEMU YA TATU

"Oya kula mwamba tukamuwahi mchumba wetu Leyla". Michael akaanza kula, Mara akaona kidole cha mtu kwenye ile supu, akaimwaga na kusimama kwa hasira.

 

Tunaendelea…

" ushenzi huu mnatulisha nyama za watu" kauli ile ilimshitua sana ibrah na Raphael kwani wao walishastukia ile hatari mapema.

"Msile vyakula vya hawa washenzi, ni wachawi hawa" Michael alipiga ngumi katika ile meza iliyoweka chakula, kisha meza ikavunjika kwani ilikuwa imeshachoka, isitoshe alikuwa na ngumi nzito sana.

Wanafunzi waliacha kula na kuangalia kile alichosema Michael kama ni kweli, kisha wakabaini kuwa ulikuwa ni miguu wa kuku na sio kidole cha mtu kama asemavyo Michael

"Jamani pombe mbaya, huu si mguu wa kuku?" Alisema mwanafunzi mmoja huku akiushika ule mguu. wanafunzi wengine wakaanza kumcheka Michael na kudai kuwa zilikuwa pombe tu, Michael alikuwa anaona kila kitu, kwasababu shingoni mwake alivaa hirizi iliyokuwa ikimuonesha mambo ya kichawi. alisimama kwa hasira na kuuliza "Yupo wapi Leyla?"

Leyla alikuwa nje mlangoni na kina Ibrah wakila chapati na chai, Alifoka nje kwa hasira na kumsogelea Leyla

"Hii sehemu sio salama hata kidogo ila siwezi kuruhusu uumizwe na mshenzi yeyote hapa, maana hapa mimi mwenyewe mshenzi kweli kweli nitauwa kila mtu atakayetaka kukudhuru"

Michael alikuwa ameshaanza kuchanganyikiwa kwa Yale matukio.

"Na wewe mbwa kaa mbali na Leyla nitakuuwa" alimgeukia Ibra na kumwambia hivo

"Kwani Leyla anampenda nani kati yetu? Kama vipi huyo hapo aseme" Ibrah safari hii aliongea kwa kujiamini kiasi.

"Niseme nini tena mimi, sikupendi Michael sikupendi nakuchukia" Leyla aliongea vile, kisha Michael akarusha ngumi nzito kuelekea kwa Ibrah ambaye aliinama na kuikwepa, kisha Michael akapitiliza kama mzoga bila breki.

"Unataka kupigana na mimi we mpumbavu? Leo nakuuwa sasa" Michael aliongea hivyo huku wanafunzi wote wakitoka nje na kuutazama ule mpambano, ambapo Michael alikuwa akihema mithili ya simba dume mwenye njaa kali. Ibrah naye alikunja ngumi zake tayari kwa mpambano.

"Acheni ujinga nyie watoto, gari limeharibika badala tujue tunatokaje alafu nyie mnapigana! Nilipata taarifa zenu tangu ipogolo kuwa mlipigana na huku mnafanya hiyvo hiyvo mbona mnanitia aibu"?! Lecture alifoka huku akimsogelea Michael na kumpiga Kofi katika shavu lake.

" tena wewe na mapombe yako ndio mkorofi". Michael alianza kutokwa na chozi katika jicho lake baada ya kubaini kuwa ni kweli mapenzi hayalazimishwi kama anavyofanya kwa Leyla, japo alikuwa anampenda sana Leyla lakini hakuwa na sababu ya kugombana na Ibrah. Alisogea pembeni na kuvuka Barabara kisha akaenda katika gari na kuchukua begi lake. Wanafunzi wengine walikuwa wakimtazama tu. Alitoka na kuchukua visu viwili ambapo watu walijua moja kwa moja, atamchoma mtu au kujiua binafsi.Alimsogelea Ibrah ambaye hakuwa na hata chembe ya wasi wasi

"Shika..." Alimpa kisu kimoja Ibrah na kumwambia

"Tumia hiko nami nitumie hiki ili tumtoe salama Leyla mahala hapa, maana sio salama"

Wakati wanafunzi wanashangaa mara ghafla yule muhudumu aliyekuwa amejifunika kwa koti (prova) alitoka nje na kumchomeka yule lecture kisu cha shingo, damu zilikuwa zikiruka kama kuku aliyechinjwa na kusababisha wanafunzi waliobaki waanze kukimbia huku wakipiga makelele.

Ibrah alimshika mkono Leyla na kwa bahati nzuri wanafunzi wote walikimbilia sehemu moja tu katika ule msitu.

"Simameni hapa" Michael mbabe aliwaamuru wenzake wasimame, kisha wakatii

"Mimi niliwaambia kuwa ule mgawahawa wanakula nyama za watu, hamkunielewa nadhani mmeona sasa jinsi ambavyo lecture Abasi alivyochinjwa kama kuku mbele yetu." Alisema huku akihema akiwa ameshika kisu chake.

"Sikilizeni, nyinyi msiondoke hapa. Mimi na Allen tutaondoka tukapambane ili tujihakikishie usalama wetu, mliobaki mtulie hapa hapa. mpo wengi hawezi kuwadhuru mmeelewa?" Alitoa maelekezo hayo Michael mbabe akiwa na rafiki yake mmoja aitwaye Allen.

