WITNESS - SEHEMU YA KUMI NA MOJA

SIMULIZI:  WITNESS

 

SEHEMU YA   KUMI NA MOJA

Niliamua kutoka nje huku nikichungulia kila pande nikaelekea ile sehemu ambayo nilimtoroka mlinzi, Nilianza kurudi kwenye ile kambi huku nikishikiria tumbo langu walinzi walikuja kunipokea na Kunipeleka sehemu ya Kukaa.

Baada ya Muda nilisikia kengele ikipiga katika jumba ya Mfalme, sikujua hii ilikua ni kengele ya nini ila mala nyingi hutumika kwakusanya wanakijiji wa Nkizwa.

Tunaendelea…

 

Walikuja vijana wawili wakanichukua, nilipelekwa kwenye chumba kingine kilichokua kimepambwa vizurii pia kilikua na harufu nzuri tu. Hapo nilianza kubadilishiwa mavazi na kuvalishwa mavazi ya heshima.

"Nahitaji kuongea nae huyu, naomba mnipishe" kijana mwingine aliyekua amesimama pembeni mda wote aliongea.

Wale vijana wengine wakatiii na kutoka nje, Muda huo mapigo yangu ya moyo yalikua yameanza kwenda kasi.Woga uliannza kuniingia,  Nilianza Kufikiria kitu kitakachotokea mbele yangu, Kama ningejua ningetoroka na Winni ili wale askari wasinikamate.

"Najua haunifahamu, mimi ndiye Medrick mdogo wa Witness" aliongea kisha akachukua kinywaji na unipa huku nae akibaki na kingine.

"Najua kwako itakua ngumu kumkubali mtu ambaye hujawai kumuona hata mala moja, ila nataka nikwambie wanakijiji wote wapo nje wanasuburi ni nani huyo anayetaka kutangazwa kwa ajiri ya kumuoa binti Mfalme ila basi hautatangazwa bali leo utamuoa huyo binti Mfalme"

Nilitamani kusema kitu lakini mdomo ulikua mzito kufunguka, ulimi haukutaka kufanya kazi yake.

"Unaonekana siyo shujaa na sijaona jina lako katika daftarii la vijana wa Nkizwa waliotakiwa kufanya mashindano ya kumuoa binti Mfalme, Inamaana kua hii nafasi hukuhitaji toka mwanzo ila kama Witiness akasema ndiyo naomba na wewe useme ndiyo, usimuabishe dada yangu". Medrick alimaliza kuongea kisha akaruhusu wale vijana waendelee na kazi yao. 

Watu wa Nkizwa walijazana katika Eneo la Mfalme, Viongozi mbalimbali wa jumba la Mfalme walikusanyika hata vijana waliokua wakiitaka ile nafasi kwa udi na uvumba walijaa kujua ni nani aliyeteuliwa kumuoa binti Mfalme. Macho yangu yalikua bize kuangaza ni wapi ningemuona Bella, baada ya kutafta kwa mda mrefu nilimuona Bella akiwa na rafiki zake wawili, hakua na furaha hata kidogo japo nilikua mbali na Bella lakini Niliweza kutambua hali yake ya mda ule. Nilikua nimeketi Juu, sidhani kama ingekua rahisi wanakijiji wale kuniona ila mimi niliweza kuwaona wote hata rafiki angu Chande akiwa na vijana wenzake. Mawazo yangu yalikua kwa Bella na Kile ambacho kingeweza kutokea.  

Baada ya Muda nilimuoana Witness akiiletwa mahari pale huku akiwa ameongozana na kijakazi wake wa Karibu Shadrassa pamoja na wengine wawili.  Alikua amependeza haswa mavazi yake ya mapambo na Cheni za Kun'gara zilizidi kuupendezesha uzuri wake, Kiufupi Witiness alipendeza, Nilimuona binti Mfalme kwasababu mimi nilitangulia kufika mahari pale ila yeye hakuniona mimi.

Tukiwa pale nilimuona Mfalme akisimama ili kuongea baadhi ya Maneno, watu walikua wametulia.

 

Itandelea

Kesho Saa 12:00 Jioni

Comments

Popular Posts