WITNESS - SEHEMU YA ISHIRINI
SEHEMU YA ISHIRINI
Naongea na wewe Witness, si unaona kama mimi nashirikiana na waasi basi acha niwe muasi mbele yako" Niliondoka na kwenda sehemu iliyoandaliwa kwaajiri ya sherehe hadi mda huo nilikua nimejifunika usoni.
Tunaendelea…
Taratibu zingine za kindoa zilifanyika, watu walikula vizuri na kunywa,Siku hiyo niliweza kumuona mama alikua amekonda pia macho yake hayakuacha kutoa machozi wamama watatu walikua pembeni yake kama wanamfariji, Ulifika mda wa Julieth na Mfalme kuapa kiapo chao cha maisha.
Kama kawaida ya kijiji pamoja na sheria za kijiji, taratibu za kimila zilifanyika, Maji yakapitishwa ili waweze kuapa kiapo chao, Julieth alinawa huku akiwa anaangalia chini nilihisi labda alikua akilia,
Ilifika wakati wa Mfalme kunawa.Yeye aliwaangalia kwanza wanakijiji wake na kuwapungia mkono, kisha akaangalia upande wa Baraza la wazee akatoa heshima, akaitoa mikono yake na kunawa alipomaliza kufanya ivyo tulishangaa Mfalme akianguka chini huku akipiga kelele za maumivu.
"Mfalme" Witness alipiga kelele huku akimfuata baba yake pale chini,
Baadhi ya viongozi walipatwa mashaka kwa jambo lile mfalme alikua amechomwa mkuki na tayari alikua ametulia hakuweza hata kupiga kelele. Baadhi ya wanakijiji tayari walishaanza kutawanyika kwa Woga. Taratibu ya kumuondoa mfalme pale ilifanikiwa, walinzi walianza kuzunguka pande ambazo mshale umetokea kama watamuona mhusika yeyote. Nilijua yule atakua ni Winni kwasababu aliapa kulipa kisasi kwa Kifo cha mama ake na alisema ni lazima angemuua mfalme na angewaeleza wanakijiji wote ukweli juu ya mama yake ili kujisafisha kwa wanakijiji.
Zilipita siku tatu bila kujua chochote kinachoendelea kwa Mfalme, Kila tabibu kutoka Milimani hata Vijiji vya jirani waliitwa kwaajiri ya kumtibu mfalme. Ilisemekana Mfalme alipigwa mshale wenye sumu na hiyo sumu nikazi kuitoa mwilini mwake.
Julieth mdogo wangu aliapishwa kua Malkia kwasababu tayari walishakubariana na kunawa pamoja, Witness hakukubariana kabisa na ile ndoa alianza kupambana na Julieth vita ya chini kwa chini. Nilipata taharifa kua wazazi wangu wamerudishwa nyumbani lakini Bella anapatiwa matibabu ya mguu wake pia alionekana ni mjamzito wa mwezi mmoja. Nilifurahi kusikia vile kwasababu nilijua ile mimba ni yangu kwa vyovyote vile, Niliamua kuondoka katika Jumba la kifalme kwasababu hakuna ninachokisubiri humo, nilijianda vizuri tayari kwa kutoka lakini nilipofika mlangoni nilikutana na Witness alikua amenizuia mlangoni, "Unaenda wapi Clement " aliniuliza,
"Kila kitu kimeisha Witness, acha niende Nyumbani"
"Uende nyumbani? Nani kakupa hiyo ruhusa? Kumbuka wewe ni mfungwa kama wafungwa wengine tu umesahau kosa lako la kunikataa na ukatoroka? "
"Lakini kumbuka mdogo wangu ni Malkia hapa hivyo ninahaki ya kuondoka humu, hawezi kubari ukanipa adhabu kwaiyo ni bora ungeniacha niende Binti Mfalme"
Witness alianza kucheka, alicheka sana tena kwa dharau
"Aliekwambia kazi ya Malkia ni kuzuia wakosaji kupata adhabu ni nani? Hii imeshaandikwa na mfalme ni lazima itekelezwe hata mimi lazima nikupe adhabu kwasababu unashirikiana na waasi tena kesho naenda huko kawape habari yao" Witness alimaliza kuongea akaanza tena kucheka, alinicheka kwa kudhihaki.
"Haya rudi ndani haraka, pia nilisikia mpenzi wako anamimba ni vizuri ila nitahakikisha mwana hamjui Baba hata akimjua atamjua kwa historia ya Waasi"
"Unamaanisha nini Witness" niliuliza kwa upole
"Nitahakikisha naua waasi wote au nitawafanyia kitu ambacho hawawezi kusahau ikiwemo na Malkia wao mpya wa Nkizwa" Alijibu Witness
"sikia Binti Mfalme bado nipo kwenye msimamo wangu, Yani mdogo wangu akipata matatizo utawajibika kwa hili"
"Yani upo ndani kwangu lakini bado unanijibu jeuri hivi hujui ni kiasi gani nakuchukia wewe" Witness aliongea na kutaka kuja kupambana na mimi. Mtu alikuja mbele na kumzuia witness,
"Jaribu kutuliza hasira zako Witness, Kumbuka huyu mtu wewe ndie uliyemhifadhi kwa malengo yako mwenyewe"
Yarabi kumbe alikua ni Medrick, siwezi elezea kwa Jinsi nilivyokua namuogopa huyu mtu, Hakua mtu wakujioneshaonesha mbele ya watu, Mda wote alipenda kua chumbani kwake lakini nilikua namuogopa hakuna mfano, Sijui alijuaje kama mimi nipo ndani kwa Binti Mfalme.
"Pia inabidi ujue huu uovu ni wa Baba kwasababu yeye ndiye aliyemtaka binti kama yule kwaiyo hunasababu ya kupambana na yule Binti" aliendelea kuongea Medrick huku akimrudisha dada yake Witness Kwenye kiti na kumketisha
"Hii adhabu ya Mfalme kuugulia kitandani inamfaa kuliko kulala kitanda kimoja na yule binti. Pia usipambane na yule binti kwasababu ni mke wangu mtarajiwa na nimempenda kuliko kawaida" Medrick alitaka kuondoka lakini Witness akamzuia, "Wewe umesamaje, unataka kumuoa Julieth yaani kale kabinti ukaoe wewe? Hujui ameshafunga ndoa na Baba" Witness alihamaki
"Wamefunga ndoa lakini hawajafanya chochote, hata ivyo Mfalme anabahati sana Yule ilibidi Nimuue kabisa. Mimi namwambia nimempenda binti yeye anaenda kumuoa kabisa si aibu hiyo, Nimesema nitamuoa yule Binti"
"Kwaiyo Medrick wewe ndiye ulimshambulia Mfalme? " Witness alimuuliza.
Medrick alitabasam….
Itaenendelea
Kesho Saa 12:00 Jioni
Comments
Post a Comment