"Tulieni mtuombee kwa mungu turudi salama, haniwezi yule mpumbavu. Naenda kumuuwa sasa" aliongea huku akimtazama Leyla aliyekuwa amemkumbatia Ibrah, kwa jicho la huzuni lililojaa wivu kabisa kisha yeye na Allen wakaondoka.

Wanafunzi wa kike walikuwa wakilia tu, huku wachumba zao wakiwabembeleza. vilio vilitawala wakidhani kuwa wameshakufa, walipiga simu kwao lakini hakukuwa na mtandao kabisa, wingu la mvua nalo likaanza kutanda jioni ile.

Walishuhudia Allen na Michael mbabe wakipotelea kwenda kupambana kwaajili yao.

"Raphael...." Ibrah alimuita Raphael kwa sauti ya upole.

"Naam Ibrah" Raphael alimsogelea Ibrah alipokuwa amekaa yeye na leyla, kisha Ibrah akamnong'oneza Raphael sikioni.

"Najua kuwa kina Michael hawawezi kurudi salama, acha nikawasaidie nadhani unaujua uwezo wangu? hivyo usiwe na shaka. baki na leyla hapo hakikisha usalama upo, Mimi nitarudi tu, usimwambie ukweli leyla." Kisha Raphael akatikisa kichwa ishara ya kukubali, huku akimkumbatia Ibrah na kuanza kudondosha machozi.

"Nakutakia kila la heri kaka" Raphael aliongea kisha Ibrah akainuka na kumwambia leyla kuwa anaenda kukojoa Mara moja, hivyo amsubiri

"Bora ukojoe hapa jamani, huko hakuna usalama kabisa" Leyla alimzuia Ibrah lakini alishindwa, Ibrah aliwadanganya wenzake kuwa anaenda kukojoa tu, kisha akawafuata kina Michael akawasaidie.

Michael mbabe na Allen walikuwa wameshafika mbele ya ule mgahawa.

"Shika kisu dogo Mimi najiweza bila kutumia kisu muhimu kutumia akili nyingi zaidi ili tumuue huyu kahaba" Michael mbabe aliongea huku akiangaza angaza katika ule mlango, akisubiri yule mtu atoke ili wapambane naye.

" Toka nje mshenzi wewe, toka utuuwe na sisi," aliongea kwa jazba,

Mara mlango ukafunguliwa na akatoka yule jamaa mwenye koti refu la prova huku akiwa ameshika kisu chenye damu.

Michael mbabe na Allen walitazamana na kutikisa vichwa vyao, kisha kwa pamoja wakaanza kumfuata yule mtu kwa hasira huku wakipiga makelele.

"Aaaaaaahhhhhhh........."

Yule mtu alirusha mkono wake ili amchome kisu Michael, lakini Michael aliinama chini kukwepa na kumpiga ngumi nzito ya tumbo yule kiumbe, kabla hajakaa sawa aliinuliwa na ngumi nzito ya uso wake unaotisha na kijana Allen kisha yule mtu akadondoka chini.

"Allen wahi" Michael aliongea kwa sauti kali, kisha Allen akamkimbilia yule mtu pale chini na kuanza kumchoma visu vingi vya tumbo mpaka alipounyofoa utumbo wa yule mtu.

"Aaahh!" Allen alishusha pumzi nzito,kisha akainuka na kumfuata Michael mbabe huku wakikumbatiana kwa muda kidgo

"Allen hapana,haiwezekani" Michael mbabe aliongea huku amemkumbatia Allen

"Hapana nini?" Allen aliuliza na kugeuka nyuma alipokuwa akitazama Michael. Kisha akamuona yule mtu wa ajabu amesimama huku ameshika kisu chake.

Allen na Michael hawakuamini wanachokiona,kwani walijua wazi kuwa kazi imeshaisha..

Walianza kumkimbilia yule mtu kwa lengo la kummaliza,Michael mbabe aliruka juu na kurusha ngumi ya uso iliyozuiwa na mkono wa yule mtu,kisha akapigwa ngumi ya shavu iliyomrusha pembeni Allen alipomsogelea yule mtu, alishikwa mkono wake wenye kisu na kunyongwa, kisha akakiachia kile kisu kwa maumivu ya kunyongwa mkono, alipigwa ngumi mbili nzito usoni huku damu zikianza kumvuja.

Wakati Michael mbabe anajiinua pale chini, alishuhudia Allen akichomekwa kisu cha koromelo lake huku damu zikianza kumtoka.

Kichaa kilimpanda Michael mbabe kisha akaanza kulipiga ngumi za uso lile jitu ambalo lilionesha kutosikia maumivu hata kidogo, alimpiga mpaka akachoka yeye mwenyewe. yule mtu alimpiga Michael ngumi moja nzito ya tumbo, iliyomrusha katika ukuta wa ile nyumba. Michael alishindwa kuinuka pale chini, kisha akawa anaona yule mtu anamfuata ili naye aje ammalizie tu, Michael alikata tamaa ya kuishi kabisa alijua pale ndipo atakapokufa ghafla akashangaa lile jitu lilipomkaribia limedondoka huku likivuja damu kichwani. Aliinua macho yake kuangalia aliyekuja kumsaidia na wala hakuamini macho yake

Je,ni nani aliyemsaidia Michael mbabe asiuliwe?

Itaendelea

Kesho Saa 12 Jioni

 

Comments

Popular Posts