WITNESS - SEHEMU YA TANO

 

SIMULIZI: WITNESS

 

SEHEMU   YA TANO   

"Bila shaka kijana Mwenyewe ndio huyu" Aliuliza mfalme

"Ndiyo yeye Mtukufu" Alijibu Baba.

"Mmh nimefanyaje tena Mimi" Nilikua nikiwaza kwa Hofu, Nilitamani kumuuliza Baba kipi kinaendelea lakini huo Ujasiri ningeutoa wap?

Tunaendelea…

 

Mfalme aliniangalia kwa umakini kama Kuna kitu anakikagua mwilini mwangu,

"Unatakiwa uanze mazoezi Kijana, na utafanya pambano kubwa unatakiwa uwe mshindi katika hili" Mfame Ngabeli aliongea.

Sikua nimeelewa alikua na maana gani Mfalme, ila niliitikia kwa Kuinamisha kichwa changu chini.

 

Baba alinishika bega na Kuanza kunitoa nje ya Jumba la Mfalme,

"Mpaka sasa sielewi mlikua mnaongea kuhusu nini" nilimuuliza Baba.

"Unatakiwa Kumuoa Binti Mfalme Witness"

Baba alipoongea ivyo ni kama Alikua amenichanganya, sikua na hata chembechembe ya kutaka Kumuoa Binti mfalme.

"Baba hii inawezekaneje wakati mnajua tayari ninamahusiano na Binti mwingine. mimi siwezi Baba"

"Ndio jina lako limeshateuliwa ivyo, Hauna jinsi" Baba aliongea kama yupo bize na mambo yake hata hakujari kuhusu mimi.

"Baba Mimi sikuandika jina, hilo jina lililoteuliwa limetoka wapi"

"Nimechoka sasa nahitaji kupumzika"

"Lakini ilibidi unisikilize, na mimi ninahaki kwa hili jambo"

"Kaitumie hiyo haki kwa Mtukufu mfalme, Mim ni baba yako na nimeshaamua wewe hiyo haki unayoizungumza ni haki gani?  Au haki upuuzi?  Clement tulia" Baba aliongea kisha akaondoka zake.

 

Nilitembea Hadi Nyumbani kinyonge sana, kiukweli sikua na furaha tena.  Nilifika Chumbani na kulala, lakini nilikua na mawazo juu ya kile alichokifanya Baba, mda Mwingine niliwaza jinsi gani itakavyokua kama nikimuoa binti Mfalme na wakati mwingine niliwaza tukio nililofanya kwa siku ya leo.

"Binti mfalme, binti mfalme si Ameshaniona katika Kundi la wasaliti, tena nilimshikia panga huku nikitaka kuokoa maisha ya Dada yake. dah" Yote yalikua ni mawazo ndani ya Kichwa Changu.

 

Nilisikia ndege wakiimba, Jua liliangaza ndani ya chumba changu kulikua kumekucha, bila shaka ilikua ni asubuhi. Hata Sikumbuki nililala wakati gani na hisi ni kwa sababu ya uchovu pamoja na mawazo.

Asubuhi hiyo nilipata wazo la kwenda kumuona Chande, Tangu jana Nilivyomuacha katika kambi la wasaliti  hatukuonana nae tena.

 

Nilitoka kwenye kichumba changu kwa uchovu mpaka njee, Huko nilimuona mdogo wangu Julieth Alijiandaa kwenda mtoni kuchota Maji.

"Chande alikuja Jana kukuangalia mara mbili, lakini hakukukuta sijui ulikua wapi" Aliongea Julieth.

"Jana nilichelewa Kurudi lakini nitaenda kumuona hata Sasa"

 

Nilitoka nyumbani ili nikamsimulie Chande kile kilichokua kimetokea na Mpango wa Baba kwangu ambao sikua nimeridhika nao.

"Kwaiyo Jana ukaamua unikimbie, vipi kama wangekuua? " Chande aliniuliza baada ya Kufika.

"Niliona ni bora nimsaidie yule dada, Maana nilimuona kabla.

"Kwaiyo ewe na yule mtu mnafahamiana nae, na nilijua tu ule mpango wa sisi kukamatwa uliupanga wewe.  Ivi Clement ulimsaidia tu mtu yule pasipo Kumjua eti kisa ulimuona kabla?"

