WITNESS - SEHEMU YA KUMI NA SABA

SIMULIZI: WITNESS

 

SEHEMU YA KUMI NA SABA

Tulitembea hadi nje ya jumba la mfalme, tuliingia ndani kwa kutimia mlango mwingine wa siri wa kutokea polini, mlango huo Winni ndiye aliyeweza kuufungua. Jumba lile lilikua na milango zaidi ya mitatu pamoja na ya siri, hadi mda huo tayari jua lilikua limechomoza kabisa, mshale wangu aliyokua amenipatia Bella nilikua nimeushika mkononi.

Tunaendealea…

 

"Nitakapokua napambana hakikisha unaingia ndani kabisa mpaka kwenye chumba cha Binti mfalme na umueleze kila kitu kama tulivyokubaliana kuwa uko tayari kumuo”

 "Na vipi kuhusu Bella? "

" Kwasasa usiwaze kuhusu yeye, haya unayoyafanya ni kwa ajiri yake"

Tukiwa hapo tuliskia kengele kutika jumba la Mfalme, ilikua ikiwakusanya wanakijiji wote, Nilijua wazi hiyo kengele ilikua ni kwa ajiri ya kifo cha Babaangu pamoja na kutangazwa kwa Bella mpenzi wangu.

"Fanya kitu Clement" Winni aliongea huku akitaka kubonyeza baadhi ya namba ili kufungua Jumba hilo.

"Nitafanya ivyo"

Winni alikifunua kitambaa chake cha Usoni kisha akanifuata na Kunikumbatia, kwa mala ya Kwanza nilimuona Winni akitabasamu tangu nifahamiane naye.

"Utakalo enda kulifanya ni tukio la kishujaa, najua itakua kazi kubwa wewe kutoka katika mikono ya Mfalme na ikiwa hujawai kupambana na mtu yeyote yule ila naamini utashinda na utapata ushindi mkubwa sana nakutakia safari njema katika kuokoa familia yako" Winni aliongea na kukirudisha Kitambaa usoni kwake,

 

Alibonyeza baadhi ya namba na kuweka kidole chake geti la Mfalme la siri likafunguka, tuliingia pasipo kipingamizi kwani mahari hapo hapakua na walinzi, jinsi tulivyozidi kwenda mbele ndivyo  tulivyoanza kuona walinzi,  Winni alikua na kazi ya kupambana na walinzi hakua na uwoga hata kidogo alionekana ni binti shujaa ila kwa jinsi alivyokua amevalia mapambo yake usingeweza kuamini kama anauwezo wa kupambana namna ile,

Tulifika Eneo la korido inayoenda mojamoja kwenye chumba cha binti Mfalme, “hapa unaweza kwenda maana hapa hakuna walinzi”.  Winni aliongea huku akikagua usalama wa eneo lile,

"Lakini sizani kama kutakua na Binti mfalme mle ndani" Wasiwasi Ulianza kuniingia tena,

"Hata kama hayupo atakua ameenda kwenye mkutano wa wanakijiji hapo nje, Fanya uingie mapema kabla hujashtukiwa" Winni alianza kuondoka

Nilitembea haraka mpaka kwenye chumba cha Witness, nilimkuta amesimama na Shadrassa kijakazi wake ni kama walitaka kutoka nje, baada tu ya kunioa Witness alikunja uso wake na kutaka kupiga kelele, Haraka haraka nilimfuata na kwenda kumziba mdomo, "Taratibu Witness utajaza walinzi, sijaja kwa ubaya mimi wala sijaja kwa fujo ila tafadhari tulia nakuomba tulia"

Shadrassa alipoona hivo akaanza kutoka nje kwa mwendo wa haraka Ikabidi nimuachie Witness ili nikamzue Shadrassa, niliushika mkono wake kwa nguvu na kumvutia kifuani kwangu kisha nikaibana milango kwa hasira, Wakati huu nilikua makini sikutaka kuleta Mchezo hata kidogo,

"Niache nasema niache" Shadrassa alianza kupiga kelele tena,

Nae witness akaenda kuchukua upanga ili kuja kupambana na mimi, Nilienda kumzuia japo alinishinda nguvu kwa kiasi kikubwa nilifanya kazi kubwa hadi kumtuliza binti Mfalme na akatulia, Ikabidi niwaketishe wote kitandani japo Binti Mfalme alikua hajatoa upanga mkononi.

"Binti Mfalme Witness naomba unisamehe, nisamehe kwa yote yaliyokua yametokea hapo nyuma. Nimerudi ili kukuomba radhi na kukuomba ukasitishe zoezi la Mfalme kumuua babaangu Sijui nilikua nafikilia nini hadi nikakutaa siku ile mbele ya umati wa watu ila nakuahidi nipo tayari hata leo hii kufunga Nndoa na wewe na naahidi nitafanya chochote utakacho", Niliongea huku nikiwa nimepiga magoti, Witness aliniangalia sana baada ya hapo alianza kucheka,  alicheka mpaka nikaanza kuona aibu mwenyewe, Ujasiri ukaanza kuniisha nilitamani nisimame niondoke ila nikajipa moyo tu nisubiri amalize kucheka

"Kwaiyo umekuja kwaajiri ya kumuokoa Baba ako si ndiyo, Vipi na Familia yako?  Mfalme anataka kumuoa mdogo wako utaweza kulipinga hili?  Au Baba apone mdogo aende?  Na nani kasema Unapendwa wewe? “. Witness alianza tena kucheka, nilitamani niseme kitu lakini nilishindwa.

"Sasa sikia mimi sikukukubali eti kisa nakupenda hapana ila nilikukubali ili ukanisaidie kupambana na waasi wenzio, wewe si kundi moja na waasi kule polini na kuna siku ulinishambulia unakumbuka?  mlitaka mumuue mdogo wangu Medrick si ndiyo, hao waasi wako si ndio waliokutorosha siku ya adhabu na sasa hivi wametuma tena eeh? "

"Witiness, Witnes jamani dah! Unaongea maneno hayo yote sikweli naomba umuokoe Babaangu Witness" Niliona Witness anaongea sana.

Kabla Witness hajaongea kitu mlango wa Chumba cha Witness uligongwa….

 

Itaendelea

Kesho Saa 12:00 Jioni

Comments

Popular Posts