WITNESS - SEHEMU YA KWANZA
SIMULIZI: WITNESS
Kwa Majina naitwa Clement Mzenga ni
mtoto wa Pili katika familia ya Bwana Mzenga, nina dada Mmoja (Dayana) na mdogo
wa Kike(Julieth).
Dayana ni dada mkubwa kabisa katika
familia yetu. Yeye alishaolewa toka mda mrefu ila bado hajabahatika Kupata
mtoto, Sijui ni Mpango wake na Mmewe waliojiwekea kua watazaa baadae au
laah. Julieth ni mdogo wangu yeye bado
yupo tu nyumbani akimsaidia mama Shughuri za Nyumbani.
Kijiji chetu cha Nkinzwa
kinaongozwa na Utawala wa Mfalme Ngabeli ni Ufalme wa 6 toka Kuwekwa kwa Mipaka
ya Utawala na Vijiji vya Jirani,
Mfalme Ngabeli Anawatoto wawili tu
wakike na Wakiume, Medrick na Witness. Medrick ndie mtoto anayesubiriwa Kua
mtawala mtalajiwa, Wasichana wengi wa Kijijini wanatamani Kuolewa na Medrick
hata Mdogo wangu Julieth.
Ilikua ni Siku ya Jumanne, Asubuhi
ya siku hii niliamka na Furaha si kidogo. Sio kua nilikua na bahati labda ya
Kupata kitu cha Thamani hapana ila ni Furaha tu niliyokua nimeamka nayo Siku
hiyo. Nilitoka njee na Kumkuta Mama yupo bize akimwaga mtama kama anawaita
Kuku,
"Kwanini Unafanya hivyo Mapema hii, Kuku si wametoka sasa ivi tu Unataka kuwarudisha Bandani tena? " Nilianza tu Kuuliza bila Salamu.
"Kunaj Jambo kwa Mfalme, Watu
Wameshakusanyika. Na wanaume wameenda mda kweli kwasababu waliitwa toka mapema,
wewe bado Umelala tu mpaka saizi"
Mama aliongea huku akiwa bize
kumwaga mtama wake, Kuelekea Bandani na Kuku wakaanza kukusanyika kuufwata
mtama huo.
"Khaaa Lakini kwanini
hukuniamsha Mama, Unajua Wakiona sipo huko Kitatokea nini? " Niliongea
huku nikishikilia kichwa. Nilijua taarifa ikifika kama Sipo hapo kitakachofuata
ni adhabu ya Kukiuka Agizo la Mfalme.
"Wewe Umeamshwa saana tu na
Mdogo wako Ukajifanya Unajua kukoroma tu. Ndio Ufanye haraka kabla
haijajulikana haupo na hauna tatizo Lolote, Si hua unaona Vijana wenzio
wanavyopewa adhabu wasipoenda" Mama Aliongea.
"Mama basi Ukienda kawape
taharifa Kua mimi ni mgonjwa, nimeshachelewa wataniuliza Nilikua wapi. Alafu umesema
vijana ndio waliitwa Mwanzo, Mimi niende saivi Kweli" Niliongea huku
nikiwaza njia nyingine ya Kufanya.
Kabla mama Hajajibu kitu kengele ya
jumba la Mfalme ilipigwa tena, Sijui Kulikua na nini huko kwa Mfalme.
"Wewe nenda haraka geti la
kule nyuma walinzi wengi watakua wameenda kwenye Kikao hicho, waliobaki ni
Wachache kaongee nao uende watakuelewa. Hiyo kengele inatutaka tufanye haraka
Sisi tuliobaki huku wamama na Mabinti wengine" Mama aliongea huku
akizifungia Kuku mlango.
Nilichukua mshare wangu mdogo
ninakopenda kutembea nako na nilikatengeneza mwenyewe, Safari moja kwa Moja
geti la jumba la Mfalme. Nilifika hadi getini na Kuona lipo Wazi, hakukua na
Mlinzi hata mmoja hapo getini,
"Kuna nini Leo hadi hapa
hakuna Walinzi, Au Mfalme ndio Ametoka Rasmi ndani ili kuongea na
Wananchi" niliongea huku nikiingia kwa tahadhari sana nisije pigwa mshare
wa Shingo na Walinzi.
"Mmh yani kama Mfalme ametoka
basi hako kabinti kake katakua kametoka maana na kenyewe sijui kana jiona ni Ka
Mfalme, kazi kujifungia ndani kama ndege wa kufugwa, Nataka nione icho kisura
chake Usikute Sura Imekunjamana kama ya Baba ake" nilizidi kuongea huku nikipiga
hatua kwa tahadhari.
Lakini ghafla nilihisi mtu Kaniziba
mdomo na Kuanza kunivuta Nyuma nyuma kama anataka Kuniua Kwa Siri. Nilijitaidi kufurukuta kwa Nguvu zangu zote
lakini Bado alinishinda Nguvu.
Itaendelea
Kesho 12 jioni
Nzuri sana Kaka
ReplyDeleteGood brother keep it up
ReplyDeleteGood kk
ReplyDelete