WITNESS - SEHEMU YA PILI

 SIMULIZI: WITNESS


 SEHEMU YA  PILI     

 Ghafla nilihisi mtu Kaniziba midomo na Kuanza kunivuta Nyuma nyuma kama anataka Kuniua Kwa Siri.  Nilijitaidi kufurukuta kwa Nguvu zangu zote lakini Bado alinishinda Nguvu.

Tunaendelea….

 

Alinipeleka mpaka kwenye kona moja katika Jumba la Mfalme, hapo nilijitoa mwenyewe huku nikijidai nmetumia Nguvu zangu wakati yeye tu alikua na nia ya Kuniachia.

 Baada ya Kuniachia nilijiinamia kidogo na kuanza kuhema kwa Kasi bila hata kumuangalia huyo aliekua ameniziba mdomo.

 Nilishtuka nikipigwa kofi mgongoni, "Kheee wewe" Nilishtuka baada ya kuinuka na kumuona mtoto wa kike, yani kumbe yeye ndie aliyekua ameniziba mdomo. "Upo ndani ya Jumba la Kifalme na bado Unamtukana mtoto wa Mfalme, Unajipenda wewe?"

Aliongea binti huyo aliekua amejifunika sura yake na Mask.

"Kwani wewe Nani humu, Mvamizi wewe nitakushtaki kwa Mfalme. Haya Toa hilo tambala lako Ulilofunikia Sura" Niliongea tu ili ajue nina Ujasiri lakini nilikua mwoga sana kwanza alionekana ananguvu kuliko mimi. Yule dada hakujibu kitu alikua ananiangalia tu, tena alinikazia macho kama Askari wa Mfalme,

"Eeh hapa Mpaka tutakutwa na Walinzi, Nijibu nikusaidie mimi niende kwenye kikao. Unafanya nini hapa na Umeficha Sura yako wakati sio kawaida ya Wanakijiji wa Nkinzwa" Niliongea huku na Mimi nikimuangali.

"Ooh unaenda Kwenye kikao" Aliongea huku akinishika mkono kunigeuza nyuma alafu akaniachia mkono,

niligeuka kuangalia mahari hapo nikaona kuna Watu Wamesimama nje wakiangalia Upande mwingine tofauti na tuliokua sisi, Kulikua ni ndani ya kuta ya Jumba la Mfalme.

Nilimgeukia tena ili nimuulize lakini sikumuona, ilikua ni ajabu mtu Kupotea haraka namna hiyo yaani dakika chache tu hayupo.

Nikiangalia mkononi nikaona ameniwekea unga unga mweusi ila sijui ulikua namaana gani nikauangalia kwa Umakini bado sikuutambua ikabidi niufiche tu nisijeonwa nao.

Kabla Sijapiga hata hatua nilisikia vishindo kama Watu wanakuja kwa Kasi, sikutaka kuzembea nilitembea haraka mpaka sehemu waliyokuepo wanachama. 

 

Nilifika pale na Kujichanganya na Watu,  ila macho yotee yalikua kulee nilikotoka na nilikua nawaza kazi ya ule unga niliopewa na yule dada aliejifunika macho yake,

Niliona Askari wakirudi kwenye kazi zao, sikukaa sawa nikaona watu wanatawanyika Wote hata Wanaume,  Sikujua hata kimeongelewa nini na mimi nikaanza Kurudi nyumbani.

Siku zilienda huku nikiwa bize na mambo mengine. hadi mda huo Sikuwai kuuliza wanaume waliambiwa nini pale kwa Mfalme wala Kazi ya ule unga aliokua amenipa yule dada.

 

Asubuhi nyingine Rafiki yangu mkubwa  Chande alikuja kunipitia Nyumbani na Kuniomba nimpeleke Msituni,  hata ivyo Sikua na kazi kubwa  nyumbani sikuona sababu ya kukataa.  Tulitoka nyumbani mapema na Kuanza Safari ya Kwenda huko.

 

"Ivi Chande siku mliyoitwa kwa Mfalme, Vijana mliambiwa nini" Niliamua kumuuliza Chande kwa Wakati huo. 

