WITNESS - SEHEMU YA KUMI NA SITA

SIMULIZI: WITNESS

 

SEHEMU YA KUMI NA SITA

"Chande ananitafta mimi kwa mabaya? " Niliuliza huku nikikaa vizuri,

" Chande anampenda sana Binti Mfalme na sizani kama anataka kuipoteza hii nafasi na ni mtu anaeaminiwa sana hata na Mfalme kwa sasa, sizani kama anaweza kubari kuipoteza hii nafasi eti kisa rafiki yani rafiki tuu"dah nilihisi kuchoka Clement Mimi.

Tunaendelea…

 

"Kwaiyo utanisaidiaje Bella" nilimgeukia bella

" Ni bora ungetulia kwanza uone ni kipi kitaendelea, na kumbuka sasa ivi kunapambazuka na Baba ako atapewa adhabu yake asubuhi ya Leo, Ni bora umpoteze mmoja kuliko kuwapoteza wote"

" Unamaana gani Bella? " niliuliza kwa mshangao

"Muache Baba apambane kwasababu alikua ni mshauri na ni mtu wakaribu sana kwa mfalme anaweza kupambania uhai wake kwa vyovyote vile ataweza lakini kama ukienda utasababisha mengine pengine vurugu yako mtakufa wote "

 

Maneno ya Bella kidogo yaliniingia ila siyo kwa asilimia zote. "Kwa hiyo nitashinda wapi kwa siku ya leo" nilimuuliza Bella

"Mmh sijajua na mahali hapa sio salama hua wanakuja kukutafta mdaa wowote au ni bora ukarudi kuwasiliana na Yule dada uliekuja nae jana aliniambia atakua pembezoni ya mto Nkizwa”, Nilimkumbatia Bella, kiukweli alikua akinifariji japo hata yeye alionekana kua na uoga palipo na mwanamke mwenye akili pana ushindi mkubwa.

Nilienda kuangalia kamshale kangu nilikokua natembea nako kabla sijapata matatizo lakini sikukakuta sijui walikaweka wapi, Tulitembea na Bella kwa uangalifu mkubwa tukielekea pembezoni mwa mto Nkizwa tukiwa njiani niliskia sauti za Watu. "Watakua kina nani hao" nilimuuliza Bella

" Vijana wa Nkizwa sijui wanashughuri gani huku, tuangalie sehemu tujifiche kwanza" Bella alijibu huku akiangaza sehemu ya kunificha.

"Clement, Clement yule kule" niliskia sauti ya Chande akiwaonesha wenzie,

"Bella rudi, kimbia acha nikamatwe kimbia" Nilimwambia Bella aliekua akinivuta mkono ili tujifiche.

"Clement watakuua Chande sio mwema kwako hata kidogo " Bella aliongea huku akinivuta.

 

Kabla hajapiga hatua ulipigwa mshale kwenye mguu wake,Niliangalia aliekua amempiga mshale ule alikua ni Chande akiwa pamoja na walinzi wa mfalme walikua wanakuja kasi pale tulipo.

"Chande, Chande rafiki angu"

"Kimbia Clement, huwezi kupona hapa nenda kwa yule dada naamini mtakuja kutusaidia, Nenda Clement " Bella aliongea kwa shida huku akilia, aliuchomoa ule mshale kwa maumivu na kunipatia,"Kama wakikufuata huu unaweza kukusaidia" Sijui Bella alikua ni mwanamke wa aina gani ila naweza kusema Bella wangu alikua ni jasiri sana. Nilitoka pale huku nikiumia Kumuacha Bella maeneo yale lakini ningefanyaje sasa, Nilijitaidi kuwakwepa walinzi na hatimae nikafanikiwa.

Kukutana na Winni nilimkuta akiwa amesimama ndani ya mto Nkizwa huku akiwa amefumba macho yake,na asubuhi ile na ubaridi wa maji lakini alionekana kutotetemeka, aliyafumbua macho yake na kuniangalia.

"Nilikwambia usirudi Nkizwa mda bado ukaona nadanganya si ndiyo" Winni aliongea huku akitoka kwenye maji na kunifuata.

"Umejitaftia matatizo pia umemuingiza binti wa watu katika matatizo ni kheri tusingekuja. Nilikwambia wewe ni mkubwa kuliko mimi lakini mimi ninauwezo na maarifa kuliko wewe Clement "

Nilibaki nikimuangalia alikua ameloa sana na maji, alichukua mshale uliokua mkononi kwangu, ulikua na damu ya Bella pamoja na nyama nyama ambazo zilitoka bella alipokua anauchomoa mshale ule.

"Ukicheza kidogo tu Binti yule atakufa, inabidi unisikilize mimi kwa Kila kitu" Mda wote nilikua namuangalia tu Winni ni kama nilikua nimechanganyikiwa ivi.

"Nitakusaidia kukurudisha katika jumba la mfalme, Uende moja kwa moja katika chumba cha Witness na umwambie akisamehe kwa yote na upo tayari kumuoa "

"Nitawezaje kufanya ivyo " Nilimuuliza kwa kustaajabu

"Kwani wengine wanawezaje? "

Aliuchukua ule mshale nakuanza kutoa vile vinyama nyama vilivyokua kwenye mshale ule na kuacha damu tu

"Lamba damu hiyo" aliongea huku akifungua kibegi chake anachohifadhia mishale na dhana nyingine.

"Eti? " niliona ni ajabu yani mi nilambe damu ya mtu, nilikua nikiskia tu kwa watu kua kuna baadhi ya watu wanakunywa damu ila mimi hata kulamba siwezi.

"Kama Bella ameweza kuukana uhai wake kwa ajili yako kwanini wewe usiikane hofu yako kwaajili yake" Winni aliongea huku akinikazia macho.

"Unamaanisha nini" Nilimuuliza

"Hiki kitakua ni kiapo chako kwa Bella, utamuokoa na utamuoa siku zijazo"

Niliilamba ile damu kwa kinyaa sana baada ya kumaliza nilitamani hata kutapika lakini ningewezaje mbele ya mwanamke shupavu na jasiri Winni.

"Kama uliyaona yote kwanini hukutoa msaada kwetu " Nilimuuliza Winni.

"Ulihitaji msaada gani ikiwa msaada umetolewa na Bella"

Winni alitoa kinguo chake chepesi kilichokua kimelowa na maji, akavaa nguo zingine mbele yangu wala hakua na aibu hata kidogo, alivaa vizuri pia aliweza kupangilia mapambo yake kama anajitazama kwenye kioo, Alipohakikisha yupo kama Binti mfalme akafunika uso wake na kuacha macho tu yaonekane. Tulitembea hadi nje ya jumba la mfalme, tuliingia ndani kwa kutimia mlango mwingine wa siri wa kutokea polini, mlango huo Winni ndiye aliyeweza kuufungua. Jumba lile lilikua na milango zaidi ya mitatu pamoja na ya siri, hadi mda huo tayari jua lilikua limechomoza kabisa, mshale wangu aliyokua amenipatia Bella nilikua nimeushika mkononi.

 

Itaendelea

Kesho Saa 12:00 Jioni

Comments

Popular Posts