WITNESS - SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

SIMULIZI: WITNESS

 

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

"Ndiyo alikubari ili kuniokoa lakini mpaka ndoa ingefungwa ndio Mfalme angetoa dawa, Ndio ivyo nae alipigwa siku ya ndoa, ni bora Binti yangu asingekubari kuolewa na Mfalme maana alikubari kashinda ili kuniokoa ila sasa huu ushindi unakua na maumivu" Baba aliongea kwa tabu

Tunaendelea….

 

Nilibaki nikimuangalia Baba kwa huruma, alikua amekonda sana, "Baba kajaribu kuongea na Mfalme atakuonesha dawa ilipo hata kwa Ishara kwasababu kwasasa si hawezi tu kuongea"

"Kwani umetoka wapi Clement" Baba aliniuliza,

"Nimetoka mto Nkinzwa" nilidanganya

"Ooh Kwaiyo huna taarifa yoyote kijana wangu"

"Taharifa gani" niliuliza

"Ya kua Mfalme amekufa na wanakijiji wote wapo msibani"

"Mfalme amefariki?? "

Baba aliitikia kwa kutikisa kichwa huku machozi yanamtoka, nilikumbuka zile kauli za Winni mimi nilijua anaongea vile kwasababu mfalme ni mgonjwa kumbe amekufa,

"Mbona amekufa bila kukupa dawa Baba, mbona amekufa mapema. Nani kafanya vile au ni Winni" niliropoka mbele ya Baba,

"Winni hawezi kufanya ivyo"

" Kwani Baba unajua mi naongelea Winni gani wewe humfaham, Atakua ni yeye Baba kwasababu aliongea kwa kejeri kule mstuni.

"Clement nimekwambia Winni hawezi kufanya vile, Mfalme amekufa kwasababu ya ule mshale wa sumu aliokua amepigwa siku ya ndoa, Ule mshale ulikua na mchanganyiko wa sumu mbali mbali na kali ndio maana walishindwa kuitoa".  Aliongea Baba

" Eeh Baba wewe humjui Winni anambinu nyingi yule"

"Winni huyuhuyo unaemuongelea alijitaidi sana kunipa dawa na alinieleza baadhi ya vitu kuhusu wewe, Yule binti namfaham toka anazaliwa ni Binti Shujaa na mwenye moyo wa kipekee alipendwa sana na wanakijiji ila alibebeshwa kesi nzito na Baba yake"

"Sasa kama alibebeshwa kesi na Baba yake si alitaka kulipa kisasi yeye ndio ameua, Baba amemuua mapema ilibidi Mfalme aoneshe dawa kwanza"

"Winni Aliniambia ule mshale ulipigwa na kijana wa mfalme, pia Winni amenisaidia sana amenitaftia dawa mbalimbali pia alijitoa sadaka na kwenda katika Jumba la Mfalme ili kunitaftia dawa lakini alikosa, amepambana sana yule binti Miungu ya Nkinzwa ikamjalie maisha mazuri, pia najua ukalibu wenu kwasababu alinieleza jinsi mlivyokutana na mpaka sasa" alieleza Baba

"Ila usimuamini sana yule anaweza kutugeuka wanakijiji, Unajua ni Jinsi gani ananguvu anaweza kuua wanakijiji wote" Baba alitabasamu tu maana alijua jinsi gani kijana wake naongea ujinga.

"Mwanangu kama miungu itawasaidia basi naomba umuoe yule Binti Winni" Baba aliongea

"Khee! Baba umeshaanza hujui kua mimi ninamahusiano na Bella natarajia kumuoa siku si nyingi"

"Bella sio wako Clement "

"Unamaana gani? "

"Ndio maana nilisema unisamehe toka mwanzo mwanangu ila mimi nimkosaji kwako kijana wangu.  unajua nilipokua nakulazimisha umuoe binti Mfalme, Upande mwingine nilikua namlazimisha Medrick amuoe Bellath"

"Baba dah kwaiyo imekuaje mbona Bella ninae mpaka saivi"

"Medrick alifanikiwa kumteka Bella na baadae wewe ukakimbia mahusiano yao yalizidi kukomaa hakuna mtu aliekua anajua hilo zaidi yangu, Na baadae Bella aliweza kukutana kimwili na juzi Medrick ameniletea taharifa kua Bella anamimba yake na inamwezi inamaana ni kabla hujarudi aliipata hiyo mimba, Nisamehe mwanangu"

Baada ya Baba kumaliza kuongea nilianza kucheka, Nilicheka huku machozi yakinitoka, Nilicheka huku nikiipuuzia story ya uongo ya Baba na kuunda ukweli ndani ya moyo wangu, Nilicheka kicheko cha maumivu,

"Baba sasa Hii ilikuaje kwanini ulinifanyia ivi kwanini mlinisaliti"

Nilikumbuka siku Medrick alivyonitorosha katika adhabu ya Mfalme alisema nikubari kumuoa dada yake ili mipango yake iende sawa kumbe ilikua ni mipango ya kumchukua Bellath. Nilijikuta nalia kama mtoto mdogo, ndio maana Bellath alikua analia asubuhi nilivyokua natoka na Witness ni kama kuna kitu alitaka kunieleza, na ndiyo maana Witness alinicheka kwa dharau siku aliyoniambia Bella wangu anamimba, Sasa mbona Bella aliahidi kunipenda kama alikua anamahusiano na kijana wa Mfalme au ndiyo sababu ya Winni kunipa ahadi ya kulamba damu ya Bella ili kuweka kiapo kua hatuta achana hata Itokee nini kumbe Winni alijua hili jambo, Sasa kwanini Bella alikubari kukutana na mimi kimwili ile siku kama anajua mda siyo mrefu alikutana na kijana wa Mfalme dah!

Nilijikuta nikiwaza kwa kila kitu,

"Nisamehe mimi kijana wangu ila ni bora ukamuoa Winni yule ndiye Binti pekee anakufaa"

Yani hata sikutaka kumuelewa Baba kabisa kwanza nilihisi ni muongo ananidanganya

"Sasa itawezekaneje mbona Medrick anataka kumuoa Julieth mdogo wangu au Baba unanidanganya"

"Mwanangu basi kila kitu nimepoteza ushindi nilioutarajia utakamilika ila utakua ni ushindi wa maumivu"

"Ushindi gani Baba" nilimuuliza,

"Kama Julieth anaolewa na Medrick"

"Unamaana gani? "

Baba hakunijibu kitu alifumba macho yake na Kuutua chini mkono wake, niliutazama mkono wake na kuuweka vizuri, 

"Sasa unaamua kusinzia unaona na kuchosha, nijibu hilo swali moja tu" Nilimuambia huku nikimshika shika mkono.

Lakini nilishangaa kuona amebaki kimya nilimuangalia usoni wasiwasi ukaniingia nikasikilizi mapigo yake ya moyo hakuna nilichokisikia, nikajaribu kuyafumbua macho yake

"Baba Baba Babaaaaaa….

 

Itaendelea

Kesho Saa 12 Jioni


Comments

Popular Posts