SAFARI YA KIFO - SEHEMU YA KWANZA
SIMULIZI:
SAFARI YA KIFO
SEHEMU
YA KWANZA
Katika gari aina ya kosta,
wanafunzi wengi wa chuo ambao walipanda humo ndani yake,walikuwa wakipiga
makelele.
"TIMUA VUMBI TIMUA! TIMUA
VUMBI TIMUA! WE WEEE...."
Watu walikuwa hawasikilizani mule ndani,waliimba
wimbo huo wa kizazi kipya uliokuwa unapigwa ndani ya gari hiyo kwa sauti kubwa.
Wanafunzi wengine walikuwa
wakinyonyana mate na kubadilishana ndimi zao bila aibu ndani ya gari hiyo.
"Dereva Lena tu wewe,spidi
gani hii bwana?! Hebu choma mafuta kama sio Lena tuone...." ilisikika sauti ya kilevi ya mwanafunzi mmoja
aliyekuwa akiitwa Michael, alisifika kwa ukorofi na ulevi pale chuoni,na leo
hii alikuwa amelewa tila tila.watu walimshangilia na kumuunga mkono
"Dereva Lena,kama sio Lena
tumwage,dereva Lena kama sio Lena tumwage". Walianza kuimba,kisha dereva
akapanga gia vizuri,na kuchochea moto huku wanafunzi wakianza kumshangilia kwa
kupiga mbinja na miruzi..
" woyoooooo...."
Basi baada ya mwendo Wa masaa sita
walikuwa wameshafika ktk mkoa wa iringa,wakitokea jijini Dar es salaam
wanafunzi wale walishuka huku kila mtu akiwa na mwenza wake,isipokuwa kijana
mmoja tu aliyeonekana kuwa mkimya muda wote, tangu safari ianze..alikuwa ni
mrefu kidogo, mweupe, amejazia kidogo misuli yake, alikuwa ana sura nzuri
haswaa(handsome) alafu alikuwa amevaa vizuri sana siku ile ya study
tour.alikuwa amepigilia flana nyeupe na suruali nyeusi(jeans) yenye michaniko
magotini..kibegi cha mkanda mmoja alichokizungushia begani mwake kilimfanya
azidi kupendeza.
"Sasa wanafunzi
tusikilizane,leo tutapumzika kidogo hapa iringa mjini,na kesho tutaanza safari
kuelekea kalenga kwaajili ya tour yetu.hivyo kuweni makini sana,sitaki kusikia
mmefanya ujinga wowote ule." Aliongea lecture mmoja mrefu
mweusi,aliyeonekana ni mtu mzima kiasi.
Wanafunzi wao walikuwa wakipiga
makelele tu bila kusikilizana vyema na mwalimu wao.walikuwa maeneo ya stendi ya
daladala ya ipogolo,basi wengine walirudi ndani ya gari huku wengine wakibaki
nje tu pale wamekaa..ilikuwa ni majira ya saa 1 usiku huku baridi kali ikianza
kupiga ktk usiku ule.
Wanafunzi wale waliilaani ile
baridi huku wengine wakijutia kutobeba masweta na koti za ziada,lakini kwa kuwa
walikuwa wanaume na wanawake basi walikumbatiana,huku wengine wakianza
kubadilishana ndimi zao bila aibu vile.huko ndani ya gari sasa,kwa kuwa
kulikuwa na giza. Basi kwenye siti za nyuma wanafunzi walikuwa wanazini tu
kuondoa ile baridi.lecture wao alienda kutafuta nyumba ya wageni karibu
akiwaacha wanafunzi wake wakilana uroda usiku ule.
"Mambo ibrah,mbona unajitenga
tenga Leo,alafu huna furaha kabisa au hukuipenda hii safari?!" mwanadada
mrembo kabisa, mwenye asili ya kisomali aliyebana nywele zake nyuma kisha
akazitupa mgongoni,Macho yake yalikuwa mithili ya mtu aliyelamba kungu lips
denda na pua ndefu ya kisomali iliyojichonga ilimfanya azidi kuwa
mrembo.Alimuuliza vile kijana ibrah huku akitabasamu na kutengeneza vishimo
mashavuni mwake.Ibrah ndiye yule kijana aliyeshuka ktk gari na kujitenga..
