WITNESS - SEHEMU YA KUMI NA TISA
SIMULIZI: WITNESS
SEHEMU YA KUMI NA TISA
"Sasa skia mimi ni Binti Mfalme sio unaita tu Witness Witness, na huyo mdogo wako mimi siwezi kumwita ama mdogo kwanza niaibu gani hii jamani, Ni lazima nifanye kitu achane na Baba iwe juu au chini ya uwezo wangu Baba hawezi kuoa katoto kale hata kama anapewa bure" aliendelea kulalama.
"Haya nawewe nipishe, Shadrassa nifuate njee" aliongea huku akitoka nje kama kachanganyikiwa ivi daah hawa watoto wa wakubwa kazi ipo siyo kwa kejeri izii, Nilitoka ili kuchungulia anaenda wapi.
Tunaendelea…
"Shadrassa tafuta njia yeyote huyu Binti asiolewe na Baba hata kama katakufa potelea kote ila hii aibu siitaki kuisikia kwa vyovyote vile" aliongea Witness
"Lakini Binti Mfalme"
"Hakuna cha lakini Shadrassa kumbuka mimi ndio mkubwa wako" Binti Mfalme alimaliza kuongea na kurudi ndani, Mimi nikarudi haraka nilipokua nimekaa kama sijasikia kitu.
Alifika kujitupa kitandani kwake, alikaa kwa mda kisha akainuka na kunifuata nilipo, "Baba ako amepona sasa kwasababu ya ujinga wa mdogo wako, ivi mtoto mdogo yule atakubalije kua mke wa baba yangu si aibu hii eti Clement, haya fanya kitu ili mdogo wako aachane na baba "
"Nitafanya nini mimi Binti Mfalme, Kumbuka sina kauli mbele ya Mfalme"
"Huna kauli, huna kauli eeh? Ulipokataa kunioa ile kauli Uliitoa wapi"
Nilibaki nimejiinamia chini nisijue nijibu nini mwanaume mimi, kumbe nae Witness nimkali kiasi hiki duuh, "Sasa sikia kama usipofanya ivyo nitasema mbele ya ufalme kua wewe unashirikiana na Waasi na uliwai pambana na mimi pia kumbuka Ufalme unajua wewe na wenzio mliwaua walinzi wa Medrick na mlimjeuri Medrick nusu ya kumuua"
Baada ya kumaliza kuongea Witness alijilaza tena kitandani kwake.
Wiki tatu ziliisha huku mimi nikiwa ndani ya Jumba la kifalme tena kwenye chumba cha Witness bila watu kujua, Nilikula chakula alicholetewa Binti mfalme na kulala katika chumba cha kuhifadhia vitabu vya kumbukumbu na baadhi ya vitu vya Binti Mfalme.
Siku iliyopangwa kwa ajiri ya ndoa ya mdogo wangu pamoja na Mfalme Ilifika, Wanakijiji wote walikusanyika ili kushuhudia tukio hilo, Sikua na imani hata kidogo siku hiyo nilijua kwa vyovyote vile naweza kufa mimi au kufa mdogo wangu, kwasababu nilimskia Witness akimwambia Shadrassa afanye chochote hata kama ni Kifo iwe tu ili Julieth asiolewe na Mfalme.
Shughuri ilianza, Wanakijiji walicheza ngoma mbali mbali kwa furaha, kuna wengine hawakua na furaha kwa Jambo kama lile ila wangefanyaje kama Mfalme ameshaamua hakuna aliyekua na kauli kwa Mfalme hata washauri wake walikua wakimwogopa Mfalme yule, Nilijichanganya na watu huku nikiwa nimejifunika watu wasinitambue, Nikiwa nimetulia sehemu nilimuona Chande akipita na rafiki zake nilitamani hata nimwite anisaidie katika hili ila Bella alishanisimulia kila kitu hivyo sikuweza kumwita,
Baada ya mida wazo la kumfuata Chande likanijia, nilianza kutembea kwa umakini huku nikiwa nimeificha sura yangu nisionwe na walinzi, Chande aliingia kwenye chumba kimojawapo bila kizuwizi kutoka kwa walinzi, Baada ya muda alitoka huku akiwa kamshikilia Bella Begani, walitembea kuelekea upande wa jiko ila haikua jikoni na mimi nikaanza kufuata kwa nyuma, Alimtua Bella chini na kushikiria kiuno chake
"Eeh mwanamke mzito wewe khaa" aliongea kwa kejeri
"Hutaki kueleza Clement yupo wapi na nimepata taarifa unatapika ovyo kwenye chumba cha adhabu"
Mda wote Bella alikua kimya tu, kwa mda wa Wiki tatu tu tayari Bella alianza kuzohofika. Pale pale alipita Julieth ambaye alikua anasubiriwa kuapishwa kua Malkia alikua ameongozana na walinzi wake, akawaonesha ishara walinzi kua wakae pembeni.
"Kwanini unayafanya yote haya Chande? Huyu si alikua kama shemeji yako kwanini hukumheshimu kwa hilo? " Aliongea Julieth kwa utaratibu
"Shemeji? et Shemeji, Mbona wewe umekubari kuolewa na mfalme mtu mkubwa kama Baba yako bila kujari chochote wala kujua kama sio heshima, Unadhani mimi sitaki kumuoa Binti mfalme halafu ngoja nikwambie kwasababu mimi nilikua ni rafiki mkubwa wa Clement hivyo nimepata nafasi kubwa ya kumkamata Clement na kumtwaa Binti mfalme hata hawa vijana wengine wanajiaangaisha tu"
"Kwa hiyo upo tayari kumuangamiza rafiki yako kisa binti Mfalme na vipi akikutaa kumbuka yeye alimpenda Clement sizani kama atakukubari wewe"
"Hayo mengine niachie mimi na wewe Bella utasema Clement alipokimbilia ile siku, nitakupiga bila kujari chochote " Chande aliongea huku akimgeukia Bella.
"Chande kumbuka mimi nina nafasi kubwa kuliko wewe humu ndani, hata kama mtanidharau ila naweza fanya chochote hata kama sijaapishwa bado. Mrudishe binti mahari pake alafu mimi nawewe tutamalizana" Julieth aliongea kwa kukasilika hata mimi sijawai kumuona akiwa ivi kabla licha ya kua mdogo wangu.
"Khee yani kidogo tu ivyo unataka kunipanda kichwani et kisa namfokea Bella, sikiliza Julieth hata mimi na wewe tutamalizana pindi nikimuoa Binti mfalme kikubwa si madaraka eeeh! na kila mtu anayataka. Wewe nenda tu huko kaolewe na mzee si umekubali mwenyewe umeona kijijini hapa hakuna vijana"
Julieth alimpiga Chande kofi bila kujali chochote hadi walinzi wakasogea kujua nini shida, "Mrudisheni huyu binti mahari pake sasa hivi" Julieth aliamuru Bella arudishwe, Alimuacha Chande akiwa kashikiria shavu lake.
"Mmh yani kidogo tu ivi yameibuka mambo makubwa, Kumbe Chande ndio kabadilika ivi dah" Niliwaza huku nikiwa nimejibana kwenye Kona.
Nikiwa hapo nilihisi kushikwa bega na mtu nyuma, sikutaka kugeuka kwa haraka maana nilikua na hofu sana, "Vipi umeona kilichotokea hapo yani hakuna hata mmoja mwenye madaraka lakini wameanza kuleteana fujo vipi kama wakapata madaraka si watageuza Jumba la Mfalme kua uwanja wa Vita" kumbe alikua ni binti mfalme
"Hata ivi sizani kama hii nafasi mdogo wangu anaitaka na anaonekana kuumia sana kuolewa na Baba yako hata angekua mtu mwingine angeumia, pia si ulisema nikamkataze Julieth kuolewa na Baba yako yani nikazuie ndoa sasa mimi nakwambia sitafanya ivyo acha tu aolewe labda anaweza niokoa kwa kifo kilichombele yangu kwasababu hata nikizuia bado tu tutakufa ila acha yeye apone mimi nife"
Niliongea kwa ujasiri ambao hadi leo sijui niliutoa wapi ujasili Ule, "Unamaana gani? " Witness aliniuliza
"Kama nikimzuia Julieth kufunga Ndoa basi jua nitakua matatizoni, na hata kama nisipoiziuia bado ninakosa la kumjeruhi mwana mfalme na kuwaua walinzi wake kama ulivyokua umeniambia kwaiyo acha Julieth afunge ndoa ili atuokoe sisi,pia nilisikia ukimwambia Shadrassa azuie ndoa ya mdogo wangu hata kama ni kwa Kifo, Sasa na mimi nakwambia kama mdogo wangu akizurika basi jua utakua matatizoni Witness"
"Ivi unajua unaongea na nani wewe? Au umechangakiwa? " Witness aliuliza kwa kuhamaki.
"Naongea na wewe WITNESS, Si unaona kama mimi nashirikiana na waasi basi acha niwe muasi mbele yako"
Nikaondoka na kwenda sehemu iliyoandaliwa kwaajiri ya sherehe hadi mda huo nilikua nimejifunika usoni.
NINI KITAJIRI JULIETH ATAKUBALI KUOLEWA NA MFALME?
Itaendelea
Kesho Saa 12:00 Jioni
Comments
Post a Comment