WITNESS - SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

SIMULIZI: WITNESS

 

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

Niliondoka kwa Hasira sana safari yangu ilikua ni kwa mwanamfalme, nilikumbuka aliwai niambia kama anauwezo wa kuoa wote wawili, Mdogo wangu pamoja na Bella, na yule hua hatanii, Bado nilikua nampenda Bella licha ya kuambiwa anamimba ya Medrick.

Kama ni Mtoto atazaliwa tu na atakabiziwa kwa Baba yake ila Bella bado yupo katika maisha yangu, sizani kama mimba ikawa chanzo cha kuvunja uhusiano na upendo wetu, Bella ni wangu na atakua wangu daima.

Tunaendelea….

 

Nilifika nje ya lango la mfalme, nilipoomba kuingia ndani waliniambia kuwa siwezi kuingia humo ndani ikiwa sina utumishi wowote wala sababu za msingi.

"Lakini mnajua mimi nina uhusiano gani humu ndani, Mtambue mdogo wangu bado ni mke w mfalme, bado ni Malkia wa Nkinzwa hivyo ni haki yangu kuja humu tena nikalindwa na walinzi" nilijitetea,

"Tena wewe hata ungekua na shida gani amri imetolewa usiingie ndani ya Jumba hili bila amri ya Binti Mfalme"

Kumbe Witness ndiye alieniwekea kizuizi kuingia ndani, Mwanzo nilikua nikiingia bila shida yeyote ila sasa hivi nazuiliwa kwasababu yake,

"Ooh sawa naomba mniitie huyo Binti mfalme wenu"

Kabla mlinzi hajajibu chochote tulianza kusikia milio ya farasi iliyionekana kuja kwa kasi sana,

"Kuna ugeni wowote" Mlinzi alimuuliza mwenzie,

"Hatuna taarifa ya ugeni wowote" mwingine alijibu.

"Wambie ndani wajipange kwa chochote"

Wakati wakiwa wanapanga hayo ilisikika sauti ya mshale uliokua unakuja kwa nguvu, Ulienda kutua ndani ya Jumba la Kifalme, Walinzi walianza kugawanyika kwa kasi, Wengine waliingia ndani na wengine walikua wakitoka nje, Mimi nilitumia nafasi hiyohiyo kuingia ndani ya Jumba la Mfalme. Punde tu ilisikika kengere ya hatari ndani ya Jumba la Mfalme na tayari walinzi walisha jiandaa vyema kupambana.

Sauti za mishale mingine mitatu zilisikika, mushale hii ilionekana kwenda juu ya nga, "Mmh kwa utaalamu huu wa mishale huyu na hisi atakua ni Winni, bila shaka amekuja kwenye falme yake" nilikua nawaza huku nikiingia ndani zaidi ya Jumba la Mfalme.

"Haraka haraka izo unaelekea wapi kijana" Alikua ni Witness alisimama mbele yangu,

"Namtafuta Medrick kaka yako"

"Nani kakupa ruhusa ya kuingia geti kuu, au ndio umepitishwa njia za siri ili uje kuwachorea ramani hao watu wako"

"Nimekwambia nimekuja kwa ajiri ya Medrick, ivi Witness mbona huelewi lakini"

"Sielewi kwasababu umeingia tu tunasikia ugeni wa ghafla nje, kama Wakiwa ni Waasi wenzio wamekutuma je tutajuaje"

"Ooh unajua kufikiria Binti mfalme, kwaiyo unataka kufanya nini labda"

"Walinzi mkamateni huyu" Witness alitoa amri,

Walinzi walisogea ili kunimata,

"Muachane, asisogee mtu kumshika" Sauti nyingine ilitetea, Sauti ile ilikua ni ya Julieth.

"Walinzi nimesema mkamateni, ivi wewe unajeuri ndani humu ndani ya kujipa madaraka ivyo. Huna uwezo wa kubishana na amri yangu hata kidogo" Witness alimuendea Julieth kwa hasira.

Julieth aliishia tu kutabasamu, bila kujibu chochote.

"Si naongea na wewe, au unajiona kama Malkia humu ndani tambua Sikupendi Julieth na sitokupenda mpaka Kesho"

"Eeh inatosha sasa Witness unajua nawaangalia toka mda hapa sijui shida nini kati yenu, Clement umesema unashida na Bella wambie walinzi wakupeleke chumbani kwangu utamkuta. Na nyie tushuke chini kunahatari" Alikua ni Medrick, aliongea huku akishuka ngazi kuelekea katika kumbi ya kifalme.

 

Itaendelea

Kesho Saa 12 Jioni

Comments

Popular Posts