WITNESS - SEHEMU YA SABA
SIMULIZI: WITNESS
SEHEMU YA SABA
"Kwasasa haina umuhimu wa hiyo
nafasi, pia kumbuka yeye aliniona kabla mda ule nakutetea asikupige panga.
Nahitaji kua salama Winni, nahitaji kubaki na mpenzi wangu" Kwa wakati huu
niliongea kwa hisia sana, nilimaanisha nilichokua nakiongea.
Tunaendelea…
"Nitakusaidia ila unatakiwa kuonana
na Binti mfalme kama jinsi Baba ako alivyokubaliana na Mfalme. Kesho usikaidi hii amri ya baba ako mimi
nitakua pamoja nawe kwa kila jambo"
Sikua na imani na Winni hata kidogo
licha ya kumuona akijiamini na anauwezo wakufanya kitu ila katika hili sikumuamini
hata kidogo.
Mapema asubuhi tayari nilikua
nimeshawasiri katika jumba la Mfalme nikiwa na Baba Yangu, Moyo haukutaka
kutuliza mapigo yake kwani yaliyokua yanaenda kasi kama yanakimbizwa, Nayo Roho
haikuniacha salama katika hili hata kidogo, kuna mda nilihisi Binti mfalme
akiniona tu basi angeinua mshale wake na kunichoma nao pembeni kidogo ulipokaa moyo
wangu.
"Subiri hapo Nakuja"
aliniambia Baba huku akikatiza Moja ya Korido iliyokua hapo.
"Oohwwh!! " hapo niliona
ndio nafasi ya mimi kushusha pumzi.
"Sasa inabidi niangalie vizuri
njia humu ili hata kikitokea chochote niwe najua kwa kutokea" niliwaza
huku nikiangalia huku na huko kwa wasiwasi.
Nilianza kutembea na kuangalia
maeneo ya jirani na aliponiacha mzee Mzenga baba yangu, niliangalia kila sehemu
ya jirani,
"Wewe hivi huoni eeh"
ilikua ni Sauti ya kike ikinikalipia, sikua nimemuona huyu binti aliyekua
amebeba maziwa.
"Kuna nini huko" hii
ilikua ni sauti nyingine ya kike kutoka Chumba cha Pembeni.
"Nisamehe Binti Mfalme alitaka
kunisukuma huyu" aliongea yule.
Yeee Binti mfalme, sikutaka hata
Kugeuka kumuangalia.
"Nani huyo na anafanya nini kwenye
jumba la kifalme" Nilisikia sauti ya Huyo binti ikiongea huku ikija maeneo
niliyosimama.
"Aah Mtukufu binti Mfalme
Nkizwayeee Nkizwa iyeee" nilisalimia pasipo kumuangalia usoni, tena
nilikua na hofu sana hata sijui Nilisalimiaje hiyo salamu.
"Nkizwa yeee" Binti
mfalme alijibu huku akiniangalia kwa makini.
"Mmh hapa nisipokaa vizurii
nitajiingiza Kwenye matatizo, nae huyu Mzee si arudi tu mimi nitakaa hapa mpaka
mda gani oohshhh" hayo yalikua ni mawazo yangu huku nikiificha Sura yangu isiweze
Kuonekana kwa Binti mfalme.
"Aah Binti Mfalme Unajua, mimi
hapa nimekuja kwa kazi moja tu yani Moja tu sijui kama unaweza Kunisaidia"
Niliamua kutunga uongo huo ili binti mfalme asiniangalie zaidi.
"We-we-wewe, tumewai onana mim
nawewe" Binti mfalme aliongea huku akijitaidi kukumbuka kitu.
"Ooh Mungu eeh hapa itakua kazi
nyingine, Nikifanya mchezo nitakufa kizembe mimi na Winni sijui yupo kweli
maeneo haya au alinidanganya" nilikua nawaza ni kitu gani ningefanya hapo.
"Yaa Ndiyoo Binti Mfalme umewai
kuniona sehemu, ila Mimi sijawai kukuona hata sehemu. Si hua mnatuita wanakijiji hapo nje halafu
wewe na mtukufu Mfalme hua mnakaa juu na kutuangalia sisi labda Uliniona
huko"
“Sijui
kama atanielewa yani” nilijiuliza mwenyewe
Niliona Binti mfalme Witness
akiniangalia kwa umakini zaidi, ni kama hakulidhika na nilichokua nimemueleza.
