KUTANA NA WAUWAJI HATARI KUWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA DUNIA

 

MTAARISHAJI: MBAJI MOHAMMAD


NANI ALIYEKUWA JACK THE RIPPER

Leo ntakurudisha nyuma kidogo hadi Karne ye 19 nikimaanisha miaka ya 1800 huku bara Ulaya katika nchi ya Uingereza. lilishuhudia matukio mengi sana ya kutisha na kustaajabisha katika maeneo tofauti.

Ambapo inaelezwa kwamba katika nchi hiyo ilikabiliwa hali mbaya ya kiuchumi ilishuhudiwa, ajira zilikua finyu, makazi yalikua mabovu kwa walio wengi, huku asilimia 55% ya watoto waliozaliwa walikufa kabla ya kufikisha miaka mitano (5), watoto wa mitaani waliongezeka, uwizi, fujo, na ulevi vilikua ni vitu vya kawaida kila siku. Umasikini uliokithiri uliwasukuma wanawake wengi kuangukia katika shughuli za ukahaba ili kuendesha maisha yao.

Lakini waswahili walishasema ng’ombe wa masikini hazai. Pamoja na umasikini uliotawala katika wilaya ndogo ya Whitechapel mikono iliyojaa damu ilivamia wilaya hii ndogo. Mikono hii haikua na huruma kwa miili ya binadamu mikono hii haikuheshimu wala kusitiri maisha ya kiumbe aliyeitwa binadamu. Mikono hii ilikua ni ya muuaji aliepewa jina la Jack The Ripper.

 JACK THE RIPPER (Serial Killer) kwa majina mengine alifahamika kama, THE WHITECHAPEL MURDERER au LEATHER APRON ni muuaji ambaye hadi leo hii taarifa zake hazijajulikana tafiti na pelelezi za ki-intelligencia zilifanyika lakini hawakuweza kumpata muuaji huyu hatari. Mara zote alifanya mauajia katika maeneo yaliyoathirika sana na umasikini. Wengi katika wahanga wa mauaji yake walikua ni wanawake tena makahaba.

Mwaka 1888 kwa kipindi cha miezi minne tu, Jack the Ripper aliua idadi ya wanawake watano ambao kati ya hao watatu miili yao iliharibiwa sana. Usiku huo, Agosti 31, 1888, kulikuwa na baridi ya kubwa huko Whitechapel, labda eneo la hatari zaidi na la London. Hisia ilikuwa kama vile msimu wa baridi ulikuwa umeshafika. Kwa masaa kadhaa, dhoruba ya radi ililipuka, umeme ukaangaza kusumbua, lakini hewa haikuwekwa wazi kwa moshi wa mara kwa mara - jogoo wa moshi na uzalishaji mwingine. Katika umbali wa mita chache tu, tayari ilikuwa haiwezekani kutengeneza chochote. Rogue Charles Cross hufanya njia ya kupita kwenye makazi duni haya ya London, akawatoa gari ndogo, ambalo analipa ushuru kwa senti chache.

Kwenye barabara iitwayo Buck Row, iliyowekwa wazi na taa ya barabarani, saa 3 na dakika 40 hugundua mwili wa mwanamke umelala chini. Anaonekana kuwa amekufa. Barabara hiyo inaacha na inaelekeza kwa maiti ya mtu mwingine kama yeye - Robert, ambaye pia anaendesha gari lile lile karibu. Pamoja wanamkaribia mwanamke. Sketi zake zilivutwa na alikuwa amefunikwa kwa damu usoni mikono tayari ilikuwa baridi, lakini miguu yake ilikuwa joto.




Jack The Ripper alikua muuaji wa aina yake. mwaka 1888 katika miezi ya September hadi Oktoba aliwatumia baadhi ya wanahabari barua zilizoeleza yakuwa yeye ndiye mtu aliyohusika na mauaji yote. Barua hizi zilikua na jina moja tu nalo ni JACK THE RIPPER. vitendo hivi vya kutuma barua ni kama vilipitiliza mipaka, jioni moja kiongozi wa patrol za usiku alipokea barua ambayo anuani yake ilisomeka kuwa “imetokea kuzimu” jina lilikua ni la Ripper na barua iliambatana ki-boksi kidogo ambacho ndani yake kulikua na kipande cha figo ya mwanadamu.