" Tuliambiwa tuandike Majina, Wanamtafta Kijana wa Kumuoa Witness"

"Witness??  si akatafte mwenyewe wakumuoa kwani lazima atafutiwe? "

"kwani wewe huwezi kutafutiwa Mke? " Chande aliniuliza

"Sio ivyo Kwaiyo nyie mmeandika majina huyo Witness mwenyewe mmewai Kumuona? "

"Kwaiyo wewe haukuandika jina? " Chande nae akauliza badala ya Kunijibu.

 

"Ndiyo, kwanza Sikujua kama mlikua mnaandika Majina.  Hata ivyo nampenda sana Bella wangu Sizani kama ningefanya huo upuuzi wa Kuandika Jina"

Bella alikua ni mpenz wangu wa mda mrefu, hata baadhi ya Watu walikua wanajua kuhusu mahusiano yetu,  Nilizoea kumwita Bella Ila jina lake Aliitwa Bellath.

"Kwaiyo Sisi ambao tumeandika majina hatuwapendi Wapenzi wetu? "

"Mtajua nyinyi"

 

Tulitembea mpaka Eneo lililokua mbali kidogo na Nyumbani, hapo nilimuona Chande akiangalia angalia kitu, Sikujua anaangalia nini na mimi nikaanza kupepesa macho yangu kuangalia angalia,

 

"Unaangalia nini wewe mbona mimi sioni kitu" nilimuuliza Chande,

"Naangalia mitego yangu huku" alinijibu

"Unafanya Mitego yako kwa Siri, vipi kama ukishikwa na Mfalme" Nilimuuliza Chande.

"Vitoweo vyenyewe vidogo alafu ukipata nyama Tatu, unalazimishwa Moja Uweke kwa Ajiri ya Mfalme, bora Nifanye ivi ivi tupate chakula na Mama angu"

"Unakujaga na Nani huku" Nilimuuliza Chande.

"Nakuja Mwenyewe tuu" alijibu

"Mmh mbona Leo hakuna Kitu Sasa "

"Ndio nashangaa Hata Mimi"

 

Wakati tukisogea mbele nilihisi nguo yangu kushikwa na mti, wakati naangaika kuitoa ule unga niliokua nimeuficha ukaanguka, Ulitoa harufu iliyosambaa sehemu yote ya pale,

Kabla hatujapiga hata hatua mtu alikuja mbele yetu, Alikua amefunika sura yake alikua ameshika mshale mkononi na Mishale mingine ameweka mgongoni kwenye kibegi chake alichobeba  kwenye bega lake la Kushoto.

Muonekano wa Huyu msichana ni kama yule aliekua ameniziba mdomo kwenye Jumba la Kifalme,

"Kheee ni wewe tena? " Niliuliza huku nikijitia Ujasiri lakini nilikua naogopa hatarii, 

"Clement tulia rafiki angu isijekua ndio tumekamatwa maana huku haturuhusiwi kuja" Chande aliongea kidogo huku akiuziba mdomo wake ili Yule binti asisikie.

Nilikubali wote tukatulia, yule mwanamke Alitembea taratibu na kwa ujasili mpaka pale tulipokuepo.

"Mmekuja huku kwa Kibari cha nani?  Hamjui huku ni sehemu za mipaka na Kuna uangalizi mwingi?  Nyie ndie mnaovusha Siri kwenye vijiji vya Jirani" Yule mwanamke aliongea.

Hapo ndio nilihisi kuchoka nilikua nasikia watu wamekamatwa mipakani na mala nyingi walikua wakiuawa.

 

"Kumbe tupo Mipakani? " Chande aliongea kwa Uwoga, Sijui na yeye alikua hajui kama tulikua mipakani au ndio alifanya vile ili aonekane hajui chochote.

 

Yule Mdada hakujibu kitu, alichukua mshare na kuurusha juu, sijui hata Ulienda Kutua wapi huo mshare. ghafla nilishangaa kuona Askari kama Sita wakituzunguka.

 

Itaendelea

Kesho saa 12 jion


Comments

  1. Daaaaa mwanangu unajua kutunga story yan hadi saizi sijaona kasoro hata moja big up maniga

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts