WITNESS - SEHEMU YA MWISHO
SEHEMU
YA MWISHO
"Kumbe unaumia eeh, huu ndio ushindi
wako. Acha upate ushindi wa yote tena ushindi wako uwe wa maumivu, pamoja na wewe
halafu wambie hawa waasi wenzio waondoke hapa kwa amani. Witness aliongea huku
akinioneshea mimi, Nilisogea karibu yake na kumpiga kibao, Witness kua mbele
yangu niliona ananijaza ghadhabu.
Witness
alichukua mshale nakutaka kunipiga lakini Winni aliuzuia mshale ule.
Tunaendekea…
Witness pamoja na dada yake Winni
walianza kupigana, ugomvi wao ulikua ni mkubwa tu, Witness aliwapanga vizuri
watu wake,
Wazee waliamuru baadhi ya raia
walio ndani ya Jumba la kifalme walikwenda kujificha sehemu sahihi maana
witness alionekana kuwa na hasira sana, watu walianza kukimbia huku witness
akizidi kugombana na Winni, Watu wakiwa bize kutafuta sehemu ya kujificha, tulisikia
sauti ya Witness aliyekua akilia kwa maumivu, watu wote waligeuka ili kuangalia
lile.
****
Dada yake Bella aliyekua amepata taarifa
juu mdogo wake kupigwa mshale na Witness, Dada yake Bella alikuja katika eneo
la mapambano bado alionekana ni mtu mwenye majonzi makubwa na alionekana alilia
mda mrefu sana, Alimuona Witness akiwa katika mapambano makubwa aliyokua akipambana
na Winni alisimama nyuma ya Witness na kumchoma kisu.
Watu wote hawakuamini kilicho
tokea, Wapiganaji wote wa Witness pamoja na Winni waliacha kupigina, Dada yake
Bella aliichomoa kisu nakutaka kumchoma tena Witness lakini mlinzi wa Witness
aliwahi humpiga mshale.
Witness pamoja na dada yake Bella
walitolewa ile sehemu. Miili watu watatu,Witness, Bella pamoja na dada yake ilizikwa sehemu karibu
na kaburi la Mfalme pamoja na Baba.
Wanankinzwa walibaki na simanzi kwa
ile lililotokea, siwezi kueleza kwa Jinsi nilivyokua na huzuni ya kumpoteza
mpenzi wangu Bella.
Winni alikua karibu na mimi kwa kipindi
chote hicho, niliishi ndani ya Jumba la kifalme pamoja na Winni.
BAADA
YA MIEZI MITATU
Ndani ya mwaka tu lakini kila kitu
kimeharibika, Ufalme umebaki na majonzi pamoja na maumivu.
Wazee wa baraza walikaa pamoja na kuamua
jambo kuhusu ufalme, Medrick aliruhusiwa kuoa ili ufalme ubaki na kiongozi na mke
pekee wa kumuoa alikua ni Julieth mdogo wangu.
Baada ya ndoa ya Medrick na Julieth
ufalme ulikabidhiwa kwao lakini mtu mkubwa wa kulisimamia alikua ni Winni. Ushujaa,
uhodari na utu wa Winni tangu akiwa mdogo ndio uliomfanya akubalike sana kupendwa
sana na wanakijiji, Sikutaka kuingia tena katika mahusiano, ila mtu pekee
aliyekua karibu yangu pia alikua akinifundisha baadhi ya vitu, Na Jinsi ya kupambana
alikua ni Winni.
MWISHO
Comments
Post a Comment