WITNESS - SEHEMU YA TISA
SIMULIZI: WITNESS
SEHEMU
YA TISA
"Clement nakuhakikishia hata
mwanamke atakae kubari Kuolewa na Medrick basi Mfalme atataka kumuingilia
kimwili ili Kuhakikisha kama binti huyo ni mschana Kweli au laah, kama siyo msichana Binti huyo atakua ameishia
tu kuingiliwa na Mfalme lakini hataolewa na Kijana wake na Kama Binti huyo
atakataa kuingiliwa kimwili na Mfalme basi atauliwa, Clement mlinde sana Mdogo wako katika
hili" Winnie aliongea na kuondoka kwa Kasi ya ajabu sana.
Tunaendelea…
Nilibaki pale nikifikilia kauli za
Winni, Ni mda kweli pale kijijini walisema binti wa Mfalme amemuua Mama yake na
yeye ameuliwa ila hawakuonesha miili ya marehemu, Kumbe huyo binti alikua ni
Winni na alikua kasingiziwa.
"Winni aliniambia nyumbani
kuna walinzi wanaonitafta mimi, sijui kama bado wapo au wameondoka"
nilikua nawaza huku nikielekea nyumbani.
Nilipokalibia kufika nyumbani
nilikutana na Askari wa Mfalme mbele, hawakutaka kusikiliza chochote Ila
nachoshukuru walinibeba kwa Heshima tofauti na nilivyowaza na Kwa mda ule
tayari giza lilikua limefunika mwanga hivyo ilikua ni kazi wanakijiji kuniona.
"Nilipelekwa sehemu ya baraza
kubwa, na hisi ilitumika kwenye vikao au ilikua ni sehemu maalumu ya Mfalme na
familia yake.
Niliwekwa mahari hapo nikiwa chini
ya uangalizi mkubwa kutoka kwa Walinzi, Nilikua nawaza ni Jinsi gani ningeweza
Kujitetea au kukataa amri ya kumuoa binti Mfalme kama ningeonana na Mfalme
mwenyewe.
Nilipitiwa na usingizi hapohapo
mpaka siku ya pili, Niliamka na kukuta nimefunikwa Shuka. Walinzi walikua
wakiniangalia kama nina ugomvi nao, Sura zao tu zilikua kama wamekula kitu
kichachu wanaugulia radha yake, Huo ujasili wa kumuangalia mlinzi kwa mda mrefu
sijui ningeutoa wapi. Nilikua pale kwa mda wa nusu Saa bila kuongea na mtu yani
wote tulikua kama tunaugomvi, nilianza kuchoka sasa ni bora ningekaa nje
angalau nione watu. Niliwaangalia wale Askari nakuanza kujikoholesha
kimasihara, ghafla niliona wanakuja wanawake wawili wakiwa na sinia mikononi
mwao walitua chini na kunipatia maji yaliyokua na kitu kama sukari ila haikua chai.
"Eeh hizi huduma vipi au wote
wameshaambiwa habari juu yangu" nilikua nawaza huku nikitoa kikombe mdomoni
na kukitua chini
"Kama kweli wameambiwa hii
habari basi itakua ni njia rahisi ya ujitoa kwa Walinzi hawa maana nimeshachoka"
"Mmh Iivi mlinzi et mimi
ninakosa au maana mmenikamata bila kuniambia sababu" niliuliza huku
nikisimama, Yule mlinzi aliniangalia tu bila Kunijibu kitu chochote, Niliamua
kusogea karibu kabisa na yeye
"Nina njaa, yani naisi tumbo
kuniuma ivi alafu eti uwani ni wapi" niliongea huku nikishikilia tumbo
langu
Askari hakujibu kitu tena, nakuanza
kuelekea upande mwingine, Nilikua nimemuelewa
ilinibidi nimfuate tu, Alikua mbele mimi nilimfuata nyuma, tukiwa Kwenye ile njia nilimuona yule
kijakazi wa Binti Mfalme akipita sehemu ya Pili. Niliacha kumfuata yule Askari
nikakatisha njia na kumfuata kijakazi wa binti Mfalme huku nikimuangalia Askari
kama hata geuka.
"Ni wewe tena, umefuata nini
hapa au niite Askari" Niliskia sauti kama ya Binti Mfalme Witness
ikiongea, ilinibidi kugeuka ili nijue kuna nini
Yaala kumbe nilikua nimeingia chumbani
kwa Binti mfalme, hii ilikua ni Kosa kubwa tena sana.
Nilisogea haraka mpaka pale alipo
binti Mfalme na kumziba mdomo ili asiongee zaidi na zaidi, wote tukabaki
tunaangaliana.
Witness alikua ni mzuri tena saana
hakua na tofauti sana na Dada ake kwa uzuri waliokua wamejaliwa. Nilikua natamani
sana kumuona binti Mfalme toka nikiwa mdogo hata Kaka yake pia Medrick ila kwa kipindi
ninachowaona ni mda ambao sina hata hamu ya kuwaona nilihisi ni kwasababu ya kuingiliana
kwa mambo, mmh et kuingiliana au ni kwasababu ya mambo ninayolazimishwa Kufanya
eti nimuoe binti Mfalme duuh.
"Binti Mfalme Kuna kijakazi na
Askari Wanakuja Chumbani kwako" Sauti ya yule kijakazi niliyemfuata ndiyo
iliyonishtua.
Itaendelea
Kesho Saa
12:00 Jioni
Comments
Post a Comment