WITNESS - SEHEMU YA NANE

 

SIMULIZI:  WITNESS

 

SEHEMU YA   NANE

"Ooh sasa hapo baba nimekuelewa, lakini baba hakuna chochote unachowaza tofauti na mimi kua Mfalme hapo badae, pia ni ufalme Upi unao uongelea wewe hadi Kifo cha Medrick eeh. Yani tusubiri Medrick Afe ndio tupate utawala!  tena ili upate utawala labda Afe bila mtoto, Ukiachana na vyote mimi sitaki utawala wala nini nahitaji kile ninachokipenda basi “. niliongea kwa msisitizo kama sikua naongea na Babaangu,  Mwisho nikaanza kuondoka.

"Clement" Baba Aliita kwa hasira na Sauti ya Juu nadhani kila mtu aliekua karibu nasi aliisikia sauti ile. Mimi sikujali hilo, niliendelea na safari yangu.Kama Winni alikuepo mahari pale basi nilihisi chochote ambacho kingetokea yeye angenisaidia.

 Ilipita Wiki moja bila mimi kuonana na baba yangu, Chumba changu cha kulala kilikua nje ya nyumba kubwa.  Nilijitaidi kumfanya Bella aniamini zaidi na kwa asilimia kadhaa nilifanikisha jambo hilo, Pia sikuacha kuongea na Chande japo kwa kiasi alionekana kubadilika hakua upande wangu kama mwanzo ila sikujali hilo. nilijua Chande hakutaka mimi nimuoe Binti mfalme kwasababu nayeye ni mmoja wa vijana wanaoipenda hiyo nafasi lakini mimi wala sikua na lengo lakua na binti Mfalme nahis kama angelijua hilo basi asengenichukia, ila ndio ivyo *Aichukiaye nafasi yako mfanye ngazi ya kutimiza malengo yako*.

"Unajua Clement saivi sikuelewi kabisa, alafu wewe si Baba ako aliniambia umechaguliwa kumuoa binti mfalme. Mbona sasa upo kama sio mtu mkubwa wa badae"   Siku moja Chande aliniuliza,

"Ooh kumbe hii taarifa alikupa Baba, Umesema hunielewi?  Hunielewi kwa lipi sasa Chande" Nilimuuliza.

"Vipi kuhusu mpango wa kumuoa binti Mfalme unaendaje" Aliniuliza Chande

" Mi hata sijui kinachoendelea hapa"

"Hujui vipi wakati wewe ndiye muhusika wa tukio hilo rafiki yangu na vipi kuhusu mpenzi wako Bella nakumbuka ulisema unampenda ndiyo maana hujaandika jina kwa Mfalme"   Ni kama chande alikua akinidadisi ivii sijui alitaka nini kwangu.  Sikuona haja yakumjibu Chande, nilimuachia uwanja mkubwa wakuongea na kuuliza pasipo majibu.

Ilipofika Jioni niliamua kurudi nyumbani, Zilibaki siku chache tu Atakae muoa binti mfalme atangazwe.  "Sijui wataweka mashindano ya ijana ili mshindi amuoe binti mfalme au Ndo wameshanipigia mahesabu mimi" Nilikua nawaza hayo huku nikiendelea na safari yangu. Sikupiga hatua nyingi niliona mtu mbele yangu, kwajinsi alivyokua amevaa niligundua mtu huyo atakua ni Winni,yaa alikua ni Winni.  Niliangalia upande wa kulia na ushoto, Nyuma na Mbele sikuona mtu, nikimshika Winni mkono na kumvutia sehemu ya kichaka.

"Wewe umekuja kufanya nini hapa, unataka kuniletea shida Winni" niliongea kwa Jazba.

"Shida ya nini sasa tambua hiki ni kijiji changu naweza kuja mda wowote tu hapa mpaka pale nitakapotimiza haja yangu, pia sikuja kwa maana nyingine ila ninachotaka kukwambia ni Kua nyumbani kwenu wametumwa Askari wa Mfalme"

"Nini? Askari wa Mfalme, Kufanya nini sasa nyumbani" Niliuliza kwa mshangao

"Unakosa la kukaudi amri ya Mfalme na Kama utakataa amri hiyo mbele ya wanakijiji basi itabidi upate adhabu"

"Ooh Clement mimi, adhabu hiyo ni Kifo hakuna adhabu nyingine, sasa unanishauri nini Winni"

"Kubali Kuolewa na Witness"

"Siwezi Winni, yani siwezi hata kuigiza nampenda Witness.  Mbona nafasi hii wanaipenda vijana wengi na mashujaa"

"Mimi naondoka ila fikiria hicho nilichokwambia, Utakufa kizembe na huyo Bella wako ataolewa na mwingine.  Wewe kubari kumuoa binti mfalme na badae utamuoa bella kama Mke Mwingine kwasababu hiyo nafasi utakua nayo nje na hapo utanisaidia mimi Kumuondoa mfalme na utawala wake"

"Hivi Winni Mfalme ni Baba ako kabisa? "

"Kila siku nakujibu kitu kama hicho"

"Kama ni Baba ako kwanini Mnapambana na Binti mfalme kama siyo ndugu. wala Binti hajalisema hilo kwenye ufalme, kwanini Ukaungane na watu nje wakati unaweza kua mtawala ndani ya Jumba la kifalme"

"Clement acha kuwa mjinga, Baba hawezi Kukubali kutawaliwa yule hata Medrick mwenyewe atatawala mpaka kifo cha Mzee. Siku zote nilikua napingana na Baba kuhusu utawala wake na ninajua siri yake kua yeye ndiye aliyehusika na kifo cha Mama, Mzee huyu ananichukia sana kuna mda alitamani kuniuwa hapo ndipo nilipoamua kutoroka, Watu wengi wanajua nimekufa"

"Sasa kwanini unagombana na Witness? ni kwanini anakuja Kwenye kambi yako na kupambana na wewe? "

"Witness anapambana na Mimi kwasababu amelishwa sumu ya uongo, Mama alikua akigombana na Baba kuhusu utawala wa Mfalme usiopendwa na watu, Kuna siku Baba alichukia sana kutokana na vile alivyokua akiambiwa na Mama Hasira zake zikapelekea kumuua Mama mbele ya Macho yangu. Winni aliangalia sehemu za Pembeni kama Mtu yeyote anakuja mahari pale, alipohakikisha hakuna mtu aliendelea kuongea

"Siku Baba alipojua nimeona kifo cha Mama alitaka kuniua, mimi niliamua kutoroka kwaiyo katika Jumba la kifalme wanajua nilimuua Mama na nikakimbia adhabu kwasababu Mfalme alidanganya ivyo.  Kuna mambo mengi yanayoendelea katika Jumba la Kifalme na Wanakijiji hawajui, pia unataka mdogo wako aolewe na Medrick ili wewe umuoe Bella si ndiyo "

"Yaah ni kweli, kama Julieth akiolewa na Medrick basi mimi sitopata usumbufu wa kumuoa Witness"

 "Clement nakuhakikishia hata mwanamke atakae kubari kuolewa na Medrick basi Mfalme atataka kumuingilia kimwili ili kuhakikisha kama binti huyo ni mschana kweli au laah,  kama siyo msichana Binti huyo atakua ameishia tu kuingiliwa na Mfalme lakini hataolewa na Kijana wake na Kama Binti huyo atakataa kuingiliwa kimwili na Mfalme basi atauliwa,  Clement mlinde sana mdogo wako katika hili" Winnie aliongea na kuondoka kwa Kasi ya ajabu sana.


Itaendelea

Kesho Saa 12:00 Jion

 

Comments

Popular Posts