WITNESS - SEHEMU YA NNE

SIMULIZI: WITNESS

      

SEHEMU YA NNE

"Uliemsukuma pale ni Witness, ni Mtoto wa Mfalme, vipi utarudi kijijini Kwenu ikiwa ameshakuona Sura yako na amejua unashirikiana na sisi au utabaki hapa?" Winni aliniuliza

Tunaendelea…

 

"Mmh Witness, mtoto wa Mfalme?  na kwanini mnapambana na mtoto wa Mfalme hamjui kuwa ni hatari kwenu?? " niliuliza

"Jali kuhusu wewe kwanza, au kubarii kua miongoni mwetu" Aliongea yule Winni

"Kwani na nyie ni kina nani na kwanini mlitukamata, na ulinipa ule Unga ili unikamate haraka au? "

"Sisi ni Wanakijiji wa Nkizwa, Mimi ni Winni, Dada yake Medrick na Witness.  Ila sipendi uongozi wa Baba yangu, siku zote nimekua mtu wa Kupinga vikali kila anachokifanya Baba, ni Utawala usiokua na amani utawala wa mabavu, wanakijiji hawana amani na maisha yao. Kosa dogo tu adhabu kubwa, kijiji kimetawaliwa na vifo, Yani hakuna amani kama mwanzo.  Sasa hicho ni Kijiji au uwanja wa Kifo"

 

Ni kweli baba yake alikua akifanya maovu sana, hakukua na amani ya wanakijiji yani Kosa dogo tu unawaza adhabu ya Kifo.

 

"Ooh sasa umeamua nini mtoto wa Kike" niliuliza maana niliona asingeweza mapinduzi mtoto wa Kike, badala angeishia Kufa tuu.

"Kila kitu nitakwambia kesho hata hivyo mda umeenda sana na ni Jioni sasa, ila hakikisha hiki nilichokwambia humwambii mtu, popote ulipo na Mimi nipo kwasababu unaharufu ya unga wangu hapo ulipo pia nisaidie kuongeza Vijana wakufanya nao mapinduzi, Na ukijaribu kutoboa siri hii amini kua nitakuua kwa mkono wangu."

" Kwaiyo unaenda kwenye jumba la kifalme na Kijijini ili kuteka vijana wa kuwaongeza kwenda kambi yako, na hutaki nimwambie mtu eeh sasa hao vijana nawaletaje kwenye kambi?  Ila sawa nahitaji kurudi kijijini kwetu njia ni hipi? " niliuliza huku nikikuna kichwa.

 

"Panda Kwenye Farasi " Aliongea Winni huku akisimama kuelekea Upande wa Farasi.

 

Maeneo hayo kulikua na upepo ule ambao umeambatana na baridi kwa mbali, nilisimama Kwa kujikunyata huku nikielekea kwenye Farasi wakati huo Winni alikua ameshapanda Ila Ananiangalia mimi tu.

Nilisimama pale kwenye Farasi na Kuanza kumuangalia Winni.

 

"Panda tuondoke huoni tunachelewa"

Nilibaki nikimuangalia Winni nilitamani kuiona Sura yake lakini ningeionaje, alionekana ni binti mzuri sana, sikutaka Kuondoka bila Kuiona Sura yake. 

 

"Ivi Unajua hatuna mda wa Kupoteza, inabidi ufike mapema kabla Walinzi hawajakaa pembezoni mwa msitu kuweka ulinzi"Aliongea Winni, alionekana asiyependa kufanya mambo yake nje ya Wakati, alikua ni binti makini na kazi yake.  Nilitamani kumfahamu vizurii ila mda Haukuruhusu.

Nilipanda kwenye Farasi na Safari ya kurudi kijijini ikaanza.  Mda wote binti alikua akinisimulia baadhi ya mambo na kunifunza kuwa Shujaa. Lakini alizidi kunisisitiza nifanye Siri mambo hayo maana ningefanya ujinga ningekufa.  "weee! na nilivyokua muoga Kufa, niliahidi kufanya Siri".

