WITNESS - SEHEMU YA SITA
SIMULIZI: WITNESS
SEHEMU YA
SITA
"Clement unanifanya mimi mtoto
siyo? Hakuna nisilojua kati yako wewe na
Binti Mfalme, haya Jana umeshinda wapi wewe siku Nzima? Kwa binti mfalme eeh, ila nakutakia Siku
njema" Bella aliongea kwa hasira na kuanza Kuondoka. Sikutaka kumzuia kwani niliona ni jinsi gani
alivyokua akiumia.
"Masikini
Clement Mimi" niliongea huku nikikaa chini.
Tunaendele…
Ilipita wiki moja bila kuwasiliana
na Bellath wala Chande, Winnie alikua akinifuatilia sana hata sijui alijuaje
mahari nilipo yani ni kama alikua akiniona kila niendapo, ila hata mara moja sikumwambia kile
kinachoendelea Kijijini, Mara nyingi
alikua akinifunza vitu vingi vinavyohusu utawala wa haki, na usawa katika
Kijiji.
"Mwanangu
kesho unahutajika katika Jumba la Mfalme " Baba aliniambia.
"Kufanya
nini tena Baba mi kuhusu Kumuoa binti Mfalme Nimeshasema sihitaji".
"Ivi wewe umechangakiwa,
Unajua hii nafasi ni vijana wangapi wanaihitaji yani umepata bahati wewe"
Baba aliongea kwa ukali kidogo.
"Baba kama Unaona Hiyo nafasi
Wanaihitaji vijana wengi kwanini Hamkuwapa hiyo nafasi? Kwanini mnailete kwangu Nisiyeihitaji. Yani ukweli tu sitaki hata Kumuona binti
Mfalme maana ninamchukia sana".
Niliongea tu ili kumfanya Baba
ahairishe mpango wake, kiukweli nilikua simuhitaji Binti mfalme ila sio kwamba
nilikua namchukuia.
"Unaongea nini wewe, ivi unataka
kufa eeh? unabishana na amri ya Mfalme.
Sitaki kusikia huo ujinga wako hapa, Kesho mapema tunaongozana katika Jumba la
Mfalme utake usitake" Baba aliongea kwa hasira sana huku akisimama na kuondoka.
"Kaka kumbe umepata bahati
kama hii yani sisi tunahangaika ili Kupata nafasi kama hizo ila wewe kiurahisi
tu umeipata na unaipiga teke. ila Kweli kaka unajua wewe ukimuoa binti Mfalme
basi mimi nitakosa bahati ya Kuolewa na Medrick mwana Mfalme" Aliongea
Julieth.
Sikumjibu kitu, niliinuka na kuanza
kuondoka. safari yangu moja kwa Moja kwa Bella, Nilitamani kumshirikisha baadhi
ya mambo mke wangu mtarajiwa Bellath.
"Umefuata nini hapa tena, Unataka
kuniletea matatizo? Tayari baba ako ameshasema asinione na wewe, Clement kesho
ndio unaenda kuonana na Binti Mfalme?
Unaniachaje mimi Clement, Ni Aibu gani utaniachia mimi" Aliongea
Bella baada ya Kuniona.
"Bella Kila mda wewe ni
kuongea tu, kwanini hunisikilizi Mimi? Kwanza sikia mimi sina mda na Binti Mfalme
na usiruhusu hili jambo likakukaa akilini mwako. Mimi ni wako tu na hicho ndio
kitu kinachotakiwa kukaa akilini mwako achana na ivyo vingine Bella".
"Nitaaminije
Mimi"
"Amini tu ivyo mpenzi wangu, Najua
ni kazi ila pokea vyovyote vile mimi sipo tayari kufunga ndoa na binti
mfalme"
"Vipi kama ukifa? Hujui upo hatarini kufa kama utakataa kumuoa
binti Mfalme".
"Nipo tayari kwa lolote Bella
ila niahidi kama hutoniacha au kunisaliti Bella".
Bella
aliitikia kwa Kutikisa Kichwa chake.
Nilimkumbatia Bella kwa hisia, nilikuwa
nawaza yale yatakayojiri mbele yangu, kwanza ninakosa la kumshikia Binti Nfalme
Panga kule kwa wasaliti kama Witness akiamua kulisema hilo mbele ya Jumba la
Mfalme basi maisha yangu yatakua hatarini. Na vipi kama Witness alinigundua na ndiye
yeye alieamua kuruhusu suala hili litokee ili apate njia rahisi ya kuwakamata wasaliti
wake akiwemo dada yake Winni. Nilimuachia Bella mawazo yangu yakiwa ni kwenda
kwa Winni, ili inabidi nikaonane na Winni labda atanishauri Chochote.
Nilifika mstuni na kuurusha mshale
wangu Juu, hii ni Ishara ambayo Winni alinifundisha kama nikimuhitaji, baada ya
mda mshare mwingine ulipigwa pembeni kidogo ya Mti, Kwa mda huo nilikua nimezoea
hali hiyo, Winni alikuja kwa kasi mithiri ya Upepo maeneo hayo.
Alinizunguka mala kadhaa na Kuanza
kunikagua, alikagua maeneo yale kwa umakini mkubwa. Alinishika mkono na kunipandisha Farasi wake
mpaka Sehemu ya Kambi. Watu wa kambi ile walishaanza kunizoea japo wengine
hawakua na imani na mimi ila wangefanyaje sasa.
"Umeniita,
kuna Shida gani? " Winni aliniambia baada ya Kuona tupo Wawili tu.
"Nimekuita
ndiyo ninashida"
"Ya
kumuoa binti Mfalme"
Nilishangaa Winni amepataje hizi taarifa,
yani kila mtu alipata taaarifa kabla mimi sijamwambia au Baba alishazisambaza
taharifa hizi maana nae anapenda sifa sana.
"Unajiuliza nimepataje
taharifa hii, Clement kila kinachoendelea kijiji cha Nkizwa hasa Kwenye Jumba
la kifalme mimi nakijua. yani hata taarifa ya wewe kumuoa binti mfalme
niliipata kabla wewe hujapata" aliniambia Winni.
"Mmh Upo vizurii sana, ila
mimi sikubaliani na Jambo la kumuoa binti Mfalme, nataka unisaidie kama mambo
yatakua makubwa basi nitahitaji Kutoroka hapa kijijini".
"Utoroke? Uende wapi?
hili kwangu ni Jambo zuri kwangu Clement, Unatakiwa umuoe binti mfalme
ili unipatie mimi nafasi rahisi ya Kufanya kile ninachokitaka. tuweze Kufanya mapinduzi
pale kijijini, ili tutafute haki ya wanyonge, ni wangapi wamebaki yatima na
Wajene pale kijijini kisa utawala huu "
"Winni unataka kupita mgongoni
kwangu lakini huangalii maisha yangu, Mimi simpendi Binti Mfalme na sijawai
Fikiria kumpenda".
"Ila
Unandoto ya umuona binti Mfalme? " Aliuliza
"Ndiyoo
ninayo"
"Basi
hiyo ndio nafasi yako ya Kumuona".
"Kwasasa haina umuhimu wa hiyo
nafasi, pia kumbuka yeye aliniona kabla mda ule nakutetea asikupige panga.
Nahitaji kua salama Winni, nahitaji kubaki na mpenzi wangu" Kwa wakati huu
niliongea kwa hisia sana, nilimaanisha nilichokua nakiongea.
Itaendelea
Kesho Saa
12:00 Jion
Nzuri sana Kaka hongera
ReplyDelete