WITNESS - SEHEMU YA THELATHINI
SEHEMU
YA THELATHINI
Taratibu alianza kulegea kabla
hajamaliza kauli yake, na mwisho aliacha kabisa kutoa pumzi. alikua ametuacha Bella wangu,
Medrick aliangalia sehemu ambako
mshale ulikua umetokea, alikua ni WITNESS, Witness ndiye aliyemuua Bella,
Tunaendelea…
Medrick alipiga kelele kwa nguvu
huku akilitaja jina la Witness, Witness alishuka chini, bila hata wasiwasi
wowote. Medrick aliukabidhi mwili kwa mlinzi na kuanza kumfuata Witness kwa
Hasira, lakini Wazee wa Baraza walimzuia. Mda wote huo Winni pamoja na kundi lake
walikua wamekaa tu wakiangalia matukio yalio kuwa yanaendelea,
"Witness nimekufanyia nini
mimi au nimekukosea nini mimi hadi unafanya haya, kwanini umemuua mwanangu na mama
yake" Medrick aliongea kwa hasira,
"Nimefanya ivyo ili haya maumivu
tuyapate wote, Umemuua Baba yangu sijafanya kitu, unautaka ufalme sijafanya
kitu, lakini pia unataka kuwasamehe waasi na kuwaruhusu kurudi katika hii
himaya, hicho kitu ni zaidi ya maumivu"
"Kwaiyo maana yako ni nini, na
ndio maana umenifanyia ivi Witness, lazima nitanya kitu Witness kwaajili
yako" Medrick aliongea kwa hasira
"Medrick unataka kunifanya
nini wewe, Ivi unajiona uko sawa kwa haya unayoyafanya, Umemuua Baba kwa Mikono
yako hakuna adhabu yoyote umepewa, Umempa Binti mimba kabla ya Ndoa, Umevunja
ndoa ya Baba, Hakuna lililofanyika juu yako, Leo wanakuja adui ndani et unataka
uwakalibishe kwa amani, Siku zote walikua wakipambana na sisi halafu leo unataka
kuwapokea"
"Nakuuliza kwaiyo hiyo ndiyo
sababu iliyofanya Ukaniulia mwanangu tumboni Witness, hiyo ndiyo sababu
nakuuliza" Medrick aliongea huku akiwa mikononi mwa wazee.
"Kumbe unaumia eeh, huu ndio ushindi
wako. Acha upate ushindi wa yote tena ushindi wako uwe wa maumivu, pamoja na wewe
halafu wambie hawa waasi wenzio waondoke hapa kwa amani. Witness aliongea huku
akinioneshea mimi, Nilisogea karibu yake na kumpiga kibao, Witness kua mbele
yangu niliona ananijaza ghadhabu.
Witness alichukua mshale nakutaka
kunipiga lakini Winni aliuzuia mshale ule
Itaendelea
Kesho Saa
12 Jioni
Tupo sambamba
ReplyDelete