WITNESS - SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

SIMULIZI: WITNESS

 

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

"Ooh kumbe unaijua thamani ya mke si ndio, kwanini hukumheshimu Bella wangu wakati ulijua ni mke wangu mtarajiwa"

TunaendeleA…

 

"Sio ivyo kuna kitu umesahau Clement ikiwezekana naweza kuoa wote wawili mdogo wako akawa mke mdogo na mpenzi wako akawa mke mkubwa" Medrick aliongea huku akimsukuma Julieth kifuani kwangu,

Nilitaka kwenda angalau nimpige hata makofi mawili tu ili moyo wangu urizike lakini Julieth alinizuia kwa kunishika mkono,

"Niache niache niache nikamuonyeshe mshenzi yule, kumbe anadharau kiasi hiki halafu anaonekana mpole tena sio muongeaji mbele za watu kumbe shetani tu yule"

"Muache aende kaka, Medrick anamipango yake kichwani elewa ivyo. Pia yule ukimletea shari anaweza kukuua haoni shida kuua"

Nilimuangalia Julieth aliyekua anaongea kwa upole na huruma tofauti na nilivyomzoea, nilimshika mkono na kumpeleka pembeni kidogo na walinzi,

"Unampango gani kuhusu yeye" nilimuuliza

"Hakuna ninachofikiria kwa Sasa"

"Kwanini hakuna Julieth, hivi hujionei huruma wewe eeh? Kila kitu kinakukuta wewe tu kwanini husemi chochote"

"Clement embu acha kila kitu kitokee, kila kitu na kikamilike sasa kwanini unazuia. Acha kila kitu kiishe Clement"

"Kirahisi ivyo Julieth"

Julieth hakunijibu kitu aliangalia Chini tu, "Sema Chochote basi"

"Clement hivi najua Baba alimsaliti mfalme kwa kumuoa mama ambaye alikua ni mke mtarajiwa wa mfalme, lakini mfalme hakufanya kitu bali alimtafuta mke mwingine nakumuoa na bado hakuvunja urafiki na Baba, Pia Baba alimdanganya Mfalme kuhusu wewe na Witness na mwisho ukamuaibisha Mfalme na Binti yake mbele ya wanakijiji, Wewe ulisaliti ufalme kwa kuuangana na msaliti Winni binti yake Mfalme, Ili kukusaidia wewe mikononi mwa Medrick basi Winni aliwaua askari wa Medrick na kumpiga mshale Medrick"

"Umejuaje yote hayo Julieth"

"Nimeambiwa na Medrick"

"Kwaiyo kwa uongo huo Medrick ameweza kuiteka akili yako ukamkubari kirahisi ivyo? "

"Kaka embu tambua kua Medrick anamengi sana tofauti na hayo. Ivi kama aliweza kumuua Baba ake kwa mikono yake unadhani atashindwa kukua wewe au mimi, Embu acha yote yapite Clement, muache Medrick afanye anachotaka kwasababu ameamua kufanya ivyo"

"Kwasababu ameamua et, Julieth nambie wewe unampango gani na Medrick je unampenda yule mtu?"

Julieth hakunijibu kitu badala yake alianza kulia na kukimbilia Chumbani kwake akajifungia mlango, Nilibaki nimesimama pale kama sanamu, Sikuelewa hata nifanye nini. Nilijua mdogo wangu anampenda Medrick, lakini Medrick tayari anamipango yake yule mtu hata sijui anahitaji nini Kwenye familia yetu.

"Umetambua kua mdogo wako anampenda Medrick et, sasa unaamua nini cha kufanya?  Kumbuka hata mimi simpendi huyo Julieth katika Jumba hili ila nampenda Bella, yule ndio anafaa kua mke wa Medrick kwanza tayari anaujauzito wake"

Alikua ni Witness sijui alifika mda gani pale na kwa jinsi nilivyokua nikimchukia hata sikutamani awe mbele yangu….

 

Itaendelea

Kesho Saa 12 Jioni

Comments

Popular Posts