Lakini mwaka 1888 hadi 1891 mauaji yaliendelea, kipindi hiki polisi walifanya uchunguzi wa mauaji ya watu 11 ambao wote inaaminika kuwa waliuliwa na mtu mmoja tu ambaye ni Jack the Ripper. Tafiti na uchunguzi zikafanyika lakini waliishia kubashiri tu kwani hawakumpata haswa mhusika wa mauaji haya ya hatari kabisa.

Mwishoni mwa mwaka 1891 na kuendelea, wingu la giza lilififia ni kama vile Ripper alistaafu kuua, au labda yeye pia mauti yalimkuta pasina kufahamiaka, kwani kipindi hiki ndicho ambacho Ripper alipotea na kila kilichomhusu yeye kilitoweka.Mauaji ya kikatili yalipungua na pamoja na yote polisi bado hawakuweza kumpata mhusika wa mauaji aloitwa JACK THE RIPPER.

Wakati waingereza wakipumzika na mauaji ya mnyama JACK THE RIPPER, nchi jirani ya ufaransa mwaka 1894 ilianza kushudia mauaji ya kikatili katika maeneo ya nje ya miji. Afadhali kilichokuwa kinatokea Uingereza kwani, muuaji huyu alieibuka ufaransa alikua ni mtu ambaye hakuwa na aibu wala heshima, alichinja, kisha alitoboa toboa miili ya wahanga kwa kisu na bila aibu wala ubinadamu alizibaka maiti za wanawake na zile za wanaume alikuwa akiziingilia kinyume na maumbile aliitwa VACHER THE RIPPER.

Jina lake halisi alikuwa anaitwa Joseph Vacher alitokea katika Familia ya watu 17 baba, mama na watoto 15 wote inasemekana waliishi katika chumba kimoja tu. pamoja na baadhi ya mifugo yao kama kuku na paka. Elimu yake ya msingi aliipata katika shule moja ya kikatoliki tena yenye sheria kali kwelikweli. Lakini ukorofi na ubabe ni kama ulikua katika asili na damu ya JOSEPH VACHER kwani hata shule hakumaliza, alifukuzwa kutokana na vitendo vya udhalilishaji wa kingono.

Akiwa kijana wa miaka 17 tu,alieshindikana nyumbani kwao. Vacher anakua mtu wa kulala kwenye nyumba za makahaba, pombe na uhuni vikawa ndio kama desturi yake. La haula, wazo kujikomboa kutoka katika umasikini lilimjia na hapa ndipo Vacher aliamua kujiunga na jeshi la nchi ya Ufaransa ikiwa ni miaka ya 1880.



Jeshini ndio sehemu ambayo Vacher alikutana na msichana mrembo aliekua ni mtumishi jeshini, aliitwa LOUISE msichana huyu Vacher aliamini ya kuwa amepata mwanamke ambaye ataishi naye kama mke kwa maisha yake yote. Hakusita, alimtafuta LOUISE na akaanzisha naye urafiki wa kawaida. 

Lakini sheria za upendeleo na matabaka yaliyokua jeshini, vilisababisha ugumu katika kutambulika na kupandishwa cheo kwa wanajeshi wa chini ambao walikua na juhudi na walistahili vitu hivyo. Vacher aliamini ya kwamba yeye ni mmoja wao.Lakini alichoshwa na mfumo kuendesha jeshi la nchi yake..hivyo alifanya jaribio la kujiua ambalo lilishindikana .Kwani wenzake walimuwahi na kumkimbiza hospitalini na huko alipata matibabu akapona kabisa, na punde aliporuhusiwa kutoka hospitali Vacher alifukuzwa jeshini mara baada ya kufanya jaribio la kujiua. Akiwa tayari ameingia mtaani, sasa sio mwanajeshi tena.  Vacher anapata wazo la kuoa, Mawazo yake yanamrudisha mpaka kwa LOUISE.

