WITNESS - SEHEMU YA KUMI NA MBILI
SIMULIZI: WITNESS
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Baada ya Muda nilimuoana Witness akiiletwa mahari pale huku akiwa ameongozana na kijakazi wake wa Karibu Shadrassa pamoja na wengine wawili. Alikua amependeza haswa mavazi yake ya mapambo na Cheni za Kun'gara zilizidi kuupendezesha uzuri wake, Kiufupi Witiness alipendeza, Nilimuona binti Mfalme kwasababu mimi nilitangulia kufika mahari pale ila yeye hakuniona mimi.
Tukiwa pale nilimuona Mfalme akisimama ili kuongea baadhi ya maneno, watu walikua wametulia.
Tunaendelea…
Watu walikua wakisubiri kile walichoitiwa, Baba alikua mbele kabisa upande wa wazee wenzake na washauri wa Mfalme.
"Nkizwa yeee" Alisalimia Mfalme huku akiunyoosha mkono wake wakulia,
"Iyee Nkizwayeee Nkinzwa iyeee" Wanakijiji waliitikia huku wakiinyoosha mikono yao kama wanashangilia Ushindi.
Mfalme aliirudia Salaam, na Wanakijiji wakaiitikia salamu yake kama mala tatu ivi.
Mfalme alikohoa kidogo kisha akageuka kuwaangalia wazee wa baraza lake, akamuangalia na Binti yake kisha akaendelea,
"Nimewaiteni hapa ili kuwashilikisha yale yanayoendelea hapa kijijini kama wanakinzwa, Kuna mda nilihitaji majina ya vijana ili kujua idadi na Kufanya mashindano kwa ajiri ya kumpata kijana hodari wa Kumuoa Binti yangu Witness, lakini Wazo lilibadilika baada ya kumuona kijana mmoja ambaye angefaa kwa ajili ya Kumuoa binti yangu"Alikohoa tena kidogo kisha akaendelea
"Tumekubaliana na wazee wangu na kuona ni bora vijana hao wakakubariana wenyewe mbele ya umati wa watu na kufungishwa ndoa hiyo kwa ridhaa yao wenyewe. Nkizwa iyeee" Mfalme Alimaliza
"Iyee Nkizwayeee" Wanakijiji waliitikia,
Niligeuka kuwaangalia wazee wengine walikua na furaha ila wengine nilihisi hawakupenda kitu icho, kuna wengine walikua na vijana wakiume tena wanaojua kupambana kabisa na walitamani nafasi hii, mimi ni nani nichaguliwe ambaye hata upanga sijui kuushika Kiukweli kuna kitu Baba alikifanya haikua bure. Upande mwingine nilikua na hofu sana ni kwajinsi gani ningesimama mbele ya umati ule ili kukubaliana na Binti Mfalme, mbele ya Mfalme na mbele ya Baraza juu.
Baada ya Mfalme kuongea hayo alirudi kuketi katika kiti chake, Alisimama mzee mwingine ambaye kijijini hapo alitambulika kama mzee Kizindwa, nae aliongea baadhi ya mambo machache na wananchi wa Nkizwa, Kisha akageuka kuangalia pale nilipokua nimekaa pia akageuka kuangalia alipokua amekaa Binti Mfalme.
Aliendelea kuongea mambo machache kisha akaturuhusu tusimamae na kuridhiana sisi wenyewe mbele ya wanakijiji wa Nkizwa.
Witness alisimama huku akisaidiwa na vijakazi, akaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu mpaka pale kwa wazee, aliinama kama ishara ya heshima na kupokea Baraka, Medrick akanikonyeza mimi pia kufanya vile, sikua mbishi nikatoa heshima na kuchukua baraka.
Wote tukaenda kusimama mbele ya umati ule wa watu. Naweza kusema katika siku zote nilizokua nikivaa mavazi ya Nkizwa siku ile ni siku pekee niliyopendeza hata baadhi ya atu hawakuweza kunitambua kwa urahisi,
Witness aligeuka na kuniangalia, hapo niliona akikodoa macho yake kama hakutegemea kuniona mimi mahari pale, Niliamua kutabasamu maana macho yake makubwa yalikua yakinitoa ujasiri.