Chande aliuliza kwa hasira, nilibaki nikimshangaa yani kwa mda ule ni Kipi kilichomfanya apate hasira ya ghafla.

"Chande kwani shida nini mimi kumsaidia yule?  Alafu sikuja kwa nia hiyo nashukuru ulifika salama jana, Ila ninajambo jipya Chande"

"Jambo gani hilo?  La kushirikiana na wale watu alafu ni kwanini waishi polini wanaonekana ni wasaliti wale, Clement unawasiliana na wasiliti hili jambo lazima lifike katika Ufalme"

"Chandee" niliita kwa hasira, yani sikua nimeamini kama Chande rafiki angu mkubwa ndo ananibadilikia vile.

 

"Clement unawasiliana na wasaliti, ulimshikia binti mfalme Panga kisa wale wasaliti.  Alafu et unataka ukamuoe binti Mfalme?  Sijui nani kakuteua wewe, Yani hata Jina hukuandika et umechaguliwa kumuoa binti Mfalme, Clement wewe ni sawa na msaliti tu"

 

Sijui Chande aliyapata wapi haya maneno na sijui ni mda gani yalimfikia.  Kumbe hii taarifa ndio iliyomchanganya Chande na Kuanza kunijibu mimi majibu ya ovyo kabisa.

"Chande nampenda binti mfalme? " Nilimuliza.

Chande hakunijibu kitu, alichukua kibuyu chake na kutoka nacho nje.

Nilibaki nikimshangaa Chande, yani Jana tulikua sawa masaa machache haya kanibadilikia ivi.  *Kweli kuna watu wasiopenda kuona ukipata bahati hasa marafiki zako wakaribu* Lakini mim mwenyewe Sikua tayari kumuoa Witness.

"Chande ulijuaje kama yule ni binti Mfalme"

"Si uliniacha nae pale, yeye ndiye aliyeniokoa na ameniambia wale wanateka vijana na kuwaingiza kwenye kundi lao"

"Kwaiyo unamaana hata sisi tungeingizwa kwa kundi lile.  Na hii taharifa Ya Kumuoa binti Mfalme Umeitoa wapi? "

"Aliniambia babaako kipindi anakuulizia, alaf usijifanye hujui kitu kwanza unanichosha hapa na nahisi ulitaka kuniingiza kwenye kundi la waasi wewe" Chande aliongea huku akiondoka.

 

Nilianza Kutembea taratibu kuelekea Nyumbani.

"Clement " Nilisikia nikiitwa nyuma, sauti haikua Ngeni hata kidogo kwangu, Huyu alikua ni mpenzi wangu Bella (Bellath) kwa jina alilopewa na wazazi wake.

"Bellath, Mbona ivyo" Nilimuuliza Bella alionekana ni mtu wa Hasira sana.

"Kwani wewe hujui?  Clement niliyoyasikia ni ya kweli?"

Niliushika mkono wa Bella kibishi mpaka sehemu ya pembeni kidogo,

"Nijibu Clement ivi ni kweli unaniacha mimi na Kwenda Kumuoa binti Mfalme?  Najua hiki kitu huwezi kukiepuka na unajua kwako ni kama bahati sana kua na Binti Mfalme, lakini Fikiria kuhusu Mimi Clement" Bella aliongea kwa huruma.

"Nani kakwambia hayo Bella, Alafu haya mambo hayana ukweli wowote ndani yake, Mimi nipo tayari kwa lolote kwa ajiri yako kwasababu nakupenda.  Tunaweza hata kutoroka na Kwenda vijiji vya jirani kuishi pamoja kama hili litatokea, ila Amini hakuna ukweli wowote kati yangu na Binti Mfalme"

"Clement unanifanya mimi mtoto siyo?  Hakuna nisilojua kati yako wewe na Binti Mfalme, haya Jana umeshinda wapi wewe siku nzima?  Kwa binti mfalme eeh, ila nakutakia siku njema" Bella aliongea kwa huzuni na kuanza Kuondoka.Sikutaka kumzuia kwani niliona ni jinsi gani alivyokua akiumia.

"Masikini Clement Mimi" niliongea huku nikikaa chini.

 

Itaendelea

Kesho Saa 12:00 Jion

Comments

Popular Posts