WITNESS - SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
"Wamefunga ndoa lakini hawajafanya chochote, hata ivyo Mfalme anabahati sana yule ilibidi nimuue kabisa. Mimi namwambia nimempenda binti yeye anaenda kumuoa kabisa si aibu hiyo, Nimesema nitamuoa yule Binti"
"Kwaiyo Medrick wewe ndiye ulimshambulia Mfalme? " Witness alimuuliza.
Medrick alitabasam….
Tunaendelea….
Medrick alitabasam tu nakuamua kuondoka bila kujibu Chochote. Nilisimama pale nilipokua nimekaa nakumfuata Binti Mfalme,
"Hii ni ajabu Witness, yani unajikuta unapambana mwenyewe bila kusaidiwa na mtu. Nashukuru kwasababu undugu unazidi kuongezeka. Nipo huru sasa acha nikatembee tembee huko nje nitakuja kukujulia hali badae"
Nilitaka kuondoka lakini Witness alinisukumia chumbani kwake kwa ghadhabu, Alianza kupiga kelele ndani kama amechanganyikiwa, Nilikaa tu kitandani kwake nakuanza kumuangalia alivyokua anapangua vitu. Hadi mda huo sikuwai kuonana na Winni wala wazazi wangu, Kauli ya Medrick kusema anahitaji kumuoa Julieth ilizidi kunizunguka kichwani nilijua ni jinsi gani Julieth atakua na furaha kupata hizi habari kwasababu alikua akimpenda Medrick.
****
Siku iliyofuata Witness alianza kujianda kama anaenda kwenye mapambano, alimtuma mmoja wa Askari wake nakumuambia akaliandae Jeshi lake la watu wachache tu. Alipomaliza kujianda alinifuata kule chumbani nilikokua nimejilaza
"Usijisahau sana ukajiachia upo sehemu za watu na wanaweza kukuamulia chochote, Jiandae tuondoke" Aliongea Witness
"Unaenda wapi, au unataka kwenda wapi"
"Kumbuka wewe ni kama mtumwa tena sio kama Ila wewe ni mtumwa kwaiyo popote nitakapo kwambia wewe twende tu"
"Sikia Witness unajua wewe ni Binti mfalme ila dharau zako ndizo zinazokushusha thamani halafu sikujua hili tangu mwanzo nilikuona kama binti mstaarabu ivi nashukuru Miungu ya Nkizwa nilikukataa mapema maana ndoa ingekua ni ya migogoro sana". Namimi sijui nilianza kupata wapi jeuri ya kumjibu binti Mfalme.
Witness alianza kucheka kama kawaida yake, alikua akianza kukucheka utatamani hata umzabe makofi ya uhakika ili jeuri imtoke
" Kila mala nakwambia Clement ivi nani alikudanganya kua mimi nilikupenda? Mimi nilishakuona ukishirikiana na waasi tena usijifanye mtakatifu hapa, Mimi nilikukubari kwa lengo moja tu ili uone ni jinsi gani mwisho wako ungeharibika, tena shukuru sana miungu ulinikataa"
"Ooh basi vizuri mtoto mzuri, Sasa sikia atakae kuja kukuoa wewe atakua amepata hasara sana tena sana yani natamani kila mtu ayajue matendo yako ili wanaume wote wa Nkinzwa wakukatae yani sura yako na dharau zako nitofauti kabisa"
"Wewe ndio wasema lakini hayo hayapo kwa watu ila yapo kwako, ni afadhari mimi na mambo yangu ila sio yanayokuja kutokea kwenye maisha yako Utalia kama mtoto mdogo Clement, haya twende huko unanichelewesha" Sikuelewa Witness alimaanisha nini, tulianza kutoka nje ya Jumba la kifalme.
Tukiwa tunakaribia kutoka nje ya Jumba la Kifalme nilimuona Bella akija kwangu huku akilia, alinifikia nakunilukia, alibaki amenikumbatia kwa mda mrefu hadi Witness akaigiza kukohoa ndio akaniachia,
"Kunashida gani mamaangu mbona ivyo" nilimuuliza Bella huku nikimfuta machozi, Bella hakunijibu kitu alibaki tu akilia
"Si Umeshatibiwa mguu wako haya rudi nyumbani". Bella alitikisa kichwa ishara ya kwamba hawezi kuondoka
"Kwanini Bella" nilimuuliza,
"Khee si ameshakuambia hawezi kutoka, utajua baadae kwanini anakataa, Unajifanya kama unajua kujali wakati huna lolote, Alafu usinicheleweshe tuondoke" Witness aliongea kwa kufoka kama nilimuuliza yeye.
Kwanza aliniaibisha hawezi kunijibu mimi vile mbele ya mtoto wa kike tena mpenzi wangu kabisa, Nilimuachia Bella pale alipo na kumfuata Witness,
"Sikia Witness usizani nakuogopa et kisa ni mtoto wa mfalme halafu kwa mazingira tuliyokutana mimi na wewe usizani kama nakuchukulia kama Binti Mfalme, Ninauwezo wa kukufanyia chochote na huo ubinti Mfalme wako"
"Clement acha bhana, kila kitu kiache kiende na uende salama huko muendako" Bella ndiye aliyekuja kunikatisha pia akampa Witness heshima yake kama Binti Mfalme. Witness hakuipokea ile heshima aligeuka kwa hasira nakuanza kuondoka huku walinzi wengine wakimfuata nyuma,
"Nitakuja badae kukuona Bella, ubaki salama" Nilimuaga Bella nakuanza kuondoka, Nilipanda kwenye farasi aliyokua amepanda Binti Mfalme na Walinzi wengine wakapakiana kwa farasi zao, kila Farasi ilibeba watu wawili tulikua zaid ya kumi na sita, Tulianza safari ya kuelekea msituni, nilijua safari ile ni kwenda kwenye kambi ya Winni. Ila kwa jinsi nilivyomfahamu vile Nkajua alipata taharifa kabla hata hatujafika kambini, Baada ya Safari ya mda mrefu tulifika kambini pale lakin tulikuta kambini kumetulia Kama hakuna mtu, Askari wote wa Binti Mfalme walishuka kwenye farasi akiwemo na Binti Mfalme mwenyewe. Walianza kukagua kwenye mahema nakuambulia patupu, ila kulionekana kulikua na watu mda mchache Uliopita.
Witness alianza kupiga piga zile hema huku akiongea kwa hasira na kwa sauti akiwatishia hao waasi wake, alipoona bado kimya alinichukua na kuniweka kati huku akitishia kuniua na kuanza kuita maadui zake,
"Sasa Binti Mfalme mimi nahusikaje na hawa adui zako, Alafu kama unaona hawa ni Adui kwanini usitoe taarifa kwenye jumba la kifalme ili mje mpambane kwa umoja embu acha masihara bhana huo ni mshale ujue utaniua " Nilimuambia Binti Mfalme huku nikiwa na wasiwasi maana mshale aliuelekezea kwangu, Lakini Binti Mfalme ni kama hakua ananisikia ivi, aliendelea kuita adui zake ili wajitokeze mbele kabla hajaniua mimi,
"Witness ivi unajua unapambana na dada yako kwanini msikae chini mkamaliza tofauti zenu" Niliendelea kuongea
"Kelele na Wewe" Witness aliongea kwa hasira huku akiuachia mshale tayari kwa kunipiga, niliyafumba macho yangu huku nikikiona kifo changu karibu kabisa .
Itaendelea
Kesho Saa 12 Jioni
Comments
Post a Comment