WITNESS - SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
SEHEMU
YA ISHIRINI NA TISA
"Sijari kuhusu hilo"
Bella alinishka mkono, tukaanza kukimbia.
Lakini hatukufika mbali, tulisikia
sauti ya mshale na punde si punde Bella alianza kulegea na kwenda chini,
Niliangalia nyuma, Witness alikua ameshika
Mishale anakuja eneo lile tulilopo mimi na Bella.
Tunaendelea…
"Witness " niliita kwa wasiwasi,
"Nilijua tu kama hili jambo
litatoke, Mtu anaona anamimba ya mwanamfalme, kwanini asitulie ehee mnatorokea
wapi" Aliongea Witness
"Unajua ulichokifanya lakini
Witness" niliuliza
"Ndiyo najua, tena najua sana
tu. Nimempiga mtu mshale, simlitaka
kukimbia haya kimbieni"
Niliangalia chini, Bella alikua
tayari ametua sakafuni na macho yake aliyafumba
"Bella, Bella" niliita
huku nikimtikisa,
Askari walikuja haraka ili wambebe
lakini Witness aliwazuia kwa shara ya mkono, nao hawa kuwa na kipingamizi kwa
Binti Mfalme.
"Witness ivi unadhani itakuaje
kama umeua" niliongea kwa hasira,
"Kawaida tu lakini
sikukusudia" alijibu huku akitaka kuondoka.
"Hukukusudia kivipi Witness,
Unamaana gani kusema hukukusudia? "
"Si mlitaka kutoroka, nilikua
naokoa maisha ya mtoto aliyetumboni asinuse harufu ya nje ya hili jengo"
Witness aliongea huku akiibenua midogo yake akaondoka.
Nilimuangalia Bellath aliyekua
amelala sakafuni japo alikua akitoa pumzi, niliwaza ni jinsi gani nitamuokoa
Binti yule na mshale uliopo katika mwili wake.
Wazo pekee lililonijia ni kuondoka
nae mahari pale na kumpeleka nyumbani, Sikujari kama Medrick atanielewaje ila
mawazo yangu yalikua ni kuhakikisha Bella anakua salama.
Nilimbeba Bella nakuanza kutoka nae
nje, mda wote nilikua nikimuangalia Bella wangu kama atakua mzima au laah,
alikua akipata maumivu sana hata pumzi yake ilitoka kwa shida
Nilifika nje ya kumbi ya Mfalme,
kitu ambacho sikufikilia awali, kulikua na askari wengi na wazee wa Baraza pia kulikua na mbishano mkubwa wa pande
mbili, Baada ya mimi kutoka watu wote walinigeukia mimi,
"Beellaaa " Medrick
alikuja na kutaka kunizaba kibao lakini nilifanikiwa kukwepa,
"Umemfanya nini huyu, unataka
kumuua Bella Clement" Medrick aliongea kwa hasira huku akimchukua ella,
lakini nafasi haikua kwake kwasababu Bella alikua ameishikilia nguo yangu kwa
nguvu sana. Kila mtu alibaki ananiangalia mimi pamoja na Medrick.
"Askari iteni tabibu
haraka" Medrick aliongea,
Lakini kabla Askari hawajafanya
ivyo, Ulikuja mshale mwingine ukamchoma Bella katika ubavu wake.
Niliita kwa sauti ya uchungu baada
ya kuona damu iliyokua ikimwagika pale chini ni ya Bella.
Hakuna aliyeamini tukio lile, Hata wazee
pia walisimama ili kushuhudia tukio lile.
Bella aliyafumbua macho yake japo
kwa shida
"Clement naumia, ninamaumivu
sana. Nakufa, lakini Nakupenda Clem--"
Bella aliyatamka haya huku akiwa
mikononi mwa Medrick na Mkono wake mmoja ukiwa katika nguo yangu, Taratibu
alianza kulegea kabla hajamaliza kauli yake, na mwisho aliacha kabisa kutoa
pumzi. alikua ametuacha Bella wangu,
Medrick aliangalia sehemu ambako
mshale ulikua umetokea, Alikua ni WITNESS, Witness ndiye aliyemuua Bella,
Itaendelea
Kesho Saa 12 Jioni
Comments
Post a Comment