Niliona watu wengi wakishangaa ni kama hawakutegemea kuniona mahari pale, Bella alizidi kuzoofika, Niliona ni kama alitamani kukaa chini ila hakuweza, macho yake yalikosa ujasiri wakuniangalia akaanza kuangalia Chini,
Alikuja mzee mmoja akaanza kutumwagia unga flani ivi siwezi kuukumbuka kama ulikua ni Unga wa aina gani ila ulikua na rangi ya kahawia na harufu nzurii, Alichukua kitu kama tawi akaanza kuongea maneno yake, aliongea kwa mda Flani Kisha akayainua Macho yake kwetu, Sijui Aliona nini ila ni kama yalibadilika furani ivi. Kisha akamgeukia Mfalme na Kutabasamu huku akitingisha Kichwa, Mfalme alikuja mahari pale na kutuwekea mikono kichwani akainama kwa mda Flani alipomaliza akaenda kuketi,
"Nkizwayee" alirudi kuongea mzee kizindwa, huku akiwa na bakuri la Maji.
"Iyee Nkizwayeee Nkizwa iyee" Wanakijiji waliitikia. Alichukua bakuri la maji na kulipeleka kwa Witness,
Witness aligeuka kuniangalia, akamuangalia mdogo wake Medrick na Mfalme Baba ake, aliwaangali Wazee wa baraza pamoja na wanakijiji kisha akarudisha macho yake kwangu huku akitabasamu akayanawa maji yale. Niliona wanakijiji wakishangilia huku Wazee wa baraza wakisimama kwa heshima kubwa,
"Nkizwa yee" aliongea mzee mmoja huku akinyoosha mikono yake juu kama wanaushindi wa kitu,
"Iyeee nkizwa yeee" Wanakijiji waliitikia kwa furaha
Mzee Kizindwa alikuja mahari pale nilipokua nimesimama na bakuri lake la maji, Mpaka mda huo bado Witness alikua akiniangalia kwa tabasamu, Niliyageuza macho yangu na kumuangalia Baba aliyekua amekaa na wanabaraza nae aliniangalia kisha akanikonyeza niweze kuyanawa maji yale, Nikageukia upande wa wanakijiji nilimuangalia Bella hadi mda huo bado macho yake yalikua chini, hakutaka kutazama Tena mbele, Niligeuka nikamuona Mama yangu akiwa amesimama na mdogo wangu pamoja na Dada yangu ambae alikwisha olewa, niliyarudisha macho yangu kwa Bella Kwa mda huo na yeye nilikuta ananiangalia.
Nilimuangalia mzee Kizindwa aliyekua amekamata beseni lake la maji nikatingisha kichwa ishara ya Kukataa Kunawa yale maji, Yule mzee ni kama hakua ameelewa akalisogeza beseni lake kwenye mikono yangu mimi nikarudisha nyuma mikono yangu. Sikutaka kunawa maji yale, Niliona Mfalme akisimama kwa hasira pamoja na wazee wa baraza, Wanakijiji walibaki wakinitolea macho huku minon'gono ya chini ikianza. Nilipogeuka kumuangalia Mama ikumuona pamoja na ndugu zangu, hata Nilipogeuka kumuangalia Bella sikumuona pamoja na Rafiki zake,
Witness aliniangalia kwa mda mrefu ni kama hakuamini kilichokua Kimetokea, Niliona akilegea taratibu na kuanza kwenda chini. Shadrassa kijakazi wake mkubwa ambaye amemfanya kama Rafiki alikua mtu wa wanza kumdaka Witness ili asitue chini kama Mzigo, Niliona Medrick akitoka mahari pale nakuondoka zake.
Mzee Kizindwa aliyarudisha maji yale kwa mala ya tatu ili niyanawe, Nilimuangalia yeye pamoja na Beseni lake alilokua amelibeba mkononi,
"Kwanini unanilazimisha Kunawa mzee, Mimi siko tayari kunawa" nilimnon'goneza Mzee kizindwa, taratibu akaanza kuondoka na Beseni lake
Itaendelea
Kesho Saa 12:00 Jioni
Comments
Post a Comment