WITNESS - SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

SIMULIZI: WITNESS

 

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

Lakini nilishangaa kuona amebaki kimya nilimuangalia usoni wasiwasi ukaniingia nikasikilizi mapigo yake ya moyo hakuna nilichokisikia, nikajaribu kuyafumbua macho yake

“Baba-- Baba—Babaaa…

Tunaendelea….

 

"Baba-- Baba-- Babaaa" niliita kwa sauti sana nilitambua Baba yangu alikua ameshakufa, Nilihisi kila kitu kizito kwangu, hata kwenda kumtafta mama nilishindwa, Nilianza kumtikisa labda alikua ananitania aliona namuuliza sana maswali lakini haikua ivyo, Baba yangu alikua amekufa yani ndio alienda ivyo, aliondoka siku moja na Mfalme. Baba alienda kumsindikiza Mfalme..

Mazishi ya Baba angu na Mfalme yaliisha, Julieth akiwa kama Malkia wa Nkinzwa aliamuru watu hawa wazikwe sehemu nje ya Jumba la kifalme, Wote walizikwa pamoja misiba yote ilifanyika nyumbani kwa Mfalme. Zilibaki simanzi katika kijiji cha Nkinzwa kwa Kumpoteza Mfalme wao lakini kwa wengine ilikua furaha kwasababu aliwatesa sana Mfalme yule, Pia hata katika familia ya Mzee Mzenga tulikua na huzuni ya kuondokewa na Baba yetu mpendwa MzeeMzenga.

Julieth akiwa kama Malkia wa Nkinzwa aliondokewa na Mume wake ambae ni Mfalme pamoja na Baba yake (yetu).

 

*****

Miezi miwili Iliisha na majonzi yalikua yamepungua kijijini Nkinzwa

Tafaharuku nyingine ilianza, baadhi ya wazee wa Nkinzwa walianza kusema Julieth atafute Shujaa mwingine wakumuoa ili apatikane mwanaume shujaa wa kukirithi kiti cha ufalme,  wengine walisema kwakua Mfalme hakushiriki chochote na Julieth basi kunauwezekano wa kuivunja ndoa hiyo na kumuachia Medrick maamuzi pia wapo waliosema ufalme unatakiwa kwenda katika ukoo mwingine kwasababu Mfalme hakutangaza Kuurithisha ufalme ule kwa kijana wake yeyote. 

Wakati waamuzi wakijiji wakiwa katika mdaharo huo wa nani awe mtawala wa Nkinzwa, Medrick alichukua maamuzi ya kupiga kengere na kuwakusanya wanakijiji wote, Hakua na Jambo kubwa la Kutueleza wala hakutaka kuchukua mda mwingi kama alivyokua akifanya marehemu Baba yake,

"Naomba mnisamehe sana wanakijiji wa Nkinzwa kwa maamuzi haya niliyoyachukua, pia samahani kubwa iende kwa wazee wa Baraza kwa kutowashirikisha maamuzi yangu niliyayachagua" Medrick aliongea kisha akatuangalia wanakijiji pamoja na wazee, kisha akaendelea.

"Najua itakua ni ghafla pia itakua Inashangaza sana ila napenda kuwaambia wiki ijayo natarajia kumuoa Julieth binti wa marehemu mzee Mzenga, Ningependa Julieth ujiandae kwa ndoa hii" Medrick alimalizia kwa kumuangalia Julieth. Julieth alisimama ili aseme kitu lakini Medrick aliwahi kumshika mkono na kuondoka nae mahari pale,

 

Nilielewa jinsi mdogo wangu alivyokua anampenda Medrick tangu mwanzo lakini sijui kama anakubariana na hii ndoa ikiwa Medrick alikwisha mpa mimba mpenzi wangu Bellath na Julieth alishafunga ndoa na Mfalme ambayo haijamaliza hata Miezi 6.

Watu walianza minon'gono ya chini chini baada ya Medrick kuondoka na Julieth, Baada ya mda alisimama Witness na kuwaamuru watu watawanyike, nae hakutaka mambo mengi akaanza kuondoka kwa hasira.

Wazo la kwenda ndani ya Jumba la kifalme likanijia, nilihitaji kumuona mdogo wangu sikua nashida katika kuingia ndani kwasababu tayari nilikwisha kutambulika. nikiwa sina hili wala lile nilihisi mtu akinishika mkono, niligeuka kumuangalia mtu huyo alikua ni nani.

"Samahani sana rafiki angu, naomba tuongee japo kidogo" Alikua ni chande ndiye aliyenishika mkono.

"Ninaharaka kidogo unaweza kuniacha, tutaongea baadae" nilimjibu,

"Najua fika kua unaharaka ila tambua kua sisi ni marafiki"

"Naelewa, yani kila kitu naelewa vipi kuna chochote kipya cha kunieleza"

Niliona chande akiniangalia tu bila kusema Chochote, Nilijua dhamira yake ilikua nikuomba msamaha Ila sikua tayari kumpa nafasi kama hiyo nyoka mwenye vichwa viwili.

Niliingia ndani ya Jengo la Mfalme moja kwa moja katika chumba cha mdogo wangu,

Nilipokua mlangoni Askari wa Jumba hilo walianza kunizuia kuingia ndani lakini badae Mdogo wangu Julieth alitoka huku akiwa ameambatana na Medrick, alionekana hayuko sawa,

"Julieth" niliongea huku Nilitaka kwenda kumkumbatia lakini Medrick akasimama kati yetu

Huruhusiwi kufanya ivyo kwa sasa" aliongea Medrick

"Kwanini?  hujui kama ni mdogo wangu"

"Lakini pia tambua ni mke wangu mtarajiwa"

"Ooh mke mimi pia najua hilo" nilimjibu huku nikimshika Julieth mkono nikamsogeza kando kidogo upande niliokua mimi.

"Hivi wewe kipi usichoelewa, na ni nani amekupa ruhusa ya kuingia ndani ya Jumba la Kifalme bila ruhusa au siku hizi mmegeuza Jumba la kifalme kama choo au sehemu ya ngoma. Julieth hawezi kuongea na mtu mwingine bila ruhusa kutoka kwangu"

"Ruhusa?? Et ruhusa, ruhusa gani unayoiongelea, halafu jua sijaja kwa ugomvi nakuheshima mwana Mfalme"

"Kama ingekua ni heshima basi mpaka kufikia mda huu ungeshikwa na walinzi kwa kutokunipa heshima ila nimezuia jambo hili kutokea. Naomba umuheshimu mke wangu mtarajiwa usimchukulie kama dada yako ila mchukulie kama Malkia wa Nkinzwa mtarajiwa"

Nilitamani kucheka Medrick alipokua akiongea, nilimuona kama mtu asiyejua kuyatimiza yale anayoyaitaji kutimizwa,

"Ooh kumbe unaijua thamani ya mke si ndio, kwanini hukumheshimu Bella wangu wakati ulijua ni mke wangu mtarajiwa"

 

Itaendelea

Kesho Saa 12 Jioni


Comments

Popular Posts