WITNESS - SEHEMU YA KUMI NA NNE
SIMULIZI: WITNESS
SEHEMU YA KUMI NA NNE
Nilianza kukumbuka kila kilichokua kimetokea nyuma, Nilikumbuka hata mala ya mwisho niliona mwana Mfalme Medrick akipigwa mshale pamoja na walinzi wake.
"Sijui wazazi wangu watakua kwenye hali gani, Kila kitu nitasingiziwa mimi ndiye niliefanya na hakuna hata moja nililohusika, Ni bora mwana Mfalme angeniacha nikapate adhabu ya Mfalme sio kuniokoa na kunitupia kwenye shida zaidi. mimi ni mnyonge sina haki ya kujitetea nitajitetea nini mimi mbele ya Mfalme, dah!! "
Tunaendelea…
Baada ya Mda Winni alikuja mahari pale kuniangalia, nadhani Sheila alimpa taharifa ya kuamka kwangu.
" Pole sana Clement "
"Asanteee, Vipi ni nini kinaendelea Nkizwa"
"Yanayoendelea pale ni makubwa ila acha mimi nikupe pole tu "
"Nahitaji kurudi Nkizwa Winni"
"Hata sasa upo NkizwakKwani unahitaji kurudi Nkizwa ipi"
"Kijijini, nahitaji nikawaone ndugu zangu, nataka nikamuone Bella wangu". Winni alikaa kimya
"Hutakiwi Kufanya ivyo bado ni mapema mno Clement " Sheila akaongea
"Haijalishi mimi nitaenda tuu"
"Sawa hakuna Shida" Winni aliitikia huku akiwa ameinama hakuonekana kufurahia mimi kwenda kijijijni, ila hakutaka kubishana tu.
Jioni ya siku ya pili niliwasili kijijini Nkizwa hakuna akiyeweza kuniona kwasababu kulikua na giza. Nilikua bado sijapona vizuri kwasababu hata baadhi ya viungo vyangu vilikua vinauma, Safari yangu nilikua nimeongozana na Winni. Tulitembea moja kwa moja hadi kwa Bella kwasababu nyumba yao ilikua ni jirani kutoka eneo nililokua nimetokea msituni. Nilimuona Bella akiwa amekaa pembeni kidogo ya gogo huku macho yake akiwa ameyaelekezea kwenye mwezi, alionekana ni mtu anae waza kitu, Nilifika nyuma yake na kumshikia bega lake, aligeuka kuniangalia kwa Wasiwasi
"Clement " Aliongea Bella huku akija kunikumbatia, lakini aliacha ghafla huku akipiga hatua za Kurudi nyuma hadi mimi nikashangaa, Niligeuka nyuma nikamuona Winni
"Niliishika mikono yote miwili ya Bella nikaizungusha kwenye mwili Wangu na kumruhusu afanye kile alichotaka kukifanya.
" Bella alinikumbatia lakini kwa Wasiwasi sana"
"Umeoa eeh, umemuoa tena Binti Mfalme Clement na ndiyo maana umekuja kwangu"
Bella aliongea huku akininong'oneza bado alikua amenikumbatia. Nadhani aliongea vile baada ya kumuona Winni, Siku hiyo Winni hakuficha Sura yake, Licha ya Winni kukaa nje ya nyumba la Mfalme hakuacha kuvaa vitu vyake vya Thamani kama Cheni, hereni, mikifu, bangili na Mapambo ya Nywele zake, bado alionekana ni bora zaidi.
"Mimi sijaoa Bella na sijamuoa Binti Mfalme ivi unajua nimerudi kijijini hapa kwa ajiri yako Bella. vipi unaendeleaje na Familia Yako"
"Tunaendelea vizuri tu" Alijibu huku akijitoa kifuani kwangu, Nilitamani abaki pale kwa da Mremfu lakini nisingemzuia kutoka. "Umeonana na Julieth Wanaendeleaje wao? "
"Vipi kwani Hujapitia Nyumbani Kwenu"
"Sijapitia bado saizi Ndio nafika kijijini"
Bella alikaa kimya, hakunijibu swali langu.
"Wanaendeleaje kwani" Bella aliendelea kukaa kimya"Bellath si nakuuliza wewe? Au kuna tatizo nyumbani? Kama kuna kitu usinifiche Bella"
"Clement hawaendelei vizuri hata kidogo, Unajua kutoroka kwako kulitangazwa kila sehemu na hadi sasa unatafutwa kwa kosa la kumjeruhi mwana wa Mfalme na kuwauwa walinzi wake, Baba yako alikamatwa kwa kosa lako na Familia yako ipo chini ya uangalizi mkali pia--" Kuna kitu alitaka kuendelea kuongea lakini aliacha niliangalia alipokua anaangalia macho yake yalikua ya namuangalia Winni, Nilisogea hadi pale alipokua amesimama Winni
"Et haya nayoyasikia ni kweli Winni, Mbona hukuniambia baada ya mimi kupata fahamu, Inabidi niende nyumbani kwetu sasa" Niliongea huku nikianza kuondoka
Winni alimwita Bella sijui hata alimwambia nini ila nilimuona Bella akinifuatilia nyuma yangu tena kwa wasiwasi.Tulitembea hadi Nyumbani kwetu, nilishangaa kwa mazingira niliyokua nimeyaona pale, Ni tofauti kabisa na nilivyokua nimeacha. Kwa hisia za haraka nilijua hakuna hata mmoja aliekua akiishi pale, Kulikua ni kuchafu na nyasi zilianza kuota ovyo.
"Bella kuna yeyote anayeishi humu ndani kweli? " Nilimgeukia Bella
"Unatakiwa kuingia ndani, Ukionwa hapa nitatizo lingine" Bella aliongea huku akiangaza macho yake huku na huko kwa Wasiwasi.
"Nambie ukweli Bella wazazi wangu wapo wap? "
Bella alinishika mkono akaniingiza ndani, Vitu vilikua vimepangwa vizuri tu,
"Hii nyumba Julieth mdogo wako aliniambia niiangalie na kulinda kila kitu kilichopo humu tuliamini ipo siku utarudi tu"
"Nawao je wapo wapi"
"Baba yako anasubiri adhabu ya kumdanganya Mfalme"
"Kumdanganya kuhusu nini"
"Kua ulikua tayari kumuoa binti Mfalme kumbe sivyo"
Nilijisikia huzuni sana kuona ni namna gani familia yangu inateketea bila kosa, Kama Baba asingenichagua mimi kumuoa binti Mfalme basi vijana wengine wangefanyaje mashindano ya kuchaguliwa mshindi wa kumuoa binti Mfalme. Hii yote ilitokana na tamaa ya Baba ya madaraka katika jumba la kifalme kweli *Tamaa mbele mauti nyuma*.
Itaendelea
Kesho Saa 12:00 Jioni
Comments
Post a Comment