WITNESS - SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
"Umetambua kua mdogo wako anampenda Medrick et, sasa unaamua nini cha kufanya? Kumbuka hata mimi simpendi huyo Julieth katika Jumba hili ila nampenda Bella, yule ndio anafaa kua mke wa Medrick kwanza tayari anaujauzito wake"
Alikua ni Witness sijui alifika mda gani pale na kwa jinsi nilivyokua nikimchukia hata sikutamani awe mbele yangu.
TunaendeleA…
"Unaweza kuniacha mwenyewe Witness, Sihitaji mazoea na wewe"
"Itakua vizuri kama huitaji mazoea na mimi, hata mimi nakuchukia sana zaidi ya unavyofikili natamani hata kesho ungetoka katika macho yangu"
"Naona unaongea upuuzi tu hapa huna lolote" Niliamua kuondoka zangu, nilimuacha Witness akiwa anatabasamu.
Nilifika Nyumbani na tayari usiku ulikua umeshachukua nafasi yake, Nilitamani kwenda kumtembelea Bellath wangu toka akamatwe na Chande hatukuwai kuonana hata siku moja hadi leoiIla nikaona bora ningesubiri kupambazuke tu.
****
Asubuhi kama kawaida baada yakufanya shughuri chache za nyumbani maana tulisalia mimi na mama yangu basi hapo nyumbani, niliamua kutoka ili kwenda kumuangalia Bella kama jinsi nilivyokua nimepanga toka Jana Usiku, Safari haikua ndefu hadi kufika anapoishi Bella. Nilifika nakumkuta Dada ake Bella amekaa nje, alionekana ni mtu wa mawazo sana, hakuhisi chochote kama kuna mtu anakuja maeneo hayo.
Nilifika nikamshika mabega yake, aliruka juu kwa hofu kubwa, mshtuko na wasiwasi ndani yake.
"Clement ni wewe, umebadilika ivi nimiezi mingapi hatujaonana pia nashukuru umekuja mda muafaka" Aliingea dada yake Bella baada ya salamu,
"Nambie Shemeji yangu, kwanza Bella nimemkuta maana nimemkumbuka ni muda sana hatujaonana" Dada yake Bella alikaa kimya kidogo kama anafikiria kitu
"Ndio maana nimesema ni kheri umekuja muda muafaka, Unajua asubuhi hata kabla hatujaamka walinzi wa Medrick wamekuja kutugongea mlango na wamemchukua Bella kwa Lazima hatukua na chakufanya mbele ya mwana mfalme"
"Kwaiyo Shemeji usitake kuniambia mmemuacha Bella aende kwa Medrick? Kwanini lakini"
"Walikuja kwa kisingizio kuwa kama atabaki hapa mimba haitakua vyema, Si unajua wanasema ile mimba ni ya M……"
"Najua shemeji najua kila kitu, kwanini singekuja kuniambia mda ule ule kwanini eti Shemeji"
"Clement ilikua ni ngumu"
"Dah haya asubuhi njema"
Niliondoka kwa Hasira sana safari yangu ilikua ni kwa mwanamfalme, nilikumbuka aliwai niambia kama anauwezo wa kuoa wote wawili, Mdogo wangu pamoja na Bella, na yule hua hatanii, Bado nilikua nampenda Bella licha ya kuambiwa anamimba ya Medrick.
Kama ni Mtoto atazaliwa tu na atakabiziwa kwa Baba yake ila Bella bado yupo katika maisha yangu, sizani kama mimba ikawa chanzo cha kuvunja uhusiano na upendo wetu, Bella ni wangu na atakua wangu daima.
Itaendelea
Kesho Saa 12 Jioni
Comments
Post a Comment