WITNESS - SEHEMU YA KUMI NA NANE

SIMULIZI: WITNESS

 

SEHEMU YA KUMI NA NANE

"Witiness, Witnes jamani dah! Unaongea maneno hayo yote sikweli naomba umuokoe Babaangu Witness" Niliona Witness anaongea sana.

Kabla Witness hajaongea kitu mlango wa Chumba cha Witness uligongwa

Tunaendelea…

 

 Shadrassa alisimama na kwenda kufungua "Unahitajika katika mkutano wa wanakijiji Binti mfalme" Shadrassa aliongea baada ya kuonana na huyo aliekua akigonga, "Mwambie sawa nakuja"

Shadrassa aliufunga mlango na kurudi pale tulipokua tumekaa.

"Nakuomba Witness" nilizidi kumsisitiza, "Bora hata umekuja baada la hili kuisha subiri adhabu yako " Binti mfalme alimaliza kuongea nakuondoka zake.

Mmh nilianza kumfuatilia Witness kwa nyuma, hakugundua na dneo la chumba chake hakukua na mlinzi hata mmoja, Alipokatisha  kwenda sehemu ya ukumbi ili kuona wanakijiji walio nje mimi nilibaki nyuma ya pazia maana eneo la huko kulikua na askari wengi, nikiwa pale nilimuona mwanamke mdogo alikua kavalishwa vizuri  Ila alijifunika kitambaa usoni,  alipozidi kuja mbele yangu nilihisi namtambua mwanamke huyo, 

Yalabii Alikua ni mdogo wangu Julieth, alionekana kukonda sana, Nilimpungia mkono bahati nzurii aliuona mkono ule. Aliwapa ishara walinzi kua wamwache kidogo na wakakubari bila kuniona, Julieth alinifuata hadi pale nilipokua Nimesimama akanishika mkono na kuniweka kando kidogo ili asionwe na mtu.

"Kaka ni wewe" Julieth aliongea na tayari machozi yalikua yameanza kumtiririka,

"Ni mimi Julieth vipi mama yupo wapi"

“Mama amefungiwa chumba cha adhabu ila hapewi adhabu yeyote, Bella amekuja ametusimulia kila kitu ila yupo katika wakati mguu pia mguu wake haujapakwa dawa mpaka sasa”.

"Sasa wewe huku unaenda wapi, umeshakubari kua mke wa Mfalme mdogo wangu, Yule si ni kama Baba tu ni kama baba yako yule"

"Nataka nikakubari kua mke wa mfalme ili kila kitu kiishe, Kila kitu kipite tuanze upya" Julieth alionekana ni jinsi gani alivyokua na maumivu moyoni mwake ila ni kama alijitoa sadaka kwa familia.

 

Nilimvuta na kumkumbatia Julieth, Nilianza kukumbuka Winni alivyokua amenisimulia kua ama ake (Malkia) aliuwawa na mfalme kwasababu alikua akisimamia haki, Kama aliweza klumuua mke wake wa kwanza na aliemzalia watoto wote atashindwa kumuua mdogo wangu aliempenda kwasababu tu ya ugomvi kati yake na Baba na kulipiza kisasi cha mimi kumkataa mwanae.

"Kwanini asingesema Medrick akuoe, mbona yule mnaendana nae iweje aseme uolewe na yeye mtu mzima. Mdogo wangu acha kila kitu kitokee ila usikubari kuolewa mimi naamini utetezi upo na haki kabla sijamalizia tulihisi mtu anakuja, Julieth alijifuta machozi haraka na kujitokeza mbele, Kumbe alikua ni askari kaja kumfuata wakaondoka,  Nilimuangalia mdogo wangu kwa uchungu na hasira mpaka akaishia zake, Uvimilivu ulinishinda, nilishindwa kuendelea kujificha nyuma ya pazia la ile sehemu, nilirudi chumbani kwa Binti Mfalme maana sikua na namna hata ningetaka kutoka bado ningeshikwa na walinzi,  Nilikaa kwenye kona chumbani kwa Witness huku nikifikilia ni jinsi gani tunapitia tabu kwasababu ya tamaa bado nasema Tamaa ni mbaya tena ni Mbaya.

Tamaa ya Baba yakutaka mimi niolewe na binti mfalme ili badae nifanye mapinduzi nitawale mimi ndiyo inayosababisha sisi kuangaika sasa na anaingia kwenye kifo.

Sikumbuki Nilikaa hapo kwa mda gani ila nilihisi mtu kanishika bega, hapo ndipo niliposhtuka toka Usingizini, "Upo vizuri yani unapata hadi mda wa kulala na kukoroma hapo" Witness aliongea kwa kejeri huku akienda kuketi, Nilikumbuka kua babaangu alikua anaenda kupata adhabu.

"Nambie Witness nini kimeendelea huko" Nilisogea haraka alipokua amesimama Witness

"Eh eh eeh ita hilo jina kwa heshima sio unaita tu kama mimi mwanao au i kwasababu huyo mdogo wako kakubari kua mke wa Baba basi unaniona mimi kama mwanao eeh? " Witness alikua amekuja na hasira tofauti na nilivyokua nimemzoea.

"Sasa skia mimi ni Binti Mfalme sio unaita tu Witness Witness, na huyo mdogo wako mimi siwezi kumwita ama mdogo kwanza niaibu gani hii jamani, Ni lazima nifanye kitu achane na Baba iwe juu au chini ya uwezo wangu Baba hawezi kuoa katoto kale hata kama anapewa bure" aliendelea kulalama.

"Haya nawewe nipishe, Shadrassa nifuate njee" aliongea huku akitoka nje kama kachanganyikiwa ivi daah hawa watoto wa wakubwa kazi ipo siyo kwa kejeri izii, Nilitoka ili kuchungulia anaenda wapi.

 

Itaendelea

Kesho Saa 12:00 Jion

 

Comments

Popular Posts