WITNESS - SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

SIMULIZI: WITNESS

 

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

"Witness ivi unajua unapambana na dada yako kwanini msikae chini mkamaliza tofauti zenu" Niliendelea kuongea

"Kelele na Wewe" Witness aliongea kwa hasira huku akiuachia mshale tayari kwa kunipiga, niliyafumba macho yangu huku nikikiona kifo changu karibu kabisa.

Tunaendelea…

 

Baadae niliyafumbua macho nakujiangalia, baada ya kujiona ni mzma wa afya kabisa nikaangalia sehemu iliyoangukia mshale.  Mshale ule ulikua umeanguka chini baada ya kuzuiwa na mshale mwingine uliotokea upande mwingine. Walinzi walikaa tayari kwa mapambano baada ya kujua adui zao wapo karibu, Nilipoona ivyo nilianza kucheka, nilicheka mpaka Witness akachukia

"Sasa nyie mda wote mpo hapa hata mishale mlikua hamjaandaa Ila mlivyoona adui zenu wapo jirani ndio mnajiandaa si mngekua mshakufa nyie" Niliendelea kucheka tena kwa dhihaki maana nilijua Winni yupo maeneo yale hakuna ambalo lingetokea.

Baada ya muda Winni alikuja tena alikuja peke ake bila mlinzi yeyote, "Umerudi tena Witness basi vizuri"

Witness aliushusha mshale wake lakini Winni aliukwepa huku akizidi kusogea pale alipo,

 "Huwezi kufanya ivyo kumbuka mimi ndiye niliyekufundisha kupigana, Alafu pole Kwasababu mpaka sasa sijui unapigania nini kwangu "

"Hujui napigania nini Eeh? Basi vizuri utajua tu" alijibu Witness,

"Ooh sawa nieleweshe"

"Kama hujui kwanini ulitoroka ndani ya Jumba la kifalme. Nakwanini unaiba askari wa Jumba la Kifalme na kuwaleta huku"

"Mimi siibi askari wa Jumba la Kifalme ila nilichukua askari wangu kama wewe ulivyoambatana na askari wako, pia hawa wengine wanapenda kuambatana nami kwasababu wamechoka maisha ya Baba yako, ivi ni nani atakae kubali kuacha raha ya Jumba la Kifalme na kuja kuishi porini? "

"Unamaanisha nini? "

"Ni vizuri kama hujaelewa, Ila ni bora kuishi sehemu ndogo yenye amani kuliko sehemu kubwa yenye Utumwa "

Witness alianza kumcheka dada yake kama kawaida yake na kicheko chake cha dharau

"Usijidanganye kwa ivyo Winni kila siku unakua ni mtu wa kunishawishii ila jua mimi sishawishiki wewe si ulimuua mama yangu kwa mikono yako basi na mimi nitakuua wewe kwa mikono yangu mwenyewe"

"Kwanini unakua mgumu Kuelewa Witness"

"Nimeishakuambia huwezi ukanitungia shairi lako na mimi nikalielewa na kuliimba mbele ya watu hata  siku moja siwezi"

 

"Ooh basi sawa kabla hujapambana nami rudi nyumbani ukauzike mwili wa mfalme ili uje upambane na mimi kwa vifo vya watu wawili mama pamoja na baba" Winni aliongea huku akiangalia anga

"Nenda salama Mfalme, nenda ukamuombe mama msamaha, pia umeondoka na maisha ya watu wengi Mfalme.  Wengi umewaua bila kosa, Umeacha yatima wengi kijijini, Umeharibu maisha ya watu hata maisha yangu pia, hakika kifo chako ni Shangwe kwa wanakijiji wa Nkinzwa hasa kwa mwanao Winni" Winni aliongea kwa furaha na kuanza kucheka kwa dharau kisha akatoka kwa kasi ya ajabu kama upepo,

"Winni" Witness aliongea kwa hasira huku akipiga mshale kuelekea upande alioenda Winni, na kuamuru askari wote washambulie eneo lile, lakini hakuna walichokua wameambulia.

 Witness alipanda farasi wake kwa hasira nakuanza kuondoka na walinzi wakamfata ivyoivyo na kuniacha mimi pale.

"Mmhh sasa huyu na hasira zake ndio ameamua kuniacha mimi hapa" niliongea huku nikiangaza macho yangu huku na huko nakuanza kuondoka"

 

Nilifika kijijini lakini ni kama hapakua na mtu yeyote, sehem zote zilikua kimya, nilienda hadi nyumbani nilimkuta Baba peke yake bila Mama,

"Baba" niliita huku nikumshika paji lake la uso maana alikua amelala huku akitoa Jasho jingi pia alikua amekonda sana.

"Clement mwanangu" Baba aliita kwa shida.

"Hii hali imekuanza lini Baba" Sikuwai kuonana na wazazi wangu tangu siku niliyotaka kumuoa binti Mfalme ni zaidi ya miezi saba sasa,

"Umekuja lini kijana wangu" Baba nae aliniuliza

"Ninamwezi na wiki, tangu siku ya hukumu yako ya kunyongwa mimi nilikuepo, Ila nilikua ndani ya Jumba la kifalme sikutakiwa kutoka.

"Ooh nafurahi kusikia ivyo, vipi mdogo wako Julieth anaendeleaje, Sijui atakua katika hali gani mwanangu Ila yote ni makosa yangu mwanangu naomba mnisamehe"

"Sisi tumeshakusamehe baba wala usijari, Kwani unaumwa nini wewe na mbona kama hutumii dawa yeyote"

"Mwanangu dawa ya ugonjwa huu anaeijua ni Mfalme pekee kwani hii ni sumu inayomuua mtu taratibu na mfalme hupenda kuwapulizia viongozi wake pindi wanapokosea" aliongea Baba,

"Kwani wewe ulimkosea nini Mfalme"

"Mwanangu mimi nilimkosea mfalme kwa kumdanganya upo tayari kumuoa binti yake na kukujazia sifa za ushujaa ambazo hata huna Ila naweza sema nilimkosea kwa kumdanganya. Na Mfalme aliapa atalipa kwa kumuoa binti yangu, nilipokua nabisha ndipo aliponipulizia huu unga"

"Sasa mbona Binti yako alishakubari kuolewa kwanini asikupe dawa"

"Ndiyo alikubari ili kuniokoa lakini mpaka ndoa ingefungwa ndio Mfalme angetoa dawa, Ndio ivyo nae alipigwa siku ya ndoa, ni bora Binti yangu asingekubari kuolewa na Mfalme maana alikubari kashinda ili kuniokoa ila sasa huu ushindi unakua na maumivu" Baba aliongea kwa tabu

 

Itaendelea

Kesho Saa 12 Jioni

Comments

Popular Posts