Ilikua asubuhi moja hivi tulivu Vacher aliamua kwenda hadi nyumbani kwao na msichana mrembo LOUISE. Kama kawaida mama yake na Louise alikuepo nyumbani pamoja na binti yake, Vacher alifika aliwasalimu na akajitambulisha kisha akaomba ridhaa kwa mama yake Louise ili aweze kumuoa binti yake.

Taarifa yake haikupokelewa vizuri kwani LOUISE alimkataa Vacher tena kwa maneno mabaya mbele ya mama yake. Hapa Vacher hakuwa na chaguo tena, wazo lililokuwa kichwani ni kumuua LOUISE na kujiua yeye mwenyewe alichomoa bastola, risasi nne alizifyatua kwa Louise na yeye akijipiga risasi 2 kwa jaribio la kujiua. Wote wawili walipelekwa hospitali walipatiwa matibabu na baada ya muda mrefu walipona. Lakini madhara makubwa yalikua kwa Vacher kwani alipooza katika upande wake mmoja wa uso na risasi moja haikuweza kutolewa, hivyo alilazimika kuishi nayo hadi atakapoingia kaburini.

Mwaka 1894, penye miti palipata wajenzi. Akiwa ni mwenye umri wa miaka 25 Vacher alirudi uraiani mara baada ya ripoti za madaktari kueleza kuwa alikua tayari ni mtu aliepona kabisa. Alianza kuishi akifanya kazi katika mashamba yaliyokua nje ya miji huku baadhi ya nyakati aliishi kama omba omba mitaani.

Haukupita muda, alianza mauaji waathirika wengi walikua ni wasichana ambao wamevunja ungo na wavulana waliobalehe. Wengi wao walitoka katika familia masikini, tena aliwaua katika mazingira ya mbali ambapo labda aliwakuta shambani au wakiwa wanasimamia mifugo katika maeneo ya mbali na makazi. \

Wahanga wa mauaji yake miili yao iliharibiwa sana, Vacher alifanya mambo ambayo hata shetani anaweza akakaa chini iliapate darasa. Mbali na kuchinja, Vacher aliitoboa vibaya miili ya watu, alibaka maiti za wanawake, na kijana aliekua muathirika wake wa mwisho alikutwa ameingiliwa kinyume na maumbile baada ya kuuawa. Huyu alikua ni JOSEPH VACHER ambaye alikuja kupewa jina la VACHER THE RIPPER au THE FRENCH RIPPER akifananishwa na JACK THE RIPPER aliepotea Uingereza miaka ya 1891. 

Lakini hakuna marefu yasiyokua na mwisho, jioni moja Vacher alimshambulia mama mmoja ambaye alikua nje kidogo ya mji akikusanya kuni. Mama huyu alijibu mashambulizi na huku akipiga kelele ambazo ziliwaleta mwanae wa kiume na mume wake ambao hawakua mbali. Walimzidi nguvu Vacher na kumuweka kizuizini. Alifikishwa katika mamlaka na uchunguzi ulifanyika lakini ushahidi haukuepo wa kutosha. Mahojiano ya muda mrefu yalifanyika na Vacher alikiri kua alihusika na mauaji ya watu 11 hadi 27 huku akidai aliwaua akiwa katika hali ya ukichaa kwani aliwahi kung’atwa na mbwa akiwa bwana mdogo suala ambalo aliamini lilimuachia kichaa katika damu yake.

Kama ilivokua matarajio ya wengi, mwaka 1898.Baada ya kugoma kutembea, Vache aliburuzwa hadi sehemu ya kuchinjiwa. Ambapo alikatwa kichwa kama adhabu ya makosa aliyoyatenda. Na hapo RIPPER wa pili alitoweka katika uso wa dunia kama alivyotoweka Ripper wa kwanza pasina kujulikana

Kalamu ya mdadisi inaishia hapa. Nakukumbusha kupitia ukurasa wetu ili uwe wa kwanza kuona Makala zetu.

Kila Siku Saa 12:00 Jioni

Kwa SHORT BACK STORY Kama hii Tukutane Kila Jumamosi Saa 4:00 Asubuhi 

 MWISHO

Comments

Post a Comment

Popular Posts