"Ah! Usijali Leyla mimi nipo
sawa tu labda hali ya hewa sijaizoea"
Alijitetea Ibrah huku macho yake
yakitua moja kwa moja katika kifua cha mwanadada yule, mwenye chuchu ndogo
zilizosimama kama sindano,
"Uongo huo ibrah tangu
tunatoka dar nilikuwa nakuangalia tu ulikuwa upo kimya sana unaonekana una
msongo wa mawazo tatizo nini ibrah?" Leyla alimuuliza ibrah huku akisogea
karibu zaidi kwa ibrah na kuweka umbali wa mita ziro kutokana na lile baridi..
"Ehee huyu ndio yule fala
anayekuchukulia demu wako."
Aliongea mwanafunzi mmoja mrefu
mweusi,akinyooshea kidole kwa Ibrah. walikuwa wapo watatu wamesimama mbele ya
kina Leyla na ibrah.
Yule mlevi aliyekuwa anapiga kelele
ndani ya gari muda ule ndio alikuwa akiambiwa na yule kijana, kisha kwa sauti
ya kilevi akasikika akisema.
"Yani we fala huna ishu alafu
unanichukulia demu wangu Leyla? Unakaa naye huku, hivi nimekuonya mara ngapi
kuhusu Leyla? sasa leo acha nikufunze adabu kidogo"
Alirusha chupa yake ya bia kuelekea
kwa ibrah,ambapo aliikwepa na kubamiza chini kisha ikapasuka,yule mlevi
alimsogelea Leyla na kumkumbatia huku wale wawili waliobaki wakianza kumpiga Ibrah.
Wanafunzi waliopo nje,walisogea
pale Ibrah alipokuwa akipigwa huku wakipiga makelele kushangilia ule mpambano
"Piga huyoo, usikubali wewe
amkaa." Zilikuwa ni sauti za uchochezi
Leyla alijaribu kujitoa kwa yule
mlevi lakini alishindwa kutokana na nguvu alizonazo yule mlevi pamoja na pombe
zake, alibaki akilia tu baada ya kumtazama Ibrah akipigwa pale chini.
"Mnichukue mimi kama
mnanitaka, mumuache Ibrah jamani msimpige hana makosa" Leyla aliongea kwa
sauti ya uchungu huku akianza kulia.
"Muacheni inatosha Leyla wangu
kamtetea ana bahati" yule mlevi aliwaamuru wale vijana ambao walimuacha Ibrah
pale chini akivuja damu mdomoni na puani.
Wanafunzi walibaki kushangilia tu
na kuanza kutawanyika pale,kila mtu akirudi alipokuwa.
Ibrah alijiinua na kujifuta damu
zilizokuwa zikimtoka kwa kutumia kitambaa chake kilichokuwepo katika kibegi
chake kisha akakaa pembeni,alipokuwa mwanzo.
"Mbona wamekupiga kizembe
vile, na hujawafanya chochote kile?" Alikuwa ni Raphael ambaye ni rafiki
yake kipenzi Wa Ibrah, ambaye alimsogelea karibu Ibrah na kumuuliza.
Ibrah alikaa kimya bila kujibu huku
akiendelea kujiweka sawa.
"Unajua kuwa wewe una uwezo
mkubwa wa kupigana lakini umepigwa kizembe tu hapo,mpaka nimeshangaa"
Aliongeza Raphael
Ibrah alimtuliza rafiki yake asiwe
na jazba huku wakibadili mada na kuanza kupiga stori zingine.Ibrah na Raphael
wanasoma chuo kimoja,lakini pia wanakaa mtaa mmoja maeneo ya magomeni jijini
Daresalaam,hivyo wanafahamiana tangu zamani sana.
Asubuhi ilifika,kisha lecture akaja
na kuwaambia wanafunzi kuwa safari itaanza asubuhi hiyo,hivyo kila mtu ajiandae
vizuri.kulikuwepo na vyoo na mabafu ya kulipia katika stendi ile,hivyo kulikuwa
na foleni kubwa ya wanafunzi waliokuwa wanataka kuoga..
"Habari yako kijana, kwani
mnaenda wapi?" Alikuwa ni mlinzi wa choo kimoja akimuuliza Ibrah baada ya
kumaliza kuoga.
"Tunaenda kalenga Uncle"
alijibu Ibrah huku akimaliza kujifuta na kutoa pesa kwaajili ya malipo.
"Kalenga? Basi mmekwisha"
Aliongea yule mlinzi huku akitoa
macho,
"Kwanini Uncle?!?"
Aliuliza ibrah kwa mshangao mkubwa.
Je,kuna nini huko kalenga mpaka
mlinzi ashangae?
Itaendelea
Kesho 12 Jioni
Dah!!! Nice
ReplyDelete