WITNESS - SEHEMU YA KUMI NA TATU

SIMULIZI:    WITNESS

 

SEHEM YA KUMI NA TATU

Mzee Kizindwa aliyarudisha maji yale kwa mala ya tatu ili niyanawe, Nilimuangalia yeye pamoja na Beseni lake alilokua amelibeba mkononi,

"Kwanini unanilazimisha Kunawa mzee, Mimi siko tayari kunawa" nilimnon'goneza Mzee kizindwa, taratibu akaanza kuondoka na Beseni lake

Tunaendelea…

Mfalme alikuja mbele yangu kwa hasira na kuamulu walinzi wanikamate,

"Nakamatwa kwa kosa gani jamani, kama sihitaji kumuoa binti Mfalme kosa lipo wapi au ni lazima" sijui niliupata wapi ujasiri wa kuongea

"Nimesema akamatwe sasa ivi na apelekwe chumba maalumu cha adhabu" Aliongea Mfalme kwa hasira, Vijana walisogea na kunikamata.

 Tukiwa katika moja ya korido ya Mfalme niliona mishale miwili ikija kwa kasi maeneo yale, niliyafumba macho yangu kwa woga, Nilisikia vijana wakipiga yowe huku wakiiachia mikono yangu, niliyafumbua macho yangu taratibu na kuanza kuangalia chini.Niliwaona vijana wale wakiwa wamelala huku wamefumba macho yao kwa maumivu,  Mishale ile iliwapiga kwenye bavu zao. Niliona mtu akija kwa kasi ya ajabu na kunishika mkono, tulikimbia katika Jumba hilo kwa siri na kwa uangalizi mkubwa, niliona walinzi wengine wakiwa wameuawa chini kwa kupigwa mishale. Tulitokea mlango mwingine kabisa tofauti na lango kuu la Jumba la kifalme, hapo niliwaona wanaume sita wakiwa na farasi, Nilipandishwa katika farasi tukaanza kuondoka kwa Kasi ya ajabu, hadi mda huo sikuona askari yeyote aliyekua akitufuata maana Waliowengi waliuwawa kimya kimya.

Tulifika sehemu tofauti kabisa sikuwai kufika kabla na kuketi hapo, Nilianza kuwaangalia wale wote niliokua nimefika nao, hakuna hata mmoja niliyekua nikimfaham. Wasiwasi ukaanza kuniingia tena, mala ya kwanza nilijua Winni amekuja kuniokoa lakini pale sikumuona hata mmoja wao ninaemfaham wote walikua ni wageni kwangu.

Kwa mbali nikaanza kusikia mlio wa Farasi aliyekua anakuja kwa kasi, nikaanza kujipa moyo labda atakua ni Winni maana kwa kasi ile haina tofauti na Winni,

Lakini ilikua tofauti na nilivyokua nimefikilia kumbe alikua ni Medrick mwana wa Mfalme, Nilianza kuomba Miungu ya Nkinzwa nisije kufa kizembe maana nilijua lazima atakua Amechukia kwasababu nimekataa kumuoa binti Mfalme (mdogo wake.

"Unajisikiaje Clement " hilo ndilo lilikua neno la kwanza, tena aliongea kwa upole hadi nilishangaa na mimi wala skumjibu kitu,

"Unajiskiaje kumkataa Witness? " aliuliza tena, nilibaki namkodolea macho yangu yangu tu.

"Ila nakupa hongera kwa kukikwepa kikombe ambacho kingekua mbele yako baada tu yakumuoa Witness" Sikuelewa Medrick alimaanisha nini nikaamua kuendelea kukaa kimya,

"Kuna kitu umekosea sana ilibidi umuoe Witness ili mipango yangu ya kufanya nitakacho iende sawa, nimekuondoa katika adhabu iliyopo mbele yako ila nakurudisha ukakubali kumuoa binti Mfalme"Sijui Medrick alikua na mpango gani juu yangu na katika Jumba la Mfalme ila kazi aliyokua ananipa ilikua ni ngumu kupokea.

"Sitaweza nasema siwezi, Yani hata kujaribu siwezi" Nilijibu kwa msisitizo

"Usilete Ubishi kijana kwanza umemuaibisha Dadaangu, ninauwezo wa kukufanya chochote nitakacho mimi na nisipate Kesi yoyote ile. Walinzi mrudisheni kwenye Jumba la Kifalme akakubari kuoa"

"Nimesema siwezi na sitaki hata uyo binti simpendi" Nilipigwa ngumi za Kifuani ambazo siwezi eleza idadi yake hata kupumua niliona Shida.

"Nimesema mmurudishe kwenye Jumba la Mfalme" Medrick aliongea kwa Hasira huku akianza kuondoka.

"Aaaghh! " Nilisikia kelele mbele yangu nilipoangalia niliona Medrick akiwa amepigwa Mshare wa bega, hata sikukaa sawa nilianza kuona wale walinzi wakianza kuanguka mmoja baada ya Mwingine.

Baadae nilikosa nguvu kutokana na Jinsi nilivyokua nimepigwa na mwana Mfalme kifuani.

 

***

Nilikuja kupata fahamu nikiwa kwa Winni, Sijui nilitumia mda gani mahali kule ila niliamka kila kitu kikiwa kinauma kichwa, kifua, Mikono, miguu pamoja na Mgongo.

"Clement umepata fahamu, Tulia bado hujapona vizuri" aliongea mdada mmoja aliekua ndani ya kambi hiyo niliopo.

"Nimetumia mda gani kukaa hapa"

"Ni kama Miezi mitano 5 ivi, tunaweza kusema umekaa takribani nusu mwaka " alijibu mdada huyo niliyemtambua kwa Jina la Sheila, alikua ni kijakazi mkubwa wa Winni.

"Miezi 5?? ni bora nikarudi nyumbani kwa sasa sijui hali ya Huko "

"Bora ubaki ili kuisaidia hali ya uko ila siyo kurudi kujua hali ya uko"

Sheila aliongea huku akitoka nje ya kambi hiyo, nikabaki mwenyewe.

 

Nilianza kukumbuka kila kilichokua kimetokea nyuma, Nilikumbuka hata mala ya mwisho niliona mwana Mfalme Medrick akipigwa mshale pamoja na walinzi wake.

"Sijui wazazi wangu watakua kwenye hali gani, Kila kitu nitasingiziwa mimi ndiye niliefanya na hakuna hata moja nililohusika, Ni bora mwana Mfalme angeniacha nikapate adhabu ya Mfalme sio kuniokoa na kunitupia kwenye shida zaidi. mimi ni mnyonge sina haki ya kujitetea nitajitetea nini mimi mbele ya Mfalme, dah!! "

 

Itaendelea

Kesho Saa 12:00 Jioni

Comments

Popular Posts