WITNESS - SEHEMU YA KUMI NA TANO
SIMULIZI: WITNESS
SEHEMU
YA KUMI NA TANO
Nilijisikia huzuni sana kuona ni
namna gani familia yangu inateketea bila kosa, Kama Baba asingenichagua mimi
kumuoa binti Mfalme basi vijana wengine wangefanyaje mashindano ya kuchaguliwa
mshindi wa kumuoa binti Mfalme. Hii yote
ilitokana na tamaa ya Baba ya madaraka katika jumba la kifalme kweli *Tamaa
mbele mauti nyuma*.
Tunaendelea…
"Vipi kuhusu mama na Julieth?
"Mama yako pia yupo kwenye
Jumba la kifalme kwa ajiri ya kutetea haki ya Julieth, Clement yanayoendelea ni
mengi huwezi kuyajua kwa haraka ivyo" Bella alikua ananiangalia kwa
huruma.
Nilimfuata Bella nikamsogeza karibu
nakumkumbatia,
"Yote nilifanya kwa ajili yako
Bella ivi unajua nikiasi gani akupenda, Nakupenda kuliko hata unavyofikiri.
Kila kitu nimefanya ili niwe na wewe Malkia wa moyo wangu, usiniache Bella kua
namsimamo katika mapenzi yetu, Usiuumize moyo wangu, Tafadhari nipende
Bella" niliongea kwa hisia nahisi hata yeye alinielewa
"Vipi yule mtu uliekuja naye,
mbona anaonekana ni mtu mkubwa katika Jumba la kifalme, Na ninani kwa upande
wako"
"Ni mtu wa kawaida tu ila
tulifahamiana nae kabla hata sijapata matatizo, Amenisaidia sana yule mdada
labda ningekuwa nisha kufa, kila kitu nitakwambia vizuri nikitulia ila niambie
kua unanipenda bella, niambie kua hutonisaliti hata ukutane na nini mbele
yako"
"Nakupenda pia Clement na nakuahidi
kutokukuacha hata nikutane na nini mbele yangu, Nitakupenda" Nilijisikia
furaha kuambiwa maneno yale machache ya Bella yaliyokua na maana kubwa ndani ya
moyo wangu, Nilianza kuuchezea mwili wa Bella, tukaanza kubadilishana mate,
mate mate nikaona mtoto anachanganyikiwa. toka niingie kwenye mahusiano na
Bella hii ndio ilikua mala ya kwanza mimi kulala na Bella na kushiriki tendo.
Nilishtuka badae sana baada ya zoezi
tulilolianya usiku nilivyoangalia pembeni
ya kitanda sikumuona Bella, nilianza kuangaza nje bado kulikua na giza. Nilitaka kutoka nje nikasikia michakacho ya vitu
kwenye chumba cha jirani, ilibidi niangalie ni kipi kinaendelea huko, nilimuona
Bella akipanga ndoo juu kisha akapanda ili Kuchungulia dirishani,
"Bella unafanya nini
hapo" Bella hakunijibu kitu ila alinionyesha ishara kua nitulie, ilibidi
nifanye ivyo tu sikua na namna,
Niliskia sauti ya Chande nje nikama
alikua na watu wengine nikataka nitoke ila Bella alinizuia, Kweli nilikua nimemkumbuka rafiki yangu
chande, tena nilimkumbuka sana tu.
"Kwanini unanizuia Bella"
Nilimuuliza bella lakini bado hakujibu kitu alibaki kuchungulia tu dirishani.
Baada ya muda nilimuona akishusha
ndoo zile chini na kuhema kwa nguvu kama kuna kitu kikubwa amekikwepa.
"Kwanini umenikataza kumuona rafiki angu Chande hujui ni jinsi gani
nimemkumbuka"
"Clement huna rafiki anayeitwa
Chande wewe, Chande siyo rafiki kwako"
"Unamaana gani bella"
"Namaanisha hutakiwi kuonana
na Chande "
"Ooh sawa mamaangu inabidi
nikajitokeze mbele ya mfalme ili kuokoa familia yangu"
"Wewe unatafta kifo eeh,
Huwezi kupona hata kidogo kwa yule mfalme ila utakufa wewe na familia
yako"
"Shida si ni mimi tu acha
niende Bella naweza okoa mmoja kati ya watatu"
"Clement kuna kitu hujui,
saivi mfalme hana shida na wewe sana ila inapaswa tu utafutwe, ulivyokimbia
Nkizwa ilibidi mfalme aje akutafte nyumbani kwenu aliamini utakua umejificha
hapo. Baada ya kuja nyumbani alimpenda Julieth mdogo wako akataka kumuoa,
mgogoro ulikua ni mkubwa zaidi ya familia yako kwasababu yule ni sawa na mwanawe
wa mwisho"
"eeh baada ya hapo ikawaje?
" niliongea huku nikikaa vizuri
"Mfalme alitumia nguvu akaamua
kumbeba Julieth na kuondoka nae, Mama ako alienda ili kutetea haki ya mwanae
hadi leo hajarudi tena, Ila Kuna siku Julieth alikuja akiwa umeambatana na walinzi, aliniambia kule hakuna Chochote kibaya ila
shinikizo la mfalme lipo palepale,
aliniachia nyumba niilinde ili siku ukija nikukabidhi kama utakuta wao
wamefariki"
"dah mkosi gani huu, ila yote
ni Makosa ya Baba angu siyo makosa yangu. Vipi nakuhusu Chande kwanini
Umenikataza kumuona"
"Nashindwa hadi kukueleza
vizuri Clement hutakiwi kujua mambo yote kwa wakati mmoja, ila ulipotoroka
vijana walipewa kazi ya kukutafta na atakaefanikiwa kufanya ivyo basi atamuoa
binti Mfalme Witness, wengine wamejiondoa kwenye swala hili ila wale wanaomtaka
binti mfalme bado wanakutafta akiwemo Chande"
"Chande ananitafta mimi kwa mabaya?
" Niliuliza huku nikikaa vizuri,
" Chande anampenda sana Binti
Mfalme na sizani kama anataka kuipoteza hii nafasi na ni mtu anaeaminiwa sana
hata na Mfalme kwa sasa, sizani kama
anaweza kubari kuipoteza hii nafasi eti kisa rafiki yani rafiki tuu"dah
nilihisi kuchoka Clement Mimi.
Itaendelea
Kesho Saa 12:00 Jioni
Comments
Post a Comment