WITNESS - SEHEMU YA KUMI

SIMULIZI:  WITNESS

 

SEHEMU   YA    KUMI

" Binti Mfalme Kuna kijakazi na askari wanakuja chumbani kwako" Sauti ya yule kijakazi Shadrisa niliyemfuata ndiyoo iliyonishtua.

Tunaendelea…

 

Binti mfalme aliutoa mkono wangu mdomoni kwake na ule uliokua begani kwake akaushika haraka na kwenda kunificha kwenye kona moja iliyoko chumbani kwake.

" Utulie huko kama ukiwa mbishi utauwawa kwa kuingia huku bila ruhusa" Witness aliniambia huku akiwa amenikazia macho.

Nilisikia kama Wanaongea ongea nje ila sikujua wanaongea nini, baadhi ya vijakazi waliingia ndani na kutua masinia mawili chini hata sikujua yalikua ya nini, Mimi niliwaona ila wao hawakuniona hadi walivyotoka, Baadae Binti Mfalme alinifuata kule niliko na kunisogeza pembeni kidogo na sanduku la langu lililojengewa ukutani hadi mda huo bado alikua ananificha tu.

Baada ya mda kidogo waliingia wamama wamakamu wawili, walimkalisha Witness kwenye kiti pembeni kidogo na yale masinia mbele kulikua na Kioo kikubwa.  Niliona wale wamama wakianza kumchana Binti Mfame Nywele zake ndefu za Asili.

"Eti Mama nikweli kijana aliyekua ameandaliwa kwa ajiri yangu amekimbia" Witness aliuliza.

"Alisema anataka kwenda Kujisaidia ila mpaka sasa haonekani aliko hata iIvyo hawezi kutoka nje ya jengo la kifalme kwasababu ulinzi ni mkali na sizani kama ametoroka itakua kuna sehemu yupo ndani ya ili jengo hawezi kuondoka kwa nia mbaya" Mmama mmoja aliekua akimpamba alijibu.

"Nawasiwasi sana Mama zangu"

"Wasiwasi wako ni nini ewe binti mfalme"

"Itakuaje kama kijana huyu mimi nisimpende, au yeye nikampenda ila asinipende mimi"

Hili Swali lilinifanya nitabasam, ni bora tu asinipende maana mimi sikua tayari kumuoa huyu Binti licha ya uzuri wake na ucheshi wake.

"Wewe ni binti mfalme kila kitu kwako kinawezekana,  Ukisema ndiyo ni ndiyo na ukisema hapana basi ni hapana,  hata kama yeye akisema hapana wewe unaweza kusema ndiyo na ikawa ivyo”

"Lakini akisema hapana hata kama mimi nikasema ndiyo si hakutakuwa na upendo hapo"

"Mwanangu hakuna kitu chenye nguvu kama mazoea, hata akisema hapana ila kama akikuzoea tu kuna siku atasema ndiyo.  Mazoea hata yawe ya ugomvi kati ya mwanaume na mwanamke yana nguvu saana"

 Wale mama baada ya Kumaliza kuongea waliondoka sehemu ile, na hisi walikua wamemaliza kumpamba Binti Mfalme. Nilijitaidi kujitoa pembeni ya lile Sanduku hata ivyo tayari nilikua imechoka, nilimtaza Binti mfalme kwa kutumia kioo alikua anapendeza sana, alivutia kuliko mwanzo Sizani kama Kuna mwanaume angekataa kumuoa binti huyo pindi angemuona.

"Umependeza saana" Nilimwambia

Binti Mfalme alitabasam huku akiangalia Kwenye kioo chake "Asantee" Akanijibu.

Sikutaka kukaa tena mule ndani, nilianza kutoka ili nirudi pale ukumbuni maana nimeshajua natafutwa na kama nisingeonekana basi hili jambo lingekua kubwa

" Subiri" aliongea Witness huku akinifuata,

"Naomba leo uwe pamoja na mimi katika kambi ya Mfalme, Pia kesho unisindize sehemu katika msitu wa Nkizwa"

"Samahani binti mfalme sio kwa kupinga ombi lako ila leo si ni siku ya wewe kuonyeshwa mpenzi mwenza wako vipi kama mkiwa pamoja alafu kesho ukiambatana nami katika Safari ya Msitu wa Nkizwa hujui kama utaniletea matatizo"

Nilijua safari ya Binti mfalme ni kwa ajiri ya kupambana na dada yake Winni, Nisingeweza kuambatana na Witness hata mala moja.

"Kila kitu ni juu yangu na hakuna baya lolote ambalo litatokea" Aliongea Witness.

" Samahani Binti Mfalme unahitajika katika Chumba cha Mfalme" Shadrasa kijakazi mkubwa wa Witness aliongea

 

Niliamua kutoka nje huku nikichungulia kila pande nikaelekea ile sehemu ambayo nilimtoroka mlinzi, Nilianza kurudi kwenye ile kambi huku nikishikiria tumbo langu walinzi walikuja kunipokea na Kunipeleka sehemu ya Kukaa.

Baada ya Muda nilisikia kengele ikipiga katika jumba ya Mfalme, sikujua hii ilikua ni kengele ya nini ila mala nyingi hutumika kwakusanya wanakijiji wa Nkizwa.

 

Itaendelea

Kesho Saa 12:00 Jioni

Comments

Popular Posts