WITNESS - SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE

 

SIMULIZI: WITNESS

 

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE

"Eeh inatosha sasa Witness unajua nawaangalia toka mda hapa sijui shida nini kati yenu, Clement umesema unashida na Bella wambie walinzi wakupeleke chumbani kwangu utamkuta. Na nyie tushuke chini kunahatari" Alikua ni Medrick, aliongea huku akishuka ngazi kuelekea katika kumbi ya kifalme.

Tunaendelea…

 

Alikuja mlinzi akanichukua hadi chumba cha Medrick, aliniruhusu niingie ndani. Kwanza nilishangaa ni kwa jinsi gani Medrick aliniruhusu haraka namna ile.

Mlinzi alibaki nje akaniruhusu mimi niingie ndani, 

"Bellath" niliita kwa mshangao baada ya kuona Bellath amekaa kitandani kwa Medrick tena akiwa bila kitu zaidi ya Shuka tu.

"Bella umeniacha kweli mamaangu"

Jamani niliumia mfano hakuna, Mtu ninae mpenda namuona kitandani kwa Medrick tena na Shuka tu.

"Clement nimelazimishwa kuingia humu na sijafanya chochote na Medrick niamini"

"Acha kunidanganya Bella, Kwa hali huyo unasema hujafanya chochote na Medrick?  Unanichukuliaje Bella, Kwanini unanifanyia ivi. Na kwanini uliamua kubeba mimba ya Medrick au hunipendi Bella? "

Bella alibaki tu akilia pale Kitandani. Baada mda kidogo mlango uligongwa, aliingia kijakazi akiwa kabeba nguo mkononi.

"Samahani Binti, Kuna hatari nje unahitajika ubadili mavazi ili uwekwe sehemu salama" aliongea yule kijakazi,

"Waala msijari, Nguo zake alizokua amevaa zikwapi. Mpeni izo nitaondoka nae mimi"

“Lakini nje ni hatari"

"Nimesema nitaondoka nae mimi" niliongea kwa ukali.

Kijakazi yule alitua nguo chini nakuondoka,

"Unampango gani bella" nilimuuliza Bella alipokua akizichukua nguo zake nakuvaa.

"Nikuulize wewe, je bado Unanipenda"

Hili swali lilikua ni gumu kwangu, kusema ukweli hadi kwa wakati ule sikujua kama nilikua nampenda Bella au laah, yani moyo wangu haukuchagua lipi jibu sahihi hadi kufikia pale.

Nilishtuka mtu akinishika bega,

"Swali ni gumu kwako eeh, najua kila kitu nimakosa yangu Clement. Mimi nilijua nakutaftia ushindi katika ile kesi yako. Nilijua kwa kufanya vile na Medrick labda ungekua huru lakini yametokea haya.  Huu ushindi umekua wa maumivu" alikua ni Bella,

"Haya yote ni Makosa ya Baba, yeye ndiye aliemtuma Medrick kwako. Lakini hukutakiwa kufanya ivyo Bella, Wazee wakiamua kitu kuhusu mimba yako si nitakukosa"

"Clement ivi ni kweli bado unanipenda"

Nilibaki kimya nikimuangalia Bella,

"Kama unanipenda basi kubari kuongozana na mimi"

Bella alinipa mkono na mimi nikaupokea, Bella aliangalia eneo lile tayari askari walikua wametoka,

"Lakini uliambiwa inabidi uwekwe katika chumba salama, ivi unadhani. Askari watakua mbali? " nilimuuliza Bella

"Sijari kuhusu hilo" Bella alinishka mkono, tukaanza kukimbia.

Lakini hatukufika mbali, tulisikia sauti ya mshale na punde si punde Bella alianza kulegea na kwenda chini,

Niliangalia nyuma, Witness alikua ameshika Mishale anakuja eneo lile tulilopo mimi na Bella.

 

Itaendelea

Kesho Saa 12 Jioni

 

Comments

Popular Posts