"Mmh bado haniamini nini, ivi
huyu anajikuta nani hapa alafu hajui kama mimi ndio nimewekewa kumuoa ina maana
hajui ilo au aliniona kwa mchoro wa picha alivyokua anaambiwa kama Mimi
nitamuoa, au ameshanigundua mimi jamani au anafikiria ni kamwanaume gani haka
nilikochaguliwa aahshiii" yani nilikua na mawazo sana neno *Au*
halikunitoka kichwani.
"Mnawaza nini sasa hapa, et
binti Mfalme " Yule kijakazi ndiye alietushtua katika mawazo yale, sijui
Binti mfalme alikua akiniwazia nini.
"Shedrisa
niletee huo upanga chumbani kwangu"
"Binti mfalme, upanga wa nini
tena jaman mimi sijaja kwako kwa vita na sijui imekuaje nimekuja hapa.
Pia ningependa ujue Baba yangu
nimtumishi wa hili Jumba la Kifalme aliniacha maeneo ya hapo ili nimsubiri. Anaitwa mzee Mzenga kama tungekua marafiki
ingekua Poa sana" niliongea huku nikimzunguka, kwa wakati huo nilikua
mcheshi sana tena sana mbele ya Binti mrembo mtoto wa Mfalme. Witness binti
mfalme alikubari urafiki huo na kunipa mkono, japo niliona alikua na mashaka na
mimi hata imani na mimi hakuwanayo kabisa ila ningefanyaje sasa.
"Kwa asilimia kadhaa nimeuweza
huu mchezo" nilikua nikiwaza huku nikipokea mkono wa Binti Mfalme
Nilitoa heshima na Kuinamisha kichwa
changu chini baadae nikaamua Kuondoka zangu kuelekea sehemu aliyoniacha Baba,
"Embu subiri" Binti
mfalme aliongea huku akija maeneo yale,
"Naitwa Witness nazani jina
langu umelisikia mala kadhaa "
"Naitwa Clement, mtoto wa kiume
wa Bwana Mzenga"
"Ooh Clement, karibu
sana" Binti Mfalme aliongea.
Hata Sikujua ananikalibisha nini,
mimi niliitikia tu kwa Kuinamisha kichwa Chini,
kila mtu akaendelea na mambo yake.
"Wewe ulikua wapi" Baba
aliniuliza baada ya Kuniona,
"Niliona nakusubir kwa mda
Mrefu nikaona bora nizunguke kidogo"
"Nimeshaongea na Mfalme, ni
muda wa kuonana na Binti Mfalme kwasasa"
"Baba mimi sipo tayari na sihitaji
hiyo nafasi, hata ivyo mbona unabinti Julieth anaetamani nafasi ya Kua Malkia
kwanini usimfanyie hilo jambo akawa Mke wa Medrick"
"Unaongea nini wewe, tena
sijaribu kunieleza huo ujinga mbele ya kasri la Mfalme. Hatuna mda wa Kupoteza kwa Sasa
twendeee" Baba aliongea kwa hasira kidogo
"Baba nielewe nimesema siwezi
kumuoa Binti Mfalme na simuhitaji"
"Clement kwani binti yule
anakasoro gani, binti ni mrembo, anaheshimika kijijini na ukiwa na yule utakua mtu
mkubwa na unaweza kua Mfalme hapo badae"
“Kwaiyo
wewe baba unataka mimi baadae niwe nani? "
"Uwe Mfalme kijana wangu, wewe
hutaki madaraka huna tamaa na uongozi, hii nafasi watu wanaililia ila mimi
nimekufanyia tu Wepesi"
"Ooh sasa hapo baba
nimekuelewa, lakini Baba hakuna chochote unachowaza tofauti na mimi kua Mfalme
hapo badae, pia ni Ufalme upi unao uongelea wewe hadi Kifo cha Medrick eeh.
Yani tusubiri Medrick Afe ndio tupate utawala!
tena ili upate Utawala labda afe bila mtoto, Ukiachana na vyote mimi
sitaki utawala wala nini nahitaji kile ninachokipenda basi "niliongea kwa msisitizo
kama sikua naongea na Babaangu, mwisho
nikaanza Kuondoka.
Itaendelea
Kesho Saa
12:00 Jioni
Comments
Post a Comment