WITNESS - SEHEMU YA TATU

 

SIMULIZI: WITNESS

 

SEHEMU    YA    TATU

Yule Mdada hakujibu kitu, alichukua mshare na kuurusha juu, sijui hata ulienda Kutua wapi huo mshare, Lakini ghafla nilishangaa kuona wanaume kama Sita wakituzunguka.

Tunaendelea…

 

Tulibebwa mpaka sehemu ya kambi, Ilikua ni kambi ndogo tu lakini kulikua na watu wasiopungua 60 kwa kukadilia kwa Ukubwa wa Kambi ile.

Tuliwekwa sehemu moja na Chande huku tukifikilia nini kingefuata baada ya pale. 

"Ivi Chande huu Mpango umeupanga wewe et eeh, haiwezekani useme hua unakuja huku wakati Kuna ulinzi Ivi, Na ulijua tu kua ni sehemu hatari, Unampango gani na Mimi? " Nikimuuliza Chande.

 

Chande hakujibu kitu Chochote kama vile hakua amenisikia wakati nauhakika asilimia zote alinisikia.

 

"Chande si naongea na wewe" Awamu hii niliuliza kwa Hasira huku nikimuangalia.

"Clement Usitake tukosane, mbona wewe unamfaham yule mdada lakini mimi sijakuuliza kitu, je ulijua kama Ninatega pale vitoweo vyangu ukaamua kutumia wale watu mi Nitajuaje? Na Ule unga uliubeba wa nini maana ulivyomwaga tu na yeye alikuja"

 

Kabla sijamjibu kitu Chande tulisikia mlio wa Farasi,  hakua Farasi mmoja wanaonekana walikua ni Kundi dogo la watu ndio wamekuja na Farasi hao.  Hapo tulianza kuona kama watu wakikimbia ovyo nje.

"Wewe mbona kama Hapa wamevamiwa, usikute wanauana sisi tumekaka hapa" Chande aliongea.

Namimi nikasimama ili Kuchungulia, kweli watu Walikua wakikimbia ovyo vyo pia wengine walikua wakipambana Kwa Kutumia upanga, ni kama kulikua na ugomvi kwenye kambi hiyo.

 

"Tuondoke hapa, tutakufa kwa ujinga" Chande aliongea huku akiangalia njia gani tunaweza kuondokea kwa usalama.

 

Katika angalia angalia, nikamuona yule binti aliekua ametukamata, alikua akipambana na binti mwingine, wote walionekana kuchoka ila yeye alionekana kuchoka zaid pia alikua akielekea kushindwa katika pambano hilo.

Badae akaangushwa Chini, Alikua hana Nguvu ya Kufanya kitu tena, Nilimuona mpinzani wake akiinua siraha yake na Kutaka kummalizia.

Sijui nilifika mda gani mahali pale, au nilipata wapi Ujasili na nguvu zile, Ila ninachokumbuka ni Jinsi nilivyo kua nimemsukuma mpinzani yule, alienda kutua chini kama Mzigo puuh!

Sikua na uwezo wowote wa kutumia upanga, nilitafta mshare ili Kummalizia lakini mkono wangu ulishikwa nyuma, Niligeuka ili kumuangalia aliekua amenishika,  Alikua ni Yule binti alietukamata, binti ninae msaidia,  binti niliekutana nae Kwenye Jumba la mfalme.

Sikuwa nimempenda yule binti wala hakuna chochote kizuri alichonianyia toka nikutane nae sijui nikwanini nilienda Kumsaidia alivyokua akipambana.

 

"Tuondoke sio salama tena" Aliongea huku akielekea kwenye Farasi wake.

Alipanda Farasi na Mimi nikapanda yani hata sikumkumbuka Chande hata Sijui alikua wapi kwa wakati Ule, yule dada Aliendesha Farasi huyo hadi Maeneo ya Mbali kidogo na Eneo hilo.

 

"Naitwa Clement, Sijui unaitwa nani" Nilimuuliza baada ya Kushuka kwenye Farasi huyo.

"Naitwa Winni"

"Winni?? " Nilimuuliza tena.

"Ndiyo, kwanini Umeamua kunisaidia kwa wakati ule hujui kama Ulikua unatafta matatizo na sura yako hukuificha kama Mimi"

 

Kweli yeye alikua ameficha Sura yake, hadi mda huo nilikua siijui sura yake, labda macho yake madogo aliyokua ameyaacha

 

"Kwanini mnapambana?  Na kwanini ulitukamata kwa mda ule, na kwanini Askari kwa askari wa Kifalme mnapambana? " Nilimuuliza.

"Unaonekana nimkubwa kiasi kuliko mimi, ila kwa hili Jambo mi nimkubwa kuliko wewe.  Je Unajua? "

"Najua nini??" Nilimuuliza

"Uliemsukuma pale ni Witness, ni Mtoto wa Mfalme, vipi utarudi kijijini Kwenu ikiwa ameshakuona sura yako na amejua unashirikiana na sisi au utabaki hapa? "   Aliongea Winni

 

Itaendelea

Kesho saa 12:00 Jion

 

Comments

Popular Posts