 

Tulifika pembezoni mwa Msitu Nkinzwa, Winni alishuka na kunitaka na mimi nishuke. Nilikua na hamu ya kuiona Sura yake, nilitamani sana kuijua sura ya Winni watoto waliopewa majina ya Hadhi yao hapo kijijini.

Nilishuka huku nikimshika bega lake, Mkono mwingene nilishika mgongo wa Farasi, wakati naweka miguu chini nilitumia mkono niliokua nimeweka Begani kwake kumfunua Kitambaa Usoni.

"Winni" niliita baada ya Kuiona sura yake, Alikua ni binti mzurii, Mapambo kama hereni na cheni za shingoni bado zilikua mwilini kwake, Sura yake ilikua na Rangi ya kuvutia.

 

Nilishtuka baada ya kupigwa kofi Shavuni, Winni alikua ananiangalia tena kwa Macho makavu, nilijua nilikua nimetenda kosa kubwa kuiona Sura yake lakini ningefanyaje wakati nilitakiwa kuiona. 

"Aah Samahani kwa hilo" Niliongea huku nikishikilia Shavu langu.

Winni hakuongea kitu, alichukua Farasi wake na kuondoka zake, Nilihisi alikua amechukia sana  na alikua na uwezo wa Kunifanyia kitu ila hakuamua tu mimi pia nilijisikia vibaya.

 

Nilifika Nyumbani huku nikiwa Nimechoka si kidogo, hapo ndipo nilipoanza kuona njaa Yani mda wote sikua nimekula Chochote.

"Ulikua wapi tangu Asubuhi, yani tunakutafuta Kama Mtoto mdogo.  Baba yako anakuhitaji kwenye Jumba la Mfalme" Mama Aliongea baada tu ya Kuniona.

Sikuhofia kuhusu Kuitwa na Baba, Kwasababu alikua ni Mtumishi katika Jumba la Mfalme nilizoea kuitwa maeneo hayo.

"Sawa Mama nitaenda"

Niliingia ndani kula Chakula kilichokua kimewekwa kwa ajiri yangu, Lakini muda wote Mama alitaka kujua nilikua wapi, alikua akinichunga kama mtoto. umri wangu ulikua umeenda hatua ambayo ingenibidi nioe ila sikutaka kufanya ivyo mapema kwasababu Kijijni kulikua na sheria nyingi hata Kama shughuri ni yako mwenyewe.

Baada ya kila kitu nilitoka kwenda kusikiliza wito wa Baba, Hadi mda huo tayari ilikua usiku sana.

Nilifika na kuwaelezea Walinzi shida yangu, hawakua na shida kwasababu walimfahamu vizurii mzee wangu. 

 

Mlinzi mmoja alitoka na baadae alikuja na Baba, nilishikwa mkono na moja kwa moja nikaanzwa kuingiza kwenye Jumba la kifalme.

"Tunaenda kufanya nini Baba? " niliimuliza

"Kwanza siku nzima ulikua wapi? "

"Polini, kutafta chochote kitu"

"Ivi Wewe unaakili kweli, vijana wenzio wapo kwenye harakati za kutafta Kumuoa binti Mfalme, wewe eti ulikua polini"

"Aah lakini baba mimi hicho kitu…." Kabla sijamalizia kujibu tulikutana na mtu wa makamo,  alikua amevalia vizuri tu na alikua amependeza kuliko kawaida kwa mapambo ya Thamani yaliyo kua kwenye mavazi na mwilini mwake.

"Nkinzwaaiyeee"

"Iyeeee nkinzwaiyeee"

Baba alitoa salam na yule mtu aliitikia pale ndipo nilipojua yule ni Mfalme mwenyewe Ngabeli na mimi ikanibidi nitoe Salami kwa mtawala wetu.

"Bila shaka kijana mwenyewe ndio huyu" Aliuliza mfalme

"Ndiyo yeye Mtukufu" Alijibu Baba.

"Mmh nimefanyaje tena Mimi" Nilikua nawaza kwa Hofu, nilitamani kumuuliza Baba kipi kinaendelea lakini huo ujasiri ningeutoa wapi?

 

Itaendelea

Kesho saa 12:00 Jioni

  


Comments